Albert Msando apotoka tena

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai. Vijana kama Msando wamebaini hilo na wanajitahidi kuweka misingi ya siasa safi ndani ya Chadema.

Mida Eight, kwanini unakumbatia misingi ya kilaghai? Kwanini kama umeshindwa kushirikiana na Msando kuweka misingi ya siasa safi angalau usikae kimya tu?

wewe kilaza mwambie huyo muhaini zitto atupe majina ya uswis
 
CHAdEmA lazima imwajibishe Msando ili kumsaidia kuwa huru katika kesi hiyo. Nashangaa kwa wakili na msomi kushindwa kiona mstari wa mgongano wa maslahi katika swala hilo.
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai. Vijana kama Msando wamebaini hilo na wanajitahidi kuweka misingi ya siasa safi ndani ya Chadema.

Mida Eight, kwanini unakumbatia misingi ya kilaghai? Kwanini kama umeshindwa kushirikiana na Msando kuweka misingi ya siasa safi angalau usikae kimya tu?

Unapoongelea misingi maana yake unaongelea genesis.Unaongelea Origin.Huyo unayetaka nishirikiane nae atakua muasisi wake kwa kuwa ni mwanachama wa muda mrefu na ni kiongozi labda kama msamiati wa neno "Msingi/misingi" una tafsiri nyingine

Halafu;Habari mbaya kwako ni kuwa siwezi kukaa kimya kama mnavyotamani.Never!
 
Msando,
Naomba nitajie kifungu chochote cha kikatiba kinacho ruhusu representation kwenye Maamuzi ya Chama. Kama hairuhusu basi na wewe ni mmoja wapo wa Mhaini. Kwa kuwa katiba haisemi sehemu yoyote kukusu mtuhumiwa ndani ya Chama kutumia Wakili kwenye maamuzi ya Vikao halali vya Chama.

Hii kesi iko kwenye maandalizi ya kwenda mahakamani. Wakili ni lazima kutumika.

Labda upeo wako wa Bavicha umeshindwa kuelewa nini kitafuata iwapo Kamati Kuu itakuwa mbogo...
 
Unapoongelea misingi maana yake unaongelea genesis.Unaongelea Origin.Huyo unayetaka nishirikiane nae atakua muasisi wake kwa kuwa ni mwanachama wa muda mrefu na ni kiongozi labda kama msamiati wa neno "Msingi/misingi" una tafsiri nyingine

Halafu;Habari mbaya kwako ni kuwa siwezi kukaa kimya kama mnavyotamani.Never!

You have chosen a very wrong side of history.

Its pity!

Juzi nilikuwa naangalia picha za harusi ya Mchange na nikasema ingekuwa vizuri Ben angehudhuria hii shughuli. Kuna vitu vidogovidogo unavikosea lakini vinakusukuma kwenye maamuzi ambayo madhara yake ni ya kudumu.

Jifunze kuwa tayari kusikiliza, usitake kuwa msemaji tu kila wakati. Wakati mwingine unaweza kuleta mabadiliko zaidi kwa kusikiliza.
 
Kama huu ndio utetezi wao naona kufukuzwa kwao kupo karibu sana! kama katiba ilichakachuliwa,nadhani wao hao ma-MM walikuwa wajumbe wa kamati kuu.swali la kujiuliza je,hawakuwahi kukiona hicho kipengele toka 2006 hadi hadi majuzi? je,hilo swala la katiba wameshawahi kulitolea hoja ndani ya vikao vya CC na kutaka marekebisho? huu utetezi wao ni wa kitoto na upo nje ya mashitaka yao na naliona anguko lao!

Sio wao tu, Hata wewe unadhani huu utetezi wako ndio utahalalisha upuuzi wa kuchezea katiba?
 
Hii ndio shida ya kuwa kanjanja.Chadema ina watu wasomi wazuri,wachambuzi wazuri na wengine wengi tu.Mbowe ni nani abadilishe katiba bila ridhaa ya baraza kuu la chama?Usipende kutumiwa.Pambana jasho likutoke ule kwa baraka toka kwa Mungu.

Kanjanja ni wewe usiekuwa na kumbukumbu! Slaa alikataa humu humu jf yapata Mwezi sasa kuwa Chadema haijawahi kuwa na Ibara inayoelezea ukomo wa Uongozi. Watu wakaleta Katiba ya kabla ya mabadiliko ya sasa yenye kipengele hicho watu wakaumbuka. 'USISEME HAKUNA MWANGA WA JUA SEMA HUONI MWANGA WA JUA'. Wewe unakuja na uongo mwengine eti kipengele hicho kilibadilishwa kwa Baraka za Baraza kuu halafu unajiita Msomi?? Mpaka mtajane nani kafanya uhuni huu japo maji yakiwafika shingonio mtasema ' it was a Typing error'
 
You have chosen a very wrong side of history.

