Alama na michoro ya barabarani (SADC)

decomm

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
726
655
Amani iwe kwenu.

Katika uzi huu tutakuwa tunajifunza / kukumbushana alama na michoro ya barabarani za SADC.

Alama na michoro hii ipo takribani 178.

Leo nitaanza na mchoro namba 173 na 174.

Hii ni mistari inayokaribia kufanana lakini ina maana tofauti kabisa ambapo medereva wengi huichukulia kama yote ni kama namba 174 (kwa maana ya kwamba mstari #173 madereva wengi hawaujui na pia hao wachoraji barabarani hukosea kuichora ipasavyo)

#173 ni mstari wa ONYO / TAHADHARI, unaelekea UKANDA WA HATARI (hivyo usiovateki)

#174 ni mstari unaotenganisha njia ya kuendeshea katika barabara (unaruhusiwa kuovateki kama ni salama)

Pia madereva wengi wamekaririshana kwamba mistari ya dash dash unaruhusiwa kuovateki ambapo si muda wote ni sahihi.

Sehemu kama IYOVI (Mikumi - Ruaha Mbuyuni) mistari hii ilitakiwa ionekane waziwazi, lakini ni sehemu chache sana imechorwa kwa usahihi.

Leo wewe umepata bahati ya elimu hii basi ifuatilie, kisha uelimishe na madereva na watumia barabara wengine.

Nimeambatanisha picha ya mistari hivyo kama inavyooneshwa kwenye 'high way codes' ama kwenye vitabu vya mafunzo ya udereva.
___
#Usalama barabarani ni jukumu letu sote.

__
D.
IMG-20191112-WA0000.jpeg
 
Ni matumaini yangu kuwa somo la mistari ya dash dash ya 'kuruhusu' kuovateki kama ni salama na kukataza kuovateki kwa kuwa unaelekea ukanda wa hatari limeeleweka.


Leo tujikumbushe / tujifunze alama za mwisho wa katazo, ambazo madereva wengi hawajui kutafsiri ipasavyo.

Mfano wa alama hizo katika michoro na alama za barabarani za SADC ni #80, #82 & #84 (angalia picha nimeambatanisha)

Hiyo mistari iliyokatiza kuonesha zuio kwa mukhtadha wa leo huwekwa minne ya rangi nyeusi ama kijivujivu, na kila mstari huwakilisha mita mia moja.

Hivyo basi, tafsiri sahihi ni kama ifuatavyo:-

#80 = Mwisho wa amri inayokataza gari moja kulipita lingine.

#82 = Mwisho wa amri inayokataza gari la mizigo kupita gari lingine.

#84 = Mwisho wa amri inayokataza kuendesha kwa zaidi ya kilomita themanini kwa saa.

Ahsante kwa kufuatilia.

Kwa wenye maswali kuhusu alama na michoro mingine ya Africa Mashariki na SADC karibuni.

___
D
IMG-20191113-WA0000.jpeg
IMG-20191113-WA0001.jpeg
IMG-20191113-WA0002.jpeg
 
Labda pengine utusaidie reference ya sheria exactly at least soft copy inavyo specify hii mita 400
 
Kwakuwa huu ni mwezi ambao wadau wengi husafiri, na kwa kuwa huduma za gari moshi zinafanya kazi basi ni vyema tukajikumbusha (tukajifunza) alama muhimu unapokaribia makutano ya barabara na reli.

Lengo ni kuzingatia alama na michoro ya barabarani na kuacha mazoea.

Alama hizo muhimu ni alama namba 40 hadi 46 kwenye orodha ya alama za barabarani za SADC & EA.

#40. = Onyo (tahadhari), mbele kuna makutano ya reli na barabara yenye kizuizi

#41. = Onyo (tahadhari), mbele kuna makutano ya reli na barabara yasiyo na kizuizi.

#42. = Onyo (tahadhari), kuna mita mia tatu kufikia makutano ya reli na barabara.

#43. = Onyo (tahadhari), mbele kuna mita mia mbili kufikia makutano ya reli na barabara.

#44. = Onyo (tahadhari), mbele kuna mita mia moja kufikia makutano ya barabara na reli.

#45. = Onyo (tahadhari), mbele kuna njia moja ya reli.

#46. = Onyo (tahadhari), mbele kuna njia za reli zaidi ya moja.

Note: Ukiwa unaendesha gari, Sheria inakutaka usimame mita tano kabla ya kuifikia reli, angalia usalama, ndipo uvuke kama ni salama.

(Samahani kwa picha zilizofifia)
IMG-20191213-WA0000.jpeg
IMG-20191213-WA0001.jpeg
IMG-20191213-WA0003.jpeg
IMG-20191213-WA0002.jpeg


decomm!
 
Back
Top Bottom