Billie
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 12,720
- 19,860
Roger alikuwa anamfundisha dada yng na pia alikuwa na uhusiano nae.Ila Roger alisifika kwa akili nyingi pale shule ya secondary Pugu high school walijuana na dada kwa kuwa alikuwa anasoma pale form 3(enzi zile Pugu palikuwa kuna mtaala wa shule za tasisi) ila Roger alikuwa form six.Alizoeleka kuja nyumbani mara kwa mara na mimi nikiwa rafiki yake mkubwa coz huwa akija lazima aje na zawadi yangu.WALI AHADIANA KUONA ila Roger alifaulu na kuchaguliwa Makerere University (Uganda) na dada akabaki pale Pugu ili amalize form four yake kibaya zaidi hawakuwa na simu kama unavyojua simu enzi zile zilikuwa zinamilikiwa na watu wenye uwezo wa juu.ILA nilipata kumsoma dada yangu vile hali yake haikuwa sawa kutokana na Roger kuwa mbali nae .Miaka minne mbele Roger alirudi kutoka Uganda na akaja mpaka shule ya msingi niliyokuwa nasoma kwa kuwa pale tulipokuwa tumepanga tulihama baada ya Mama kujenga nyumba yetu(single parent family) ndipo nikapanda kwenye gari alilokuwa amekuja nalo baada ya kuniombea ruhusa pale shuleni kwa vile nilikuwa mdogo enz zile nilijikuta kumsahau kidogo kwa vile alikuwa amenenepa kiasi chake.Basi njiani tulikumbushana na akaniuliza swali "nimekuja kumuona dada yako na mama hivi wapo"?nikamjibu "wapo"Akaongeza swali lingine dada yako kaolewa? Mi nikajibu "hapana ila anaishi kwake na mmewe".Roger akatamka "SHIT"na akagonga usukani wa gari na honi ikalia.Ila hakukoma kuuliza " Ana mtoto?"mi nikajibu "hapana ila ana mimba kubwa"Ghafla akapiga breki na kusikitika sana.
Tukafika nyumban bahati nzuri dada alikuwa yupo pale home kwa ajili ya uangalizi wa ujauzito wake wa kwanza(kwa mama) Gari lilipaki na hatimaye tukashuka mama alikuwa wa kwanza kutuona na hatimaye dada yangu ila cha kushangaza Dada na Roger walikimbiliana na kukumbatiana kwa furaha hadi machozi yakawatoka.Walikataa kukaa sebulen na kuniagiza viti ili wakae nje.Mama cha kushangaza akabun kasafari ili kuwapa nafasi wazungumze Nilichokiona ni kuwa walikuwa wanaliliana tuu kwa kuwa mi nilikuwa nawachungulia pale nje kupitia dirisha la chumba chetu na namimi nikajikuta namkumbuka rasmi Roger kutokana na zawadi zake ambazo zingne nilikuwa nazo kama Uniform za mpira(jes),na mkebe wa vifaa vya shule.
Tuishie hapa na ntaendelea ila nataka kujua nani alaumiwe ikiwa dada anasema alisubiri kutokana na kutokuwa na mawasiliano kulimtisha ndo akajikuta ndani ya mikono ya mume mwingine na Roger yeye anasema alipatwa na tatizo la kifedha ndio maana ikamladhimu kubaki kwa rafiki yake Mganda huku wanafanya tenda mbalimbali ikiwemo ualimu ndo maana hakuweza kurudi hadi pale alipomaliza degree yake na pia anasema ameshatuma barua 3 kwa anuani ya Pugu high schooa dada hakuzipata hizo barua.
TUENDELEEENI JAMANI:Kwanza naomba samahani kwa kuikatisha maana haikuwa kusudio langu betri iliisha coz natumia simu kupost hii story.
Nilitoka dirishan nakabadili nguo zangu na kwenda kufunua ma Hot pot kucheki wameniwekea nini Nikala nikaenda kucheza(maisha ya uswahili coz sikuwa get kali) Basi kurudi kutoka kwenye mpira sikumkuta mgeni wala dada mama ila nilikuta nimeachiwa Sh elfu 20 za kibongo ila mama alizizuia nakusema ngoja Nikuwekee ntakuwa nakupa kidogo kidogo .Ila mida iliyoyoma hadi ikafika saa 2 usiku sikumuona dada kurudi kwa kuwa niliambiwa kapanda gari na kaenda kumsindikiza mgeni.PUNDE SI PUNDE hazikupita dak 5 nikaona mwanga mkali wa gari ukimulika kuelekea nyumba yetu ilikuwa gari ile ile ya Roger akamshusha dada na akaniulizia mimi dada aliingia ndani na kuniita.Nikaenda mpaka kwenye gari nikatoa shukrani kwa ule mzigo akanisifia sana kuwa mi nilikuwa mtoto mzuri kwan walimu walinisifia sana na kumuonesha faili la maendeleo yangu pale skuli.Na alianza kunijaza moyo kuwa nisome sana hata kama kwetu hakuna uwezo na kunipa vijihabari vya shida alizopitia yeye wakati anasoma na kuapa kuwa hatavumilia kuona zile shida zikinurudia mimi kifupi akanipromise kunisuport kifedha.JAMAA AKAONDOKA ILA SASA kila weekend alikuwa anakuja na gari na kumwaga zawadi na kusindikizwa na dada kama kawa kurudi saa 2 hadi 3 na mbaya zaidi tripu hiz zingine dada alikuja ananukia arufu ya pombe na ulegevu fulani hivi wa kilevi.Kuna siku kama 2 hivi Mme wa dada na Rodger walishawahi kugongana ila walisalimiana na kukaushiana tuu.Baada ya tukio hilo mmewe dada akaibuka na issue ya kutaka kumuoa dada(kubaliki ndoa kwa wakatoliki wanajua hili) ila dada alipinga kwa hoja yake kuwa hawezi kufunga ndoa na TUMBO KUBWA vile kulitokea mvutano mkubwa sana kwenye hili hadi mme wa dada akaona kashindwa kwenye hili, miez kadhaa mbele dada akajifungua mtoto wa kiume na mmewe akarudisha ombi lake la kutaka kumuoa ila dada akakana na akatoa sababu ya kuwa mwili wake haukukaa vizuri baada ya kujifungua so akamuomba mumewe ammpe muda atakapo hitaji ndoa atamuambia yeye mwenyewe.LIKAIBUKA lingine la namba inapiga mara kwa mara kwa dada na kumfanya mmewe apandishe jazba na kuleta mashtaka kwa mama.Akidai kuwa anakuta nakala za sms za kutumiwa voucher nyingi kama elfu 20 au 25 mara kwa mara