Albino auawa na kukatwa viungo vya siri... [NI UZUSHI, SI KWELI]

Status
Not open for further replies.

Livanga

JF-Expert Member
Apr 15, 2010
470
148
ALBINO AUAWA NA KUKATWA VIUNGO VYA SIRI LAKINI WAUAJI WANG'ANG'ANIA KATIKA MWILI WA MAREHEM.

Tukio hili limetokea Leo katika mji wa Nansio wilaya ya Ukerewe ambapo wauaji hao baada ya kumwua albino huyo na kuanza kukata via vyake vya uzazi wamejikuta waking'ang'ania kwenye mwili Wa marehem huyo.

Wananchi wenye hasira walianza kuwapiga watu hao lakini polisi waliwahi kufika na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

Hadi hvi sasa mwili wa marehem uko chumba cha kuhifadhia maiti cha hospital ya Nansio na wauaji hao bado wameng'ang'ania kwenye mwili wa marehem.

Nitaendelea kuwajuza nikipata habari kamili.

==========
UPDATE:

Mwandishi wa JamiiForums ameongea na RPC mkoani Mwanza, Valentino Mlowa, na amekanusha kuwepo kwa tukio hili na kuwa ni uzushi unaosambazwa kwa kasi.
 
Kwa hiyo hao wauaji nao wameingizwa kwenye chumba cha maiti au?

Tiba
 
RFA wametangaza kuwa RPC wa mkoa wa mwanza kasema ni hii habri ni uzushi, na kuwataka wananchi wasiwe wanaacha shughuli zao na kukusanyika kwa habari za uzushi.. Kama kawaida watu walishajaa hospitali ya Nansio kushuhudia..
 
Asante sana kwa kulidadavua hili manake chanzo changu kule ukerewe kilipotea hewani.
RFA wametangaza kuwa RPC wa mkoa wa mwanza kasema ni hii habri ni uzushi, na kuwataka wananchi wasiwe wanaacha shughuli zao na kukusanyika kwa habari za uzushi.. Kama kawaida watu walishajaa hospitali ya nansio kushuhudia..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom