Alamu spesheli

Kamuzu

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
993
298
Jamaa mmoja alikorofishana na mke wake kiasi cha kuishi bila kuongea kwa muda, mawasiliano ya ndani yalikuwa yanafanyika ama kwa ishara au kuandika kwenye karatasi na kuiweka mezani na kuchukua majibu baadae.

Hali iliendelea hivyo mpaka siku moja jamaa akiwa anajiandaa na safari ya kwenda nje kikazi, ilibidi aandike ujumbe wa kumweleza mkewe amwamshe ikifika saa 9 usiku ili awahi kufika uwanjani, maana anajijuwa kuwa ni mlalaji mzuri na hakuwa na simu wala saa ya kuweza kutega alarm, hivyo akaamua kutumia kalekale ka utaratibu kao. Akaandika 'ikifika saa 9 niamshe niwahi ndege,' kisha kama kawaida akaweka mezani na kulala. Mwanamke aliuona ujumbe huo, naye akalala. Ilipofika saa tisa usiku, jamaa akiwa bado anakoroma, mwanamke akaamka, akachukuwa kalamu na kuandika, 'saa tisa imefika amka uwahi ndege' kisha akarudi kulala. Kidume alipoamka ilikuwa kweupeeee amechelewa tayari.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom