mwaikenda
JF-Expert Member
- Mar 26, 2011
- 903
- 141
Wana Jf,
Naomba ieleweke kuwa Katiba ya CHADEMA toleo la mwaka 2006 ndiyo msingi mkubwa wa kuendesha taasisi. Ufafanuzi uliotolewa leo kwa vyombo vya habari na Wakili Albert Msando ni upotoshaji mkubwa wa Katiba ya Chadema na hii inatokana na aidha uelewa mdogo wa Katiba hiyo na/ au ni makusudi kwa malengo ya huyo anayedai kumwakilisha.
Upotoshaji huo ni kama ufuatayo;
Mosi, hatua iliyochukuliwa Kamati Kuu kumsimamisha uongozi huyo anayedai kumwakilisha ilifikiwa kwa lengo moja tu la kunusuru Chama kama hatua ya dharura kwa mujibu wa ibara ya 6.5.2 ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama pamoja na marekebisho ya mwaka 2013 ili kuruhusu utaratibu wa kinidhamu wa kawaida kwa mujibu wa Katiba na Kanuni. Itakuwa ni taasisi ya ajabu ambayo itasubiri madhara makubwa ya uharamia uliokuwa unataka kufanyika alafu Kamati Kuu kama chombo cha kusimamia utendaji wa Sekretarieti ikae kimya alafu wahaini waendelee kuutumia mwanya wa kikanuni kuharibu na kuathiri taasisi nzima. Hata hivyo Kanuni ipo kimya kuhusu dhana ya dharura, lakini kisheria dharura ni kutokana hali husika katika wakati huo au kutokana na mazingira yaliyopo (Prevailing circumstance).
Pili, kuhusu kupatiwa taarifa kamili ya mwenendo wa kikao cha Kamati Kuu kama ambavyo amedai kuwa mpaka sasa yeye na huyo anayemwakilisha hawajapokea, amepotoka kabisa. Kanuni aliyonukuu ambayo ni ibara ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji kazi za Chama inatamka kuwa taarifa kamili ya mwenendo itawasilishwa kwenye kikao cha juu. Suala hapa ni je Msando amekuwa kikao cha ngazi ya juu pamoja huyo anayedai kumwakilisha?
Tatu, kuhusu anayedai kumwakilisha kutotajwa kwenye Waraka wa uhaini na hivyo kutokuwa na makosa ni jambo ambalo linaingia kwenye maudhui na hoja ambazo anayedai kumwakilisha anatakiwa kuzijibu katika muda aliopewa na kikao cha Kamati Kuu na hivyo hatua yake ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ni aina ya utoto na kutaka msamaha/huruma ya umma (public sympathy) na kuendeleza mjadala usio na tija kwa vyombo vya habari.
Nne, Wakili Msando ameshindwa kutoa dhana ya anayedai kumwakilisha kupewa mashtaka na kutakiwa kujibu ndani ya siku 14. Je haikidhi matakwa ya kikanuni kama alivyoainisha?
Tano, anayedai kumwakilisha anakwepa kujibu tuhuma 11 zilizoainishwa katika hati ya mashtaka ili baada ya maamuzi, na kama hataridhika na maamuzi akate rufaa.
Sita, itakuwa ni taasisi ya ajabu ambayo inaona hujuma kubwa dhidi yake alafu iache kuchukua hatua za dharura kujinusuru.
Saba, Ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba ya Chama toleo la mwaka 2006 ikisomwa pamoja na marekebisho ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama ya mwaka 2013, vifungu vyote hivyo vinazungumzia hatua za kuvuliwa uanachama. Ikumbukwe kuwa hatua zilizochukuliwa ni za kiuongozi na sio kumvua uanachama huyo anayemwakilisha. Hata hivyo hati ya mashtaka pamoja na agizo la kujibu ndani ya siku 14 imekidhi utaratibu wa kikanuni kama anavyodai wewe.
Nane, ieleweke kuwa Wakili Msando ni Diwani wa CHADEMA katika akiwakilisha Kata ya Mabogini huko Moshi. Naomba arejee Kanuni za Madiwani ibara ya 5.0 (d) ambayo naomba kuinukuu "Diwani anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhfa na nafasi aliyonayo kama Diwani kukijenga Chama ndani na nje ya Halmashauri". Kama Wakili naamini anajua hatua za kuchukua akiendelea kukomalia suala hili, nimkumbushe tu kuwa anatakiwa ajiuzulu hiyo nafasi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na afanye kazi yake ya uwakili kama anataka kuendelea na kushiriki kupinga maamuzi ya Kamati Kuu.
Naomba kuwasilisha.
Mwaikenda
=========================
Majibu kutoka kwa Albert Msando

Mwaikenda,
1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?
2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?
3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?
Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.
4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.
5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?
Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.
Ahsante.