Albert Msando ‘amwaga’ vifaa vya Corona kwa wanahabari Arusha, adai hali ni mbaya sana

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wakili wa Kijitegemea, Alberti Msando ametoa msaada wa barakoa 100 pamoja na vitakasa mikono 100 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19 kutokana na kazi yao kuwa na mwingiliano wa watu.

Akikabidhi msaada huo leo kwenye Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha(APC) kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Claud Gwandu, Msando alisema wanahabari ni watu muhimu katika kutafuta habari hivyo hatua ya kuwapatia barakoa na vitakasaa mikono itawawezesha kupambana na ugonjwa huo.

Alisema wanahabari ni watu muhimu katika kutoa taarifa sahihi za kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kuelimisha jamii juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Korona ikiwemo kuhakikisha wanafuata taratibu zote zinazotakiwa katika kujikinga na ugonjwa huo.

Alisema wanahabari wananchango mkubwa katika utoaji wa taarifa zao ikiwemo kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi licha ya ugonjwa huu wa Korona kuwepo kwa jamii.

"Lazima mchukue tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona kwa kuandika habari sahihi na kutoa habari kwa wananchi hivyo ni lazima muandike habari ili wananchi wajue "

"ukweli ni kwamba na niseme bila kuficha hali ni mbaya Arusha, msiposema ukweli tutazikana, ifike mahali muweke mguu chini na mseme ukweli bila kuogopa"

Naye Mwenyekiti wa APC, Gwandu alishukuru kwa msaada huo kwa wanahabari ambao utawasaidia kujikinga na ugonjwa huo na kutoa rai kwa wadau wengine kujitoa kusaidia wanahabari katika kupambana na ugonjwa huu wa Corona.

Pia wanahabari wengine wa Mkoa wa Arusha Lillian Joel Uhuru na Cynthia Mwilolezi wa Nipashe walishukuru kwa msaada huo ambao utawasaidia kujikinga na maambukizi ya Covid - 19.

Ends....

zaidi soma: Waandishi Clouds 360 wamshukia kama mwewe wakili Msando kwa kupotosha kuwa Arusha hali ni mbaya kwa Corona - JamiiForums

Wakili Albert Msando ashikiliwa na Polisi baada ya kutoa taarifa ya hali ya maambukizi ya Corona na kuhamasisha waandishi kuandika ukweli - JamiiForums

IMG_20200428_112314_7.jpeg
IMG_20200428_112316_8.jpeg
IMG_20200428_112309_5.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Janga la corona limemuibua wakili Albert Msando jijini Arusha na kugawa vifaa vya kujikinga na janga hili.
Katika zoezi hilo wakili huyo alinukuliwa akisema "ukweli ni kwamba na niseme bila kuficha hali ni mbaya Arusha, msiposema ukweli tutazikana, ifike mahali muweke mguu chini na mseme ukweli bila kuogopa"
Hii inaenda kinyume na maelezo ya Waziri mkuu na kamati ya kupambana na janga hili wakati mkoa huo wa Arusha ukiwa na wagonjwa 7 tu kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya mpaka hivi sasa.

 
Ni vema Wakili angeliwashirikisha maofisa afya ili kubaini uhalisia wa hali mbaya.
 
Back
Top Bottom