ALAMA ya 666 tuipokee, Itarahisisha mengi. Watu waache kupotosha.

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
3,688
2,000
ALAMA YA 666 TUIPOKEE, ITATUSAIDIA KWA MENGI.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kwa waliosoma jumbe zangu nyingi watagundua kuwa Mimi ni mwandishi wa maandiko huru. Nayaandika haya Kwa wapenda Uhuru, wenye Fikra huru, lakini Uhuru wenye maarifa yenye akili.

Sikatai Dunia inamakundi yanayohasimiana, kila kundi Kwa ufundi hutaka ushindi. Makundi yote mawili hutaka mamlaka na Utawala dhidi ya binadamu. Kuishi ni kuchagua kutawala au kutawaliwa. Vyovyote iwavyo lazima tuishi, kushindwa kuishi ni kushindwa kutawala hivyo kutawaliwa ndio mwanzo WA kushindwa.


Kundi moja hutaka kutawala watu wakiwa WATUMWA wakati kundi la pili hutaka kutawala watu wakiwa WATU HURU.

Naweza kuyapa majina makundi haya mawili ili kurahisisha Uelewa Kwa wasoma jumbe hii.

1. Kundi linalotaka kutawala watu wakiwa WATUMWA nimelipa jina " UTUMWA HURU (UTH 07)"

2. Kundi linalotaka kutawala watu wakiwa Huru nimelipa jina " UTASHI Huru ( UTH 06)"

Nitatumia "UTH 07" na " UTH 06" Kama code zinazowakilisha makundi tajwa hapo juu.

Code 06 ni namba inayowakilisha utawala/ milki ya binadamu.

Code 07 ni namba inayowakilisha utawala/ milki ya miungu.

Wafuasi WA UTH 07 ndio waliochelewesha maendeleo ya Dunia Kwa sababu wanapenda kutawala watu wakiwa WATUMWA. Hawapendi watu wawe huru, na hii hupelekea watu kukosa ubunifu na uvumbuzi wa mambo yatakayomsaidia mwanadamu kuishi maisha ya Raha mustarehe.

UTH 07 ndio walioweka matabaka katika jamii ya mwanadamu,

Silaha kubwa ya UTH 07 ni Imani ambayo huijenga kupitia dini. Dini nyingi kama sio zote zinamizizi ya UTH 07.

Tofauti na UTH 06 ambapo silaha kubwa kwao ni Akili/utashi na maarifa, kupitia elimu ambayo ni matokeo ya tafiti.

Vita iliyopo sasa ni baina ya UTH 07 dhidi ya UTH 06 katika kuwania utawala wa kuongoza wanadamu.

UTH 06 hawanaga maneno mabaya kwa UTH 07 kwani moja ya kanuni zao ni kuwaacha watu wawe huru katika utashi wao. Hii ni tofauti na upande wa UTH 07 ambao ni wafuasi wa miungu isiyoonekana. Hawa huwa na majungu na kashfa Kama sio matusi Kwa wafuasi WA UTH 06.

Ni kawaida kumsikia Mfuasi wa UTH 07 akimtukana Mfuasi wa UTH 06 Kama Mfuasi wa Shetani.

UTH 07 kupitia dini wameshawatawala watu kifikra na kuwafanya watumwa. Hawapendi maswali mengi na Kwa vile wanaamini katika miungu basi nao hujigeuza sehemu ya miungu hiyo.
Ni ngumu Sana kumkosoa Mchungaji, Askofu, au Kuhani Kama sio Nabii Kwa wafuasi WA UTH 07 na huenda ikawa kosa kubwa Kwa atakayefanya hivyo. Kwani wao hulazimisha watu kutumia uoga kufikiri wakiita hiyo ndio Imani kwao.

Wafuasi WA UTH 07 wanapenda kuwekea watu visheria vyao kwani huwafanya Kama watumwa. Sheria za vyakula, kuwa ule hiki na usile hiki, vaa hivi na usivae vile, oa huyu na usiolewe na Yule. Basi ilimradi.

Mara nyingi huruhusiwi kuuliza Kwa nini nisile hiki na Nile kile, Kwa nini nivae hivi na nivae vile. Ukiuliza watakuambia unakufuru au hauna adabu.

Hii ni tofauti na UTH 06 ambao huruhusu Utashi huru kufanya kazi zaidi kuliko utumwa huru.
UTH 06 wao wakikukataza Jambo hutoa sababu ya kutokulitumia na unapewa na elimu ukitaka, pia unaruhusiwa kuuliza maswali yoyote yatakayokuja akilini.
UTH 06 hawakupi mipaka isipokuwa unapewa Uhuru katika njia yako isiingilie Uhuru wa mtu mwingine.

UTH 06 wamejikita zaidi kurahisisha maisha ya binadamu kuwa rahisi Kwa kuvumbua Teknolojia zitakazowarahishia wanadamu katika Mazingira wanayoishi.

Moja ya Teknolojia muhimu ni pamoja na mabadilishano ya Mali baina ya mtu na mtu au makundi ya watu ambayo huitwa Biashara.

Zamani kabla ya Teknolojia ya Pesa kuvumbuliwa na Wana UTH 06 kulikuwa na mfumo wa ubadilishano wa Mali Kwa Mali ambao Kwa lugha ya wakoloni huitwa Barter Trade system. Biashara zilikuwa ngumu mno katika mfumo huu.
Katika kurahisisha Biashara, au mabadilishano ya mali, bidhaa na Huduma Wana UTH 06 wakavumbua Mfumo wa Sarafu/pesa.

Mfumo huu wa kutumia pesa umerahisisha maisha yetu, wote tumashahidi, mpaka sasa mfumo huu upo.
Lakini kutokana na Ongezeko la bidhaa na Huduma kuwa nyingi mfumo wa Sarafu nao unapitwa na wakati.
Imeingia mifumo mipya Kama vile yakutumia Code za kieletroniki kupitia Benki au simu zetu.

Wana UTH 06 wanazidi kuifanya dunia iendelee kuwa sehemu salama na yakufurahia. Usalama wa pesa/Mali zetu unazidi kuimairishwa.

Teknolojia inavyozidi kukua itakuwa vizuri Kama Mifumo ya ubadilishano wa Bidhaa, Huduma na Mali utawekwa katika miili yetu.
Hiyo ndio Wana UTH 07 huita 666 na kuisema Kama alama ya mnyama au ya Shetani Jambo ambalo ni uongo wa mchana.

Wanachojaribu kuwadanganya watu na kuvumisha propaganda zao ni katika namna ya kutapatapa nafasi Yao isipokwe na Wana UTH 06.

UTH 07 hupenda kuwatumikisha watu katika utumwa wao wabaki kuwa wakubwa.

Niishie hapa.

Ni yule;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 

elishaezekiel

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
330
1,000
Son of man, remember that you are mortal and in the end, God wins.

Have you seen a dead man? How helpless he is!!!!
Let not this breathe of life deceive you!!
That you speak to the point of blasphemy.
Have you thought of your death? Of your own Mortality? How You will lie covered with sand in your Grave?

Have you thought of how you walk, how you breath??
Are you even aware of your nature?
Do you see your intestines behind your belly? Your heart and your lungs behind your ribs??
Are you aware of them?
Your brain behind your skull??

Have you even thought of these things??

Your skeleton??
Or the skin and the muscles!!

Who arranged these things and kept them in order?
Don’t be deceived!!
Do you even know that the earth is floating in space??? How big is this space??
Have you thought of the nature of the sun, the moon??Don’t be deceived...
A wise man is not obsessed with the beginning of things but how things end even for himself...
 

Chris_Mike

Senior Member
May 5, 2019
149
250
Son of man, remember that you are mortal and in the end, God wins.

Have you seen a dead man? How helpless he is!!!!
Let not this breathe of life deceive you!!
That you speak to the point of blasphemy.
Have you thought of your death? Of your own Mortality? How You will lie covered with sand in your Grave?

Have you thought of how you walk, how you breath??
Are you even aware of your nature?
Do you see your intestines behind your belly? Your heart and your lungs behind your ribs??
Are you aware of them?
Your brain behind your skull??

Have you even thought of these things??

Your skeleton??
Or the skin and the muscles!!

Who arranged these things and kept them in order?
Don’t be deceived!!
Do you even know that the earth is floating in space??? How big is this space??
Have you thought of the nature of the sun, the moon??Don’t be deceived...
A wise man is not obsessed with the beginning of things but how things end even for himself...
Ume ongea mazito sana kiongozi, tusiruhusu hii pumzi ya maisha itudanganye
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
173,182
2,000
giphy.gif
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom