Albert Chalamila: Mimi ni mwanasiasa nisiyeendekeza njaa, nina degree za kutosha hivyo siyumbishwi!

Tabia ya wizi kwa wengi ma DC, RC ni kawaida, udhulumu moja kwa moja wananchi, wakurugenzi wao kwenye miradi, mbunge inabidi akae kimya ili waelewane vinginevyo ni ugomvi!
 
Kwanza wanabodi waombe msamaha kwa kumwita Chalamila ni RC msitafu,sema RC wa zamani wapi alikwambia amesitafu?
Pia Kama hana njaa mbona bado anapiga kelele? Ulimuona wapi Mwanri Agrey akipiga kelele?
RC Mtumbuliwaji😅
 
Elimu yake haikumsaidia , ndiyo maana alifukuzwa kazi,kizembe kwa kuhimiza wananchi wa Mwanza,wajitokeza kwa wingi na Mabongo ya malalamiko kwenye ziara ya Rais mkoani Mwanza.Hii Ni kielelezo tosha kuwa hajaelimika au Elimu yake haikumsaidia kutatua changamoto za wananchi wake.Aache kujiliwaza au ni Kiki ya kutokea hadharani baada ya kukaa kimya toka amefukuzwa
 
We ni mjinga Chalamila alifanya hivo mkusudi ili atumbuliwe alijua hawezi kufanya kazi na mama! Maana mama ni mtu asiyejisimamia!
 
Akihutubia kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa shule ya Range Primary & Sec school mjini Ilula RC mstaafu Albert Chalamila amesema yeye amesoma UDSM kwa miaka 7 na ana degree, post graduate diploma na Masters za kutosha hivyo hana njaa.

Chalamila amesema viongozi wengi wakiteuliwa wanaendekeza wizi wa mali za umma ili wasistaafu wakiwa maskini lakini yeye hakuwa mmoja wao kwa sababu elimu yake ni mtaji.

Chalamila amewataka wanafunzi kuzingatia masomo wawapo shuleni na wasiendekeze makundi, ndio maana hata yeye alipokuwa RC wa Mbeya aliwachapa viboko wanafunzi waliochoma mabweni

Jumaa kareem!
Yeyote ajiitaye msomi huyo ni kilaza namba moja, wasomi halisi huitwa wasomi kutokana na matokeo ya kazi zao popote wafanyapo kazi.

Uko wapi usomi wa Chalamila?
 
Back
Top Bottom