Albert Einstein: Kutoka kuwa kilaza darasani hadi kuwa nguli wa fizikia

Kwa Tanganyika mpaka kuweza Kuwa back Technology hii sidhani tuna vitu vingi Sana vya kufanya kuliko kujiingiza kwenye matatizo haya name kwa uzembe WA watu weusi sidhani Kama tunaitaji technology hii japo kwa sasa ni muhimu sana hasa kwa mambo ya source of energy

Nishati pekee ambayo dunia inategemea yani Mafuta na Gas inakwenda kuisha pia ni gharama sana kuendesha nishati hizo mpaka sasa 17% ya umeme duniani unazalishwa kwa nishati ya Nuclear huku Ufaransa 75% ya umeme wanaotumia niwanishati ya Nuclear Duniani kuna Nuclear reactor 440 ambazo zinazalisha umeme wa 390,000 megawatts (MWe) katika nchi 31 pia kuna Nuclear reactor 60 zinajengwa maeneo mbalimbali duniani na zingine 160 zinatarajiwa kujengwa so unaweza kuona matumizi ya Nuclear kuzalisha nishati yakizidi kuenea Duniani pia kuna reactor ndogo ndogo 200 zinazooperate kwenye meli na submarine 150
Nuclear reactor yenye 508 MW capacity ndani ya saa 24 inaweza kuzalisha umeme wa 12,192 megawatthours (MWh) pia kutengeneza bomu la Nuclear ni process kubwa sana si kumiliki kinu cha umeme cha nuclear ukaweza kutengeneza bomu, kwani zipo Uranium za aina mbili yani Uranium-238 (U-238) na uranium-235 (U-235) sasa maajabu ni kuwa Uranium-238 (U-238) ndio nying sana duniani karibu 99.3% huku Uranium 235 (U-235) ambayo ndio unaweza kutengenezea bomu la Nuclear ni 0.7% ya hifadhi yote duniani toka mwaka 1789 bwana Martin Klaproth mwanasanyansi wa Kijerumani alipogundua madini ya Uranium na mpaka uweze kutengeneza Bomu moja la Nuclear unaitaji kuwa na 50KG za Uranium 235(U-235) hili kuweza kukamilisha chain reaction kitu ambacho ni kigumu sana na inachukua miaka mingi sana
Kwani sisi Tz tunashwnda wap hadi tusiweze? Tufanyaje ili iwezekane?
Cc
Palantir
 
Wazungu siwaaminiigii saaanaa..wamekaaa kujifanyaga wanajua kila kitu, japo of course wanajua kila kitu. Afrika maginiaz tupo wengi huenda na wewe ukawa mmoja wapo lakini mazingira tunakulia, aina za familia tulizonazo n.k. Ni nani atakaa chini ya mti anaenjaa anasubiri tunda lianguke ale. Mwenzetu tunda au jani limeanguka mtini ameshatengeneza na kufikiria theory. Kwanini tunatembea hatuanguki kwenye sayari hii ya dunia na inasemekana kwenye sayari ingine huezi tembea?

Tutasema yote mwisho wa siku mwanzo ndo msingi wa kila kitu.
Majiniazi mliogundua kukeketana sio? Shitholes bwana
 
Huwa nahisi kuna siri kubwa kwenye vyakula tunavyo kula, ukiachilia mbali mfumo wetu wa elimu. Mbona hatugundui na kuvumbua km wazungu? Japo tunapata AAA za PCM etc.
Sisi wazuri wa kusoma historia ya sayansi sio sayansi.Afrika tumenasa kwa sababu bado tunasumbuliwa na njaa nà maladhi na huwezi kuwa na nafasi ya kufanya utafiti kama bado unasumbuliwa na NJAA NA MALADHI
 
Hapo ndipo tulipokomea. Hatuangalii the other side of coin. Tanzania ya viwanda ni meipenda kwa moyo yote coz rasilimali tunazo, hapa nazungumzia malighafi. Rasilimali watu bado. Technolojia kwetu bado tatizo. Kampuni za simu zote ma co na executive officers ni wageni most of them. Kwanini? Ndivyo tulivyo. Aliyetengeneza rada awe sponsored, apelekwe kwenye vyuo mashuhuri ajifunze aje atusaidie. Tuende tukajifunze kwao, wao wanafanyaje na sisi tushindwe.

Kwa sasa hakuna cha kugundua kipya mpaka kesho theory za isaac newton na albert bado wanazitumia wazungu. Tufundishe kile kitakachomsaidia mwanafunzi mara baada ya kuhitimu masomo yake kwa maana elimu yake hapo ndipo inapoanzia.
Sio lazima kuvumbua hats kujitengenezea mwenyewe vitu itakusaidia we elimu yetu inatulazimu tuwe watumwa unaona maproffesor walio kesha wakisoma miaka kibao Leo hii wanamwangukia makonda nakufuata anacho kisema haijalishi yuko sahihi au LA
Hii nchi yechu alie aribu mfumo wa kwanza ni Mwinyi Maana viwanda vyote vilikuwa na Expart wakati wa Nyerere Kawaondoa kuwa nchi haina fedha kilicho fuata ni kubaki na maghofu mpaka sasa tumebaki na walimu wenye fikra za kukoloniwa kazi kuvaa miwani kama fashion ukiangalia hadi nyerere anatoka madarakan tulikuwa sawa na China eti Leo wanatukopa kwa mashart nafuuu hii nchi bhana


Leo hii mtian wa hesabu watu wanapewa multiple choice kwa mbwembwe eti darasa LA saba wanafuta unamchukua mwalimu wa sekondar akafunsishe primary wakati kazoea kutreat watu wazima unadhan watoto atafundisha nini mwishowe unamwambia mtoto wa primary refer vurugu tupu
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Majiniazi mliogundua kukeketana sio? Shitholes bwana

Kila mtu ni jiniazi kwa upande wake. Ni jinsi gani tu unavyofanya kwenye vile unavyoviamini. Unaeza kuwa yeyote unaetaka kua.
 
Tanzania itaamka pale tu wasomi watakapo achana na siasa na kuzifuata professions zao. Ya ngoswe tuwaachie yakina ngoswe. Umesomea mambo ya uchumi kama lipumba fanya mambo ya uchumi. Umesomea mambo ya udaktari fanya udaktari.
 
Kwani sisi Tz tunashwnda wap hadi tusiweze? Tufanyaje ili iwezekane?
Cc
Palantir
Mambo mengi yanachangia tushindwe, kwanza wataalam hatuna, pili gharama za ununuzi wa mitambo ni kubwa, hizi nuclear plant zinahitaji maji mengi sana katika uendeshaji wake ingawa bahari tunayo. Changamoto kubwa ni kwamba sisi bado tupo tunasoma tu introduction of physics wenzetu wana deal na application of physics hapo ndio tunapoachana
 
Ifike mahali siasa ziwekwe pembeni, wasomi wengi wa Tanzania hawa-apply elimu wanayoipata vyuoni kwenye real life badala yake hukimbilia kwenye siasa.
 
ALBERT Einstein ni mwanasayansi maarufu aliyeleta mapinduzi katika ulimwengu wa sayansi ambapo enzi za utoto wake walimu walimwita kilaza darasani.

Maisha ya awali ya Eistern hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu cha Intelligence Quotients- IQ (160-190).

Msomi huyu ambaye alianza kama mjinga, aligeuza ujinga wake kuwa mwanasayansi mashuhuri na katika historia ya duniani hatoweza kusahaulika.

Mwanafizikia huyu raia wa Marekani mwenye asili ya Ujerumani, alifanya mapinduzi ya sayansi ya fizikia, anajulikana zaidi kwa kugundua sayansi ya mabomu ya nyuklia.

Einstein alizaliwa mwaka 1879, huko Ulm, Ujerumani, alipata elimu ya awali katika mji wa Munich. Alikuwa mwanafunzi mwenye kiwango cha akili kidogo baadhi ya walimu wake walidhani kuwa ni walemavu wa akili (mentally handicapped); kutokana na kushindwa kuzungumza vizuri alipokuwa na umri wa miaka tisa.

Hata hivyo, alivutiwa na masuala ya asili ya ulimwengu. Alikuwa na hisia za ajabu ya kushangaza na aligundua kuwapo kwa nguvu isiyoonekana (Invisible forces) inayoongoza sindano ya dira (campass).

Alipokuwa na umri wa miaka 16 aliweza kufanya mahesabu ya kutatua na kufumbua masuala ya fizikia na uhandisi.

Einstein alimaliza elimu ya sekondari akiwa na miaka 16 na hakupenda kuendelea na masomo, akaamua kuachana nayo na kusoma mwenyewe huku akitafuta njia ya kuingia chuo kikuu.

Mwalimu wake akamfukuza kwa sababu ya mtazamo wake ambao ungeweza kuwaathiri wanafunzi wa darasa lake.

Einstein alijaribu kutuma maombi ya kujisajili na chuo cha Federal Institute of Technology (FIT) huko Zurich nchini Uswisi, lakini ujuzi wake wa masomo yasiyo ya hisabati hakuwa na uwezo nayo hivyo kusababisha kufeli mtihani wa kujiunga na chuo hicho.

Kwa ushauri wa mkuu wa chuo, alienda kujiunga na chuo cha Cantonal huko Aarau, Uswisi na kufanikiwa kupata diploma ambayo ilimwezesha kukubaliwa na chuo cha FIT mwaka 1896 ambapo alishindwa awali.

Akiwa hapo, alitambua uwezo wake mkubwa katika masuala ya fizikia kuliko hisabati.
Einstein alifaulu na kuhitimu katika chuo cha FIT mwaka 1900, lakini kwa sababu ya kutoelewana na mmoja wa profesa wake hakuweza kuendelea masomo kutokana na kukosa msaada wa fedha.
Mwaka 1902, aliajiriwa katika chuo cha Bern akiwa mkaguzi, nchini Uswisi, lakini baada kufikisha umri wa miaka 26 alitimiza vigezo vyote vya kumwezesha kufundisha chuo kikuu. Aliandika utafiti wake wa kwanza kuhusu mapinduzi ya sayansi.

Utafiti huo ulimpa umaarufu Einstein, na vyuo vikuu vikaanza kumgombania kwa huduma zake, mwaka 1909, baada ya kutumika kama mwalimu wa chuo cha Bern aliitwa kufanya kazi akiwa profesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Zurich huko Uswiss. Miaka miwili baadaye alichaguliwa kuwa profesa kamili katika Chuo Kikuu cha Ujerumani huko Prague, nchini Czechoslovakia. Ndani ya mwaka mmoja na nusu akarudi katika chuo cha FIT akiwa profesa kamili.
Hatimaye, mwaka 1913, wanasayansi maarufu wa Max Planck na Walther Nernst walisafiri kwenda Zurich kumshawishi Einstein kukubali kuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Berlin huko Ujerumani, pamoja kuwa mwanachama kamili wa Chuo cha Sayansi cha Prussia ambapo alikubali hiyo ofa.

Maisha ya awali ya Eistein hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu yaani IQ (Intelligence Quotients-160-190).

Einstein alianza kujulikana katika masuala ya Fizikia na umaarufu wake ulizidi kuongezeka kutokana na tafiti zake kukubalika, hatua ambayo ilizifanya kazi zake kupata sifa kem kem katika ulimwengu wa Fizikia.

Akiwa nchini Ujerumani, kipindi hicho chuki dhidi ya Wayahudi iliongezeka, Einstein alianza kupata mashambulizi kutoka kwa wanasayansi wenzake Philipp Lenard na Johannes Stark ambao walikuwa washindi wa tuzo za Nobel katika masuala ya Fikizia.

Wanafizikia hao walianza kuhusisha nadharia ya Einstein kuwa ‘fizikia ni Kiyahudi.’ (Theory of Relativity) hivyo, mwanasayansi huyu alijiuzulu kutoka Chuo cha Prussia cha Sayansi mwaka wa 1933.

