Albino bado wanauawa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Mauaji ya albino bado yanaendelea
Tangu BBC ilipofichua kwamba waganga wa kienyeji au wa jadi ndio wanaochochea mauaji hayo Julai 21 mwaka jana idadi ya watu waliouawa imeongezeka toka watu 27 hadi 52.
Hii ni pamoja na mauaji matatu yaliyofanywa mapema mwezi huu katika kipindi cha wiki moja - mawili katika jiji la Mwanza Kaskazini mwa Tanzania na moja katika mkoa wa Tabora Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, na pia albino aliyepigwa dafrau na kuachwa afariki dunia katika hali ya utatanishi katika mkoa wa Mara, Kaskazini mwa nchi.
Maisha ya wasi wasi
Vitisho vimezikumba baadhi ya familia katika jiji la Dar es Salaam baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba zao katika majira ya usiku.
Tunaweza kukiangalia kipindi hiki cha mwaka mmoja katika sehemu kuu mbili. Hali ya mauaji ya albino na hatua zilizochukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo vya ukatili kwa imani za uchawi.
Usalama hakuna
Maelfu ya watu wenye ulemavu wa ngozi wamejikuta wakibadili kabisa utaratibu wa maisha yao. Mauaji haya yalipoanza yalikuwa yanatokea maeneo ya vijijni.
Lakini sasa vitisho vimewakumba hata albino wanaoishi kwenye maeneo ya mijini na hata jijini Dar es Salaam.
"Wakimbizi ndani ya nchi"
Kuna wale waliotafuta hifadhi katika maeneo ya serikali ya kuomba ulinzi, baadhi ya wazazi wamelazimika kuwaacha watoto wao katika shule za bweni za wanafunzi wenye ulemavu au vituo vya wazee wasiojiweza.
Hii nimeshuhudia katika utafiti wangu wa hivi karibuni kwenye kambi ambazo sitazitaja kwa sababu za kiusalama.
"Ulinzi imara"
Winifrida Rutatiro, na mwanae wa kiume Lucas Rudayira walikimbia katika kijiji chao huko Usagara, mkoa wa Mwanza baada ya Nyerere Rutatiro kuuawa kikatili mwezi Julai mwaka jana na wauaji waliokimbia na miguu yake miwili.
Wanakijiji walianzisha ulinzi wa jadi wa sungusungu na kuwalinda lakini baada ya muda waliacha na kuwashauri waondoke hapo na kwenda kwenye eneo lenye usalama.
Serikali iliwapeleka Winifrida na Lucas kwenye kambi hiyo maalumu mkoani humo ambako nilimkuta akiwa ametulia na hana wasi wasi tena wa kuuawa.
Watu wachache wenye ulemavu wa ngozi wameimarisha ulinzi kwenye nyumba zao ikiwa ni pamoja na kuzungushia ukuta na seng'enge na pia kuweka ulinzi wa mbwa.
"Juhudi za serikali"
Tangu mwishoni mwa mwaka 2008 serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbali mbali kupambana na mauaji hayo.
Rais Jakaya Kikwete aliwaahidi wananchi wake kwamba mtu yeyote akipatikana na hatia ya kufanya mauaji hukumu yake itakuwa ni kunyongwa.
Mwishoni mwa mwezi Januari, Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda alitoa amri ya kufuta leseni za waganga wa kienyeji na wale wa Tiba asili.
"Waganga wakaidi amri"
Hata hivyo uchunguzi unaoendelea kufanywa na BBC unaonyesha kwamba waganga wa kienyeji wa aina zote bado wanaendelea na shughuli zao za ushirikina, za kupiga ramli, kile wanachokielezea kuwa ni utabibu na hata kuwashawishi wateja wao kwamba wanaweza kuwatajirisha kwa kuwazindika.
Na kwa mujibu wa waganga hao wa kienyeji, hakuna zindiko lisilokuwa na viungo vya binadamu hata kama ni damu, kucha au nywele za anayezindikwa.
"Chimbuko la mauaji"
Baadhi ya waganga wa maeneo ya mijini na vijijini wanasema kwamba hawawezi kuwaacha wateja wao wateseke kwa kuwa tu Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda alifuta leseni za waganga wa kienyeji baada ya uchunguzi kugundua kwamba waganga ndiyo chimbuko la mauaji ya albino.
Serikali hiyo pia ilianzisha upigaji kura za siri ili kuwataja wauaji, wauzaji na wanunuzi wa viungo vya albino, na wale wanaochochea mauaji hayo na pia kuunda kikosi kazi cha kuwasaka na kuwakamata wahalifu na pia kukomesha ukatili huo.
"Polisi na viongozi wa kidini"
Mwezi Juni mwaka huu kesi zilianza kusikilizwa katika mahakama kuu za Kahama na Shinyanga, kaskazini mwa nchi hiyo.
Miongoni mwa watuhumiwa ni waganga wa kienyeji, wafanyabiashara, wavuvi, viongozi wa kidini na wale wa utawala wa ngazi za chini za serikali.
Na hapo awali baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi walikamatwa huko Shinyanga kwa tuhuma zinazohusiana na mauaji hayo ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
"Kienyeji, jadi na tiba asili?"
Hata hivyo wale wanaojiita waganga wa tiba asili wanataka watofautishwe na waganga wa kienyeji au jadi. Wanadai kwamba wao wanatumia mitishamba katika matibabu yao na wale wa jadi na kienyeji wanatumia uchawi na viungo vya binadamu kuwaroga maadui wa wateja wao na pia kuwazindika wateja wao.
"Wauzaji wa viungo hawajakamatwa"
Waganga wawili kati ya wale waliokiri kwenye uchunguzi wa BBC kwamba wanatumia na viungo vya binadamu na wanauza viungo vya albino kwa ajili ya kuwatajirisha wafanya biashara na pia kuwazindika wanasiasa ili washinde uchaguzi na vile vile wanashirikiana na polisi katika shughuli zao bado wanaendelea na kazi zao. Hili ni jambo la kushangaza kwa kuwa BBC ilitoa taarifa hizi polisi.
Ni dhahiri kwamba kuna ugumu na katika utekelezaji wa amri hiyo ya kufunga shughuli za waganga wa kienyeji au wale wa jadi katika kila kona ya Tanzania.
"Tanzania itaweza?"
Na huenda hiyo imesababisha mauaji hayo kuendelea hadi sasa, na watu wenye ulemavu wa ngozi kuendelea kuishi kwa wasi wasi katika nchi ambayo hufahamika kama kisiwa cha amani barani Afrika.
Je Tanzania inaweza kweli kukomesha kabisa mauaji ya albino? Hicho ndicho kitendawili kikubwa!

http://www.bbc.co.uk/blogs/albinomurders/2009/07/albino-bado-wanauawa.html
 
Mnh, how sad jamani. I was home (In Tz) this summer, and heard on the news that kuna shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi imekuwa inavamiwa mara kwa mara, this was in Moshi. The school was asking for protection from the government, but from what I could see no urgent steps were being taken. It gets me worried sana kweli, kama sisi Africans tunaanza kuuwana wenyewe. Will the racism ever end this way? I fear for these people's lives, I really do.
Lakini I'm glad kama the government is finally looking at it.
 
Back
Top Bottom