Albert Msando apotoka tena

wewe ndiyo umepotoka mkuu hili la zitto kuvuliwa nafasi zake za uongozi na cc wakati zitto alipewa uongozi na halmashauri kuu?
 
Asante sana Mkuu@mwaikenda, sasa nyie badala ya kwenda serena nyookeni jangwani kwenye mahakama ya umma.

Zitto tupa kule!!

we rukaruka tu lakini mwisho wa siku utamjua zitto kuwa ni nani kwenye hii dunia na chadema kwa ujumla.
 
Mwaikenda,

1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?

2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?

3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?

Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.

4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.

5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?

Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.

Ahsante.

Why are you taking it public kama wewe ni mwanachama na mbali ya hapo ni diwani hujui taratibu za chama kweli? Serena Hotel imekuwa sehemu ya mamlaka za chama hadi ujitokeze kila siku kwenye hadhara
Unaonekana mtoto kweli aisee
 
Huyu Msando ni mchumia tumbo anajulikana na amekuwa akitukana viongozi wa Chadema kila siku kupitia FB wall yake!

Sijui Chadema iliokota wapi mamluki hawa na kuwapatia uongozi.

huyu naye afanyiwe kazi...
 
seriously BEN

there is no need to take you guys serious on anything until you grow up as a party... mmekua kama timu sisyo na klabu

kutwa fyee fyee fyeeee mitandaoni

that is not leadership

TIMING,

Wakati mchakato wa kuwajibishana ukiwa unaendelea kikanuni na kikatiba busara ni kuwa upotoshaji wowote wenye athari kichama ni lazima ujibiwe na mamlaka husika au wapenzi na wafuasi wa chama na hata wanataaluma ambao hawana chama .

Upotoshaji haupaswi kuendelea na kuharibu taswira ya chama kama CHADEMA ambacho kimebeba dhamaba kubwa ya watanzania katika kusukuma mabadiliko

Chama kikikaa kimya wakati shughuli ya kukichafua na kuzusha kila aina ya uongo basi hakitakua chama serious na hata dhamana waliyopewa hawatakua wameiheshimu
 
Last edited by a moderator:
Eti mtu wa CCM unamsemea Zitto.

Shame!!

wewe unataka kunitibua nkuropokee madhambi yako hatimaye nipigwe ban bure madhambi yako nayajua sana halafu unajifanya mwema huna lolote mtu mzima halafu unakuwa wa ajabu kutwa nzima kupotosha umma sijui unapata nini kwenye huo upotoshaji wako.
unasema mimi mwanaccm ulinipa kadi ya ccm wewe watu wengine utadhani mnashindia mikaa bana.
 
JF,

Issue sio Msando Albert ni nani au kwa nini anatetea.

Issue ni rahisi natetea nini na utetezi wangu uko based kwenye nini.

1. Utaratibu wa kumvua Zitto nyadhifa haukufuatwa.

2. Sababu zilizotolewa ni circumstantial. Hazijitoshelezi. Zote zinatokana na waraka wa Mwigamba.

Kabla ya kutukana, kudharau na kukejeli yajadiliwe ninayoyasema na sio mimi.

Kama kijana, mwanachadema mwenye taaluma ya Sheria nina wajibu kusema haya. Sasa nikosolewe makosa yangu kwa nafasi hizo tatu na sio vinginevyo.

Mpaka sasa hakuna mahali ambapo hoja inatolewa ya wapi sistahili kusemea. Jazba hazijengi wala kuelekeza njia sahihi kama lengo ni kujenga.

Ila kama nia ni kupiga story tu kumaliza siku ni sawa pia.
 
Huyu Msando ni mchumia tumbo anajulikana na amekuwa akitukana viongozi wa Chadema kila siku kupitia FB wall yake!

Sijui Chadema iliokota wapi mamluki hawa na kuwapatia uongozi.

Mtu akiwa na mawazo tofauti tu ni mamlaka!

Ndio maana mnapenda mazezeta kama Heche.

Cc sixgates
 
Last edited by a moderator:
Why are you taking it public kama wewe ni mwanachama na mbali ya hapo ni diwani hujui taratibu za chama kweli? Serena Hotel imekuwa sehemu ya mamlaka za chama hadi ujitokeze kila siku kwenye hadhara
Unaonekana mtoto kweli aisee

Eti ni mwanachama wa Chadema.

Nyang'anya Kadi hyo.Sijui viongozi wa Kanda ya Kaskazini wanafanya nini hawaoni huu utovu wa Nidhamu wa huyu anayejiita Diwani wa Chadema.
 
Why are you taking it public kama wewe ni mwanachama na mbali ya hapo ni diwani hujui taratibu za chama kweli? Serena Hotel imekuwa sehemu ya mamlaka za chama hadi ujitokeze kila siku kwenye hadhara
Unaonekana mtoto kweli aisee

tangu lini chadema ikafuata utaratibu wa kichama kuzungumza mbona kila mtu huropoka lake mahara popote pale subirini mnyika na lisu watakavyolipuka kwenye hili swala.
 
Huyu Msando ni mchumia tumbo anajulikana na amekuwa akitukana viongozi wa Chadema kila siku kupitia FB wall yake!

Sijui Chadema iliokota wapi mamluki hawa na kuwapatia uongozi.
Huyu jamaa anatumia mianya na fursa kuongeza kipato chake. Kwake yeye Zitto ni fursa ya kujipatia pesa, hana ethics wala siasa hazimuusu kivile.

Ila nafurahi sana kwa namna Msando anavyoli-handle hili suala; anazidi kujenga mazingira kwa mteja wake kutimuliwa uanachama; yule Mheshimiwa hawezi salimika siku shoka la CC likishuka.
 
Nitashangaa sana vijana 2a ufpa ben saa 9 na jercko waspodominate huu uzi na vbaraka wengne wa mwkt wa maisha pale ufpa
 
Back
Top Bottom