Its pity!

Juzi nilikuwa naangalia picha za harusi ya Mchange na nikasema ingekuwa vizuri Ben angehudhuria hii shughuli. Kuna vitu vidogovidogo unavikosea lakini vinakusukuma kwenye maamuzi ambayo madhara yake ni ya kudumu.

Jifunze kuwa tayari kusikiliza, usitake kuwa msemaji tu kila wakati. Wakati mwingine unaweza kuleta mabadiliko zaidi kwa kusikiliza.

This is nonesense.Usiushushe mjadala kwenye level ya picha za harusi.

Ambition za kishamba kabisa unazileta humu.Hii ni comment ya great thinker kweli?
 
Kijana kapotea moja kwa moja,na kujibu hoja kwa emotions baada ya kujua kapotoka. Nenda kaendeleze deal zako Arusha
 
NAOMBA NIKUJIBU KWENYE HIYO RANGI YA UGOLO yenye kuzungumzia udharula wa kuchukua maamuzi na haki ya kusikilizwa. Hizo hoja zingine ulizoziibua hazina mashiko na ziko kiushabiki zaidi kuliko "kweli"


a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.

b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.


Udharula wa kipengere "d" unauwezo na mamlaka ya kuvunja vipengere "b" na "c" iliyokwenye maandishi ya bluu, lakini kipengere "a" hakijatajwa kwenye kipengere "d" kama kinaweza kuvunjwa na hicho kipengere "d". hicho kipengere "a" ndio msingi wa haki ya kusikilizwa bila kipengere "a" hiyo katiba itakuwa inatoa fursa kwa watu wenye chuki binafsi kama Lema na Msigwa kufukuza wenzao hovyo kila wanapojisikia.


Tena tukizingatia wahusika waliomba kujiuzulu lakini Tundu Lissu kwa kujifanya anajua zaidi au huenda kwa kutumika kwake bila kujua akatoa hoja ya watuhumiwa kuvuliwa nyadhifa zao, basi kuvuliwa huko kwa nyadhifa kunahesabika ni adhabu au hatua za kinidhamu ambazo kwa kutii takwa la kifungu "a" ilibidi zichukuliwe mara baada ya wahusika kupewa mashtaka yao kwa maandishi na kisha wayajibu ndani ya wiki mbili.



Zitto kasomewa mashtaka badala ya kupewa kwa maandishi, lakini mbaya zaidi kasomewa mashtaka siku moja na siku hiyohiyo kajitetea na siku hiyohiyo hukumu ikatolewa kwa wahusika kuvuliwa nyadhifa zao. Hivi kweli huu ndio utawala wa sheria? au hii ni sheria ya wapi? hii ndio demokrasia ya chama chetu cha CHADEMA.


Mbowe kama Lipumba, kwa uongozi wake shupavu ameipaisha CUF na kwa kung'ang'ania madaraka kumeishusha CUF. Maamuzi haya ya kibabe ya kamati kuu kwa vyovyote vile ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Mbowe kubaki madarakani kwa kumvunja mbawa mtia nia. Kutangazwa kwa ratiba na tarehe ya uchaguzi siku chache mara baada ya maamuzi haya kibabe ni kiashiria tosha cha maamuzi yale ya kamati kuu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mbowe kugombea bila kupingwa na Zitto. Sababu ni ajabu kwa Mwenyekiti na mwanademokrasia kubariki maamuzi haya ya kibabe na yenye kukiuka misingi ya kikatiba na ya haki ya kusikilizwa.


Nia njema huja sanjari na maumivu lakini nia ovu hukabiliwa kwa ustahamilivu, usishue chombo ili hali maji yajaa lakini unaweza kutengeneza kupwa kwa maji, kila jambo lina wakati wake lakini wakati unawezwa kutengenezwa pia, na kivuno cha mdudu chungu leo, kesho huenda ndio shibe yako, naomba haya Zitto Kabwe ayajue na yawe sehemu ya maisha yake.


Pole Zitto Zuberi Kabwe yote yana mungu, dunia ni hino hino, waja na ada zao ni wale wale tandu Adamu {a.s} hadi kwa Muhamad{s.a.w}, kwahivyo hayana budi kuwa midhali ungali chini ya jua. Tema mate chini ili waja waendelee kujilisha upepo kwa kudhani watashibisha matumbo yao yenye njaa ya tamaa, uchu na ung'ang'anizi wa madaraka wenye lengo la kufuta alama chafu za uongozi wao zilizochorwa kwa kalamu ya moto kwenye chuma cha pua.


