albino akikuibia SIMU kariakoo utamkimbiza??madhara yake unajua??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

albino akikuibia SIMU kariakoo utamkimbiza??madhara yake unajua???

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mwanaizaya, Dec 15, 2008.

 1. m

  mwanaizaya Senior Member

  #1
  Dec 15, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu wenzangu ni hali ya kusikitisha sana inayowzukia hawa ndugu zetu albino's...imefika sasa hata watoto albino's ukiwakuta wanavuka barabarani ukawafwata kuwasaidia wanakimbia kama mwewe........
  inasikitisha sana JK kutokuwa makini na hili..nimekaa nikafikiria wote ni binadamu na tuna hisia kama binadamu wote...nikasema niwaulize wenzangu
  ZERUZERU AKIKUIBIA SIMU KARIAKOO UTAMKIMBIZA...IKITOKEA UNAMKIMBIZA UNAJUA MADHARA YAKE...MUNGU EPUSHIA MBALI!!!!
  NAOMBA MSAADA WENU...
   
 2. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  utamuacha tu manake anaweza kukugeuzia kibao mpaka ukaishia pabaya.
   
 3. m

  mwanaizaya Senior Member

  #3
  Dec 15, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani watu watanza kukuwashia moto wewe kabla ya kujibu alikuwa anataka mkono wangu!!!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  LOL!!!!...Madhara yake ni kifo!!!! Maana njemba zitajumlisha 2 na 2 na kupata jawabu kwamba unanyemelea viuongo vya Albino huyo ili uvipele kwa Waganga.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Chances are one in a million kukutana na albino kibaka.Hata ukukutana naye na akakuibia basi huyo si wa kawaida, kimbia ndugu yangu!!
  Mpaka utakapoonekana wewe ndo umeibiwa "wananchi wenye hasira kali " watakuwa wamemaliza kazi yao.
   
 6. m

  mwanaizaya Senior Member

  #6
  Dec 15, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutangaze hali ya hatari mauaji ya albino
  Faraja Mgwabati
  Daily News; Sunday,December 14, 2008 @20:03

  VITENDO vya mauaji ya albino nchini kwa imani za kishirikina, vimevuka mipaka na kulifanya jambo hilo siyo tena la kubembelezana, bali nguvu inahitajika kutumika kuondoa aibu hii.

  Takribani albino zaidi ya 30 wameshauawa hadi sasa na dalili zinaonyesha mauaji hayatakoma leo wala kesho kwani hata wakati viongozi wakuu walipokuwa wakikemea mauaji hayo, kesho yake unasikia tena kuna mwingine ameuawa.

  Viongozi wa serikali, wa dini, taasisi za kijamii, wanasheria na vyama vya kupigania haki za binadamu vya ndani na nje na hata wanahabari, wamelaani mauaji hayo, lakini haijasaidia.

  Naamini sasa umefika wakati kwa serikali kutangaza hali ya hatari au kutangaza mauaji ya albino kuwa ni janga la kitaifa kwa kuwa usalama wa raia hawa wenye ulemavu wa ngozi upo mashakani, nao ni Watanzania kama wengine wanahitaji kuishi kwa usalama bila hofu.

  Nasema hivyo kwa sababu siamini kama kukemea au kulaani au kutoa elimu kwa jamii pekee yake kunatosha, bali nguvu ya dola zaidi inahitajika kumaliza tatizo hilo.

  Sioni sababu ya kuweka nguvu nyingi kwenye kuelimisha jamii kwa sababu hakuna mtu katika karne ya leo asiyejua kwamba kuua mtu ni kosa la jinai na adhabu yake ni kunyongwa.

  Hivyo naamini kwamba wauaji wa albino wanajua wanachokifanya ila tu kwa sababu wamepumbazwa na ujinga wa waganga wa kienyeji ndiyo maana wanachukua jukumu hilo zito la kuua wenzao.

  Sasa watu kama hawa siyo wa kucheka nao tena, bali ni kuwashughulikia kwa nguvu ya ziada tena ikibidi adhabu iwe kubwa zaidi ya wale wanaopatikana na hatia ya mauaji mengine kwa kuwa wanaoua albino wanadhamiria.

  Ndani ya hali ya hatari, endapo itasikia albino ameuawa au usalama wake umetishiwa, ifanye msako wa nyumba hadi nyumba ikiwakamata wahusika wote wakiwamo waganga wa jadi wote wa eneo hilo.

  Pia viongozi wa vijiji husika na hata wananchi ambao wanaweza kuwahisi wanahusika kwa namna moja au nyingine ili kupata ushahidi wa kutosha. Kwa kuendesha msako wa nyumba hadi nyumba bila shaka wahusika watakamatwa haraka, lakini pia wakishakamatwa wabanwe hadi wataje wanzao wote waliohusika wakiwamo waganga wa jadi wote wawekwe ndani.

  Upelelezi wa kesi za wauaji wa albino ufanywe haraka ili wahusika wachukuliwe hatua haraka huku kesi hizo zitangazwe zaidi na vyombo vya habari ili kuwa fundisho kwa watu wengine.

  Kikosi cha Operesheni Maalumu chini ya Kamanda Venance Tossi kinaweza kutumika kufanya kazi hiyo pamoja na kazi nyingine wanazozifanya kama za kukamata na kuchoma mashamba ya bangi.

  Naamini bila kutumia nguvu mauaji ya albino yataendelea zaidi na tutakapokuja kushtuka ndugu zetu hawa watakuwa wamekwisha na hao waganga watahamia kwa watu wengine.

  Baadaye wataanza kusema wanataka viungo vya Wazungu na wananchi wanaotaka utajiri wa haraka wataamini wataanza kuua Wazungu, itakuwa dhambi juu ya dhambi.

  Tusisahau kuwa waganga wetu ndiyo walisababisha matukio ya uchunaji ngozi yaliyosababisha mauaji mengi ya watu hasa Mkoa wa Mbeya miaka michache iliyopita
   
 7. c

  capuchino Member

  #7
  Dec 16, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mi ntalia tu najua nikimkimbiza siipati
   
 8. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Acha kumkimbiza kutaka simu yako madhara makubwa yatakupata lakini hata kumchumbia tu binti wa Kialbino sasa hivi ni noma. Eti unaenda kupeleka posa, nataka kumuoa binti albino kwanza watataka kujua historia background yako kisha kasheshe inaanza.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mimi nitamkimbiza na kuita mwizi kamata mwizi huyo watu watanielewa bila shaka.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Breaking News;
  Madaktari wazitwanga:
  Dar madaktari wa mabingwa wa kitengo cha upasuaji wametwangana wa kitengo cha upasuaji wametwangana makonde mazito ndani ya hospitali ya muhimbili nusura yakutoana roho,riport wetu bwana MAGANSA ametaarifu kuwa chanzo chao mabingwa hao kimetokana na kugombania kumfanyia upasuaji wa mkono Albino alie jitokeza hospitali hapo baada ya kupata ajali na kutakiwa kukatwa mkono.Kwa taarifa zaidi stay online......
   
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mi naona ni kuwasamehe bure! Ila jina la zeruzeru si surio nafikiri ni vyema tukawaita albino!
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mwanaizaya,

  Usilete utani wa kividuduvidudu kuhusu mauaji ya albino!

  Umeanza kwa kujifanya unasikitishwa na janga hili kumbe unatafuta gia ya kuchomekea ki riff chako uchwara kuhusu mauaji haya. "Zeruzeru akikuibia simu utamkimbiza" maana yake nini kama sio kudhihaki sensiitivity na suspicion iliyojengeka dhidi ya yeyote anakae onekana kama anam-pursue albino. Hiyo sensitivity inahitajika, na sio jambo la kulikejeli kwa swali la kizandiki na kichekechea kama hilo.
   
 13. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hawatakuelewa bila shaka
   
Loading...