Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,561
- 19,056
Highway ya kuanzia Ubungo mataa hadi Kibaha ipo katika hatua za mwisho kukamilika. Ni barabara nzuri sana yenye upana na nafasi ya kutosha kupitisha idadi kubwa ya magari bila kusababisha usumbufu miongoni mwa watumiaji wa barabara hiyo
Hata hivyo kuna hii kero ya alama za speed limit za 50kph kila baada ya hatua kadhaa! Pamoja na kuwepo vibao vingi kuonyesha 50kph hakuna vibao vya kuonyesha ukomo wa katazo hilo au viko kwenye maeneo machache sana!
Bahati mbaya, askari wa usalama barabarani wanatumia vibao husika kutoza faini madