Alama ya ishara ya kidole ni vipi itafsiriwe kama tusi ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Wadau awali nilipata changamoto ya fikra thread hii niiweke jukwaa lipi ! Hatimae nikajiridhisha kua hata MMU itafiti, kwani nikikusudiacho kinaweza kuvunja/kuhatarisha MAHUSIANO & URAFIKI.
Kwamba inapotokea mikwazano ya kawaida baina ya mtu na rafikie, ama mtu na mpenziwe mmoja kati yao akimuoneshea alama ya ishara ya KIDOLE kirefu cha katikati mkonononi (haijalishi kiwe cha mkono wa kulia au kushoto).
Kidole hicho huashiriwa kwa kuelekezwa juu kikielekezwa kwa aliekusudiwa.
Nimeshuhudia hili mara nyingi na ambapo kifuatacho ni Dhahma, ugomvi, kupigana na amani kutoweka kwa wanaohasimiana. Binafsi yangu napatwa na mashaka kwamba hii ishara imepata ithibati kutoka Taasisi za kisheria kwamba ni tusi rasmi ?
Aidha naomba kuelimishwa, kama ishara hii iko recognise Mahakamani kua ni tukano ?
Nawasilisha.
 
Mh kwa kawaida ni tusi ila kisheria hata sina uhakika km TBS (Wahusika wa lugha) wamehusishwa. Ila kwa mitaani ni bonge la tusi
 
tusi la kimataifa, kuna mchezaj england jina ckumbuki, alifunga gol akawaonyesha kidole kwa mashabik pinzan akafungiwa mech kadhaa.
 
labda ungepeleka jukwaa la sheria ili asaidiwe kujua kama ishara hii inatambulika kisheria

Au ipelekwe kwenye jukwaa la siasa ili kujua kama inakubalika kisiasa, maana cdm wananyoosha kwa mtindo wao, ccm pia. Ila cdm wakikutana na wanaccm basi wanawapa dole la k.ati, baadaye ni vurugu
 
Mbona yapo maalama mengi tu yanamaanisha matusi we umeona hilo tu judge.
 
ni ishara ya tusi, si unajua mara nyingi kidole hiko ndicho kinachotumika kwenye kuchokonoa bungo linapoliwa!? Sasa ukimuonesha m2 hiko kidole ndo unaashiria mambo yetu yaleee......
Sijui km kisheria ni tusi, lkn ni ishara inayojulikana duniani kote.
Nyengine ni ile kumuonyesha mtu mkono either uwe wa kulia au wa kushoto unafanya km unaupinda hivi then unamuonyshea mtu km unaemsukumia vile. Hii ukimfanyia m'me ndo noma zaidi mana afadhali kwa m'ke kutiwa ni kawaida.
 
tusi la kimataifa, kuna mchezaj england jina ckumbuki, alifunga gol akawaonyesha kidole kwa mashabik pinzan akafungiwa mech kadhaa.
Christiano Ronaldo enzi yupo Man U aliwahi pata adhabu kwa kuwanyooshea mashabiki kidole cha kati, baada ya kuzomewa..
 
Back
Top Bottom