Albamu Ya Ameniponya Kuzinduliwa Leo"

// Ad Code here

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
54,784
27,570
Albamu ya Ameniponya kuzinduliwa leo Dar


Na Amina Athumani

WAZIRI wa maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya Ameniponya itakayozinduliwa leo katika ukumbi wa Landmark Hotel jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam ,Mkurugenzi wa Air Source Afrika , Stephen Jutta ambao ndio walioiandaa albamu hiyo, alisema ina nyimbo nane na zimetengenezwa na kuimbwa na mwimbaji wa nyimbo za Iinjili na muigizaji wa filamu za kijamii Catherine Kyambiki.

Alisema, Katherin anatarajia kupanda jukwaani akiimba nyimbo mpya na za zamani huku albamu yake mpya ikiwa na lengo la kuikomboa jamii katika mambo mbalimbali.

Alisema mbali na uzinduzi huo pia kutakuwa na wasanii watakaotoa burudani ambapo kutoka Kenya ni Subi Mgau, wakati kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watakuwepo Garvar Group na Tanzania atakuwepo Upendo Safari, Papa G na Joseph Mwasulama pamoja na wageni mbalimbali.

Naye Catherine alisema kutokana na kutosikika kwa muda mrefu amepania kuwapa burudani ya kuimba pamoja na kupiga gitaa katika baadhi ya nyimbo zake atakazozizindua.

Alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Ameniponya, Wewe ni Bwana, Mikononi mwa Bwana, Baba niongoze na Mungu Niponye.
 
Back
Top Bottom