Molemo, nitajie matusi yangu kwa Chama na Kamati Kuu. Nitaona aibu.
Ulinzi wa nini nahitaji? Unawapa sifa CCM wasizostahili hata kidogo. Katika maisha yangu CCM wangekuwa wameongea na mimi au wamenitumia kwa hata jambo moja wangejisifu sana. Hilo halitakaa litokee na wanajua hivyo.
Inawezekana kabisa wewe ni mwanaCCM unajidai Chadema kwa kusema uongo na uzushi ili ionekane kuna tatizo. Tunawashtukia na tutawakomesha. Ujanja wenu wa kuchonganisha kwa kutumia kivuli cha kutojulikana kimefika mwisho.
Hatuendekezi upuuzi. Na kama ni mwanachadema na unaamini unachosema nipigie simu unieleweshe na mimi nitakuelewesha. Hakuna sababu ya kujificha. Nitumie PM na nitajadiliana na wewe vizuri tu.
Ha..Ha..Haaa!!
Nijibu maswali yafuatayo..
Ni sahihi kwenda Serena Hotel kuzungumzia uliyoyazungumzia huku ukijua waandishi wa habari siyo walioshtaki hao waasi unaowatetea?
Pili Ukiwa kama Diwani wa Chadema ni sawa kabisa kufanya unachokufanya??
Kwanini nikupigie simu huku ukiwa wewe unatangaza mambo ya Chadema Serena Hotel??
Unapinga vijana wa UVCCM hawakuwa wanaratibu watu waliokuwa wanaingia mkutanoni Serena??
Huoni wanachadema makini wamekosa Imani na wewe??
Kwa hiyo ulivyoandika unakomesha tabia unayoisema ndani ya Chadema unamaanisha unakomesha tabia ya Mbowe,Dr Slaa na Kamati Kuu??.
Tuanzie hapo Mkuu..