Wakoloni waliwaita wapigania uhuru waahini na wachochezi, CCM inaimba wimbo kama huo wa kikoloni, lakini la ajabu baadhi ya viongozi wa CHADEMA, aidha kwakuwa watu walioshika mpini hulka zao hufanana au kigeugeu hakina mji wao, nao wameanza kuwaita wapinzani wao katika kuwania uongozi na wakosoaji wao kuwa ni wasaliti, mamluki na kubwa zaidi ni waahini kama vile CHADEMA ni dola kumbe ni chama tu cha siasa.


Njano5.
0655345394
1. Amekata rufaa bila kujibu mashtaka 11
2. Unajua kuwa kuna kuvuliwa uongozi mna hatua zake kikatiba paoja na kuvuliwa uanachama hatua zake kikatiba?
Kumbe na wewe ni hewa tu
 
hizi mbwembwe za kisheria zinatoka wapi kwa mtu ambaye amekiri kucheza mpira wa miguu chini ya meza? huwezi kucheza mpira wa kishetani halafu ukataka kujitetea kwa mbinu za namna hii. Kaka Msando kama ningekuwa na uwezo ningempa huyo Zitto adhabu sawa na aliyopewa JONG SONG huko korea kaskazini. adhabu mujarab kwa msaliti ni kifo.
Mwaikenda,

1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?

2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?

3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?

Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.

4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.

5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?

Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.

Ahsante.
 
Ha ha haha! Hivi unaelewa unaandika kwenye public forum?Bila ridhaa yake?What do you mean?

Omar,Kwanza declare interest zako katika hili sakata.Leo wanafiki wote watajitokeza.

Urafiki wako na watu usijaribu kuuingiza kwenye mijadala maana hautakua objective zaidi ya kuleta mihemko.

Nilishakuambia mara kadhaa jenga hoja kulingana na age na uwe principled.Wewe kama msaidizi wa Dr.Salim ulitakiwa ujifunze mengi kutoka kwake.

Unafiki utalimaliza taifa kama tutaacha kuwaambia ukweli watu wa sampuli yako.

Hivi mdongo wangu unajua maana ya neno kuwa principled? Unanikumbusha enzi za siasa za chuo kikuu ambazo inaelekea wewe bado haujaweza kumature... No wonder ukatengeneza emails za kina Mwigulu na Nchimbi kujaribu kusaidia propaganda zenu... typical students politics!
 
Wewe asante kwa ufafanuzi diwani huyu anatafuta umaarufu zito tunamtupilia mbali viongozi wa kamati kuu sio wajinga watu wenye akili anae mtetea zito hana nia nzuri na chadema kabisa
 
Nimerudisha Thread kutokana na upotoshaji unaondelea kutaka kwa baadhi ya wachangiaji "maalum" kwenye thread za Mwanakijiji na Yericko
 
Msando huwa napata taaabu saana kuona maamuzi ya haki na ya kumpa mtu haki ya kujitetea nyinyi mnaweka kipaumbele cha nafasi zenu katika chama

1. ningefurahi kama ungeniambia pale wanapo sadifu kama wewe si mkamilifui wakufanye nini.
2. kakosea wajibu wake kumuongezea vyeo au kumvua mpaka utetezi wake utakapotimilika na kuishawishi kamati kumrudishia nafasi zake.
3. nisadie kumuuliza zitto hivi ZILE PESA ZA KWENDA KUFUATILIA MABILIONI NJE YA NCHI zinatoka kwenye kamati ya POAC au ni mshahara wake wa kiuzalendo.
4. ni kweli ile ilikuwa kazi ya TISS lakini wakaamua kumpa yeye kuifanya ili awe kiongozi wa maslahi ya jamii.
mimi nauliza kama mwanachama ili nione kama ana haki au laaa
5. BEN sanane nisaidie kuniulizia vizuri
Nilipo kuwa Chuo na kiongozi wa Chuo kama Speaker sikupenda mtu kuonewa na badala yake nilitaka kujiridhisha kabla sijatoa final decision
 
Hivi mdongo wangu unajua maana ya neno kuwa principled? Unanikumbusha enzi za siasa za chuo kikuu ambazo inaelekea wewe bado haujaweza kumature... No wonder ukatengeneza emails za kina Mwigulu na Nchimbi kujaribu kusaidia propaganda zenu... typical students politics!

Unaweza kuthibitisha ni lini na wapi nilikotengeneza E-mail za Nchimbi na Mwigulu?


JF is not a rumour-mongering site.

You are just another dolt looking for relevance.

Maturity na hizo old school statement unadhani zina uhusiano wowote na kuwa "Principled"?

Bado Unadhani maturity ni mvi?

So,Stop trying to hoodwink us with these oldlines
 
Back
Top Bottom