Albino waipa kisogo Serikali

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
SERIKALI kutokuwa na mkakati endelevu wa kupambana na matukio ya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ndiyo chanzo cha kutotokomea kwa ukatili huo, anaandika Regina Mkonde.

Hayo yamesemwa na Musa Kabimba, Katibu Mkuu wa Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijijini Dar es Salaam kuelekea siku ya Kimataifa ya kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu ualbino inayoazimishwa Juni 13 kila mwaka.

“Sisi watu wenye ualbino nchini haturidhiki na kasi ya kuimarisha usalama wetu nchini kutokana na kutkuwepo kwa mkakati endelevu wa serikali katika kupambana na vitendo vya kikatili dhidi yetu,” amesema Kabimba.

Amesema, viongozi wa serikali mara kwa mara huonesha jitihada za kupambana na wahusika pindi zinapotokea taarifa za matendo ya kikatili na kwamba, baada ya muda huacha kuendeleza jitihada za kutokomeza matendo hayo.

“Kuna operesheni nyingi zilizosimamiwa na serikali na kufanikiwa, kwa nini matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino hayasimamiwi ipasavyo, na kama kuna mkakati wa kutokomeza matukio hayo halafu hakuna mafanikio kama si jipu ni kitu gani?” amehoji.

Amesisitiza kuwa, mikakati madhubuti ya kulinda maalbino haipo na kama ipo wanaifahamu baadhi ya wakubwa ambao hawataki kuidhihirisha.

“Kati ya albino kumi, tisa kati yao wana ugonjwa wa kansa ya ngozi kutokana na kushindwa mudu gharama za mafuta yanayozuia athari za mionzi ya jua, jambo la kusikitisha asilimia 75 ya albino wako vijijini ambako dawa hizo haziwafikii kwa urahisi,” amesema.

Nemes Temba, Mwenyekiti wa TAS amesema kuwa serikali haina budi kuongeza bajeti ya watu wenye ualbino pamoja na kutoa huduma za bure kwao kama inavyotolewa kwa watu wenye matatizo mengine.

“Hapa nchini kuna watu zaidi ya milioni mbili ambao huenda kliniki kupata dawa za ARV bure tena zikiwa na gharama kubwa kuliko dawa za watu wenye ualbino ambao wako wachache, kilichopo ni kwamba serikali haijatoa kipaumbele kwetu,” amesema na kuongeza.

“Ila ninaamini kwa kuwa imeanza kutenga walau bajeti ndogo kwa ajili ya watu wenye ulemavu, ipo siku watatambua umuhimu wetu na kutuongezea bajeti kwa kuwa itasaidia kupunguza idadi ya vifo.”

Katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuliitakayofanyika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Aidha TAS kimetoa wito kwa jamii wa kutotumia jina la Zeruzeru na au walemavu wa ngozi kwa kuwa linalenga ubaguzi pamoja na kutofafanua ipasavyo hali yao kutokana na kwamba wao si walemavu bali kuna madini waliyokosa.


Chanzo: Mwanahalisi
 
Back
Top Bottom