Kwa mara kadhaa, Einstein alikuwa akitembelea Chuo cha California Institute of Technology nchini Marekani, ambapo safari yake ya mwisho mwaka 1933 alipewa nafasi katika Institute for Advanced Studies huku Princeton, huko Massachusetts.

Akiwa nchini Marekani, mwaka 1939 Einstein alikuwa mstari wa mbele katika utengenezaji wa bomu la atomiki, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo, Franklin D. Roosevelt kuelezea kuwa Wajerumani wamepiga hatua katika maendeleo ya sayansi, kwamba Adolf Hitler anaweza kuwa wa kwanza kutengeneza silaha za atomiki.

Hii ilichochea jitihada za Marekani kutengeneza bomu la nyuklia. Einstein alishtuka na kusikitishwa kutokana fumbo maarufu la Fikizia E = mc 2 ambalo lilionyesha njia ya kutumia katika kutengeza bomu la nyuklia ambalo lililolitumika kulipua mji wa Hiroshima nchini Japan, mwaka 1945.

Einstein alifariki Aprili mwaka 1955 kwa maradhi ya tumbo. Kabla ya kufariki, aliomba mwili wake uchomwe moto, lakini tukio la kushangaza mtaalamu wa magonjwa ya damu (pathologist), Thomas Harvey aliondoa ubongo wakati mwili wake ukifanyiwa uchunguzi. Harvey alichukua ubongo ili kutafuta siri ya kiwango cha akili yake (genius).

Baada ya kupata kibali ambacho kilikuwa kinakataliwa kutoka kwa mtoto wa kiume wa Einstein, Harvey baadaye aliukata ubongo wa Einstein vipande vipande na kuupeleka kwa wanasayansi mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi. Tafiti kadhaa zimefanyika kuhusiana na ubongo wake tangu miaka ya 1980, lakini matokeo yake yamekuwa yakikataliwa au kutopewa heshima yoyote.

Lakini mwaka 1999, uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Canada ilichapisha utafiti wenye utata unaodai Einstein alikuwa na ukuta usio wa kawaida katika sehemu ya ubongo uliompa uwezo wa Hisabati.

Wakati Albert Einstein anaendelea kutengeneza fedha nyingi, ingawa alifariki mwaka 1955; mwaka huu jarida la Forbes lilimtaja katika nafasi ya 10 kuwa miongoni mwa watu waliokufa lakini wanaendelea kuzalisha fedha. Einstein mwaka huu pekee amezalisha Dola za Marekani milioni 10 kutokana na jina na sura yake kutumika katika bidhaa, mabango, kompyuta, roboti na mifuko.
Hakuwa mmarekani

Alikuwa ni muisrael pure alikuwa ujerumani Kabla ya Vita vya 2 vya Dunia kama ilivoa ada kuwa wayahudi wengi sana walikuwa ujerumani lkn hakuwa RAIA wa ujerumani

Baada ya Hitler kuanza kuwauwa wayahudi Albert Einstein pia alikamatwa mda huo vita vga 2 vya dunia vimeanza

Alipokamatwa tayari Hitler alikuwa ashaambiwa kuwa huyu MTU anaweza kuimaliza vita vya 2

Alipofikishwa kwa Hitler, Hitler alimwambia atengeneze Bomu litakaloifanya ujerumani kushinda vita huku akimwahidj kumpa Mali na uraia

Einstein akamwambia apewe masaa 48 wakamwachia

Einstein akatorokea USA ndipo akakutana na Raisi Roosevelt akaeleza kila kitu akaahidiwa uraia ili afanye yake

Einstein akaingia maabara akaja na michoro na namna ya kutengeneza hayo mabomu

Haya ndo mabomu 2 yaliyoiangsmiza Japana vita vya 2 vya dunia Hiroshima na Nagasaki

Ni.kazi.ya Alber Einstein
 
Back
Top Bottom