Albino auwawa na kuondolewa baadhi ya viungo Lindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Albino auwawa na kuondolewa baadhi ya viungo Lindi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,285
  Likes Received: 5,639
  Trophy Points: 280
  Na Said Hauni, Lindi

  WAKATI Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua kampeni ya upigaji kura za siri, ili kuwabaini wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya mauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), polisi mkoani Lindi, umeokota mwili wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi, ukiwa unaelea majini kwenye mto Rukuledi, huku ukiwa umekatwa baadhi ya viungo vya mwili wake.

  Mwili wa Albino huyo uligunduliwa na wakazi wa kijiji cha Mmangawanga Machi 5 mwaka huu, ukiwa unaelea kwenye maji ya mto Rukuledi, huku baadhi ya viungo vyake vikiwa vimekatwa.

  Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Sifuel Shirima amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, ambalo ni la kwanza kutokea tangu kuanza kwa vitendo hivyo hapa nchini petu.

  Shirima alisema kwamba, mwili wa albino huyo ambaye ni mwanaume, umekutwa ukiwa umekatawa mikono yote miwili, kuondolewa sehemu zake za siri pamoja na kuchunwa ngozi ya paji lake la uso.

  Alisema, mwili wa albino huyo unaokadilia kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30, bado jina wala mahali alikokuwa akiishi hakujaweza kufahamika mara moja, amekatwa mikono yake yote miwili, kuondolewa sehemu zake za kiume na kuchunwa ngozi kwenye paji lake la uso.

  “Tayari tumeshasambaza taarifa katika vijiji na wilaya zote za mkoa na ile jirani, wafanye uchunguzi ili kubaini miongoni mwa familia kama kuna ndugu yake mwenye ulemavu wa ngozo hamuoni,” alisema Shirima.

  Shirima pia amewataka wananchi wa mkoa huo, kutojisahau, badala yake waongeze ushirikiano na vyombo vya Dola katika kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi, ili vitendo hivyo visiweze kuendelea kushamili kwenye mkoa na Taifa kwa ujumla.

  Katika tukio la pili, Shirima alisema mkazi wa kijiji hicho cha Mmangawanga, Shirazi Mtambo {6} amekufa baada ya kushambuliwa na mamba, alipokuwa na wenzake wakioga maji kwenye mto huo wa Rukuledi.

  Alisema, mamba huyo aliyekuwa katika mawindo alifanikiwa kumkamata mtoto huyo na kwenda naye kwenye maji ya kina kirefu, lakini jitihada za vijana wenzake kutoa taarifa kwa wakubwa,walifanikiwa kuupata mwili wake na kuuzika siku hiyo hiyo
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Albino wangekuwa na mwanga wangeenda ubalozi wa Unigereza kuomba asylum wana-case nzuri tu ya kupewa asylum. Hiyo ndio njia pekee ya kunusuru maisha yao otherwise, sasa wataanza kutumiwa na watu kwa manufaa ya kisiasa.
   
Loading...