KWELI Alama nyeupe zinazoonekana angani ndege zikipita Siyo Moshi unaotolewa na Roketi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
photo_2024-11-25_10-30-36 (2).jpg

photo_2024-11-25_10-30-36.jpg
 
Tunachokijua
Roketi ni chombo cha usafiri kinachotumia nguvu za mlipuko au uchomwaji wa mafuta maalum ili kusafiri kwa kasi kubwa kuelekea angani au hata anga za mbali. Mafuta ndani ya roketi yanapochomwa, hutoa gesi kwa kasi kubwa kuelekea chini/nje, na kusababisha roketi kusukumwa kuelekea juu.

Roketi sio ndege wala chombo kamili bali ni aina ya injini inayofungwa kuendesha chombo cha anga kwenda kasi au kwenga anga za juu zaidi au nje ya Dunia, mfano, vyombo viendavyo kasi au anga za mbali kama vile Space_Shuttle, Satellite, Space_Module, Makombora {Missiles} n.k.

Ni injini ya kipekee na inaweza kufanya kazi katika mazingira mengi magumu ikiwemo ndani ya maji na nje ya dunia {Space} ambako hakuna hewa yoyote ya kuweza kuvutwa ili kuwasha injini ndiyo sababu 'rocket' huwa inabeba hewa yake yenyewe ya Oxygen na mafuta ndani ili kuweza kufanya kazi popote.

Kumekuwapo mistari kama moshi inayoonekana mara kadhaa nyuma ya baadhi ya ndege zikipita huku mistari hiyo ikidaiwa kusabishwa na Roketi.

Je, ni kweli mistari hiyo ni Moshi unaotolewa na roketi?

JamiiCheck imepitia machapisho mbalimbali na kubaini kuwa mistari inayoonekana nyuma ya ndege inapokuwa inapita siyo Moshi bali ni mvuke unaotolewa na injini ya ndege kutokana na joto kali la injini ambapo mvuke wenye joto ukikutana na baridi kali angani husababisha kuganda na hivyo kutokea kwa mistari(contrails) ambayo hudumu kwa muda na baadaye kufutika, Contrails hutokea kwa ndege inapokwenda anga ya juu sana.

Vilevile, kuna mistari hutokea wakati ndege ikimwaga mafuta ambapo mistari hiyo hufutika kwa haraka zaidi. Mistari ya contrails inatofautiana na ile inayojichora wakati ndege ikimwaga mafuta ikiwa angani. Ndege kumwaga mafuta angani kitaalamu FuelDump au Jetsoning ni utaratibu wa dharura unaofanywa na rubani kutoa mafuta nje ya tanki za ndege ikiwa angani.

Mara nyingi ndege kubwa na za kati zina uwezo wa kumwaga mafuta angani kupitia matundu maalumu 'Nozel' yaliyopo nyuma ya mbawa endapo itapatwa na dharura inayohitaji kutua haraka hasa pale muda mfupi baada ya kupaa.

article_5009001853_1x.jpg

Kwa mujibu wa National weather service wanaeleza kuwa mistari inayojichora nyuma ya ndege ni Mistari ya contrails hutengenezwa wakati mvuke wa maji moto unaotolewa na injini ya ndege baada ya kuchomwa kwa mafuta unapotolewa kwa kasi nje na kuwa matone au chenga za barafu kutokana na baridi kali sana katika angahewa ya Dunia. Ili condensation itokee, hali ya hewa inapaswa kuwa ya baridi kali sana na unyevunyevu wa kutosha.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Rocky Mountain (RMI), contrails mara nyingi huundwa katika urefu wa kawaida wa ndege zinapopaa, kati ya futi 32,000 hadi 42,000 (sawa na mita 10,000 hadi 13,000) katika tabaka la juu la troposphere, Hii ni kwa sababu mistari inayojichora (condensation) mara nyingi hupatikana katika urefu huo. Japo mara chache hutokea kuanzia futi 25000 kutegemeana na hali ya hewa ya eneo husika iwapo lina kiwango cha baridi kali.

144789028_853560398759071_2137099163242843915_n.jpg

Hivyo basi, Roketi pamoja na ndege zote zenye uwezo wa kupaa kwenda anga la juu zaidi kuanzia futi 32000 huweza kusabaisha mistari hiyo, kwani hufikia anga lenye hali ya hewa ya baridi kali hufanya mvuke unaotolewa na injini ukikutana na baridi kali huganda hewani na kusababisha kuonekana kwa mistari, mara nyingi ndege kubwa zote kama Jet nk hupaa kufikia usawa huo na kuacha mistari. Kwa kuwa angahewa hubadilika mara kwa mara, hali zinaweza zisiwe sawa kwa contrails kutokea katika urefu huu. Hii ndiyo sababu si kila ndege huunda mistari ya contrails kila inapopaa kwani bila baridi kali contrails haziwezi kuonekana.
Huo siyo moshi. Inafahamika kwa kizungu kama Chem-trails.
kutokana na kuwa kule juu angani kuna baridi kali hewa huwa imebana sana hivyo joto kutoka kwenye engine za ndege zinakuwa kama zinachemsha hiyo hewa ndo hiyo mistari unayoiona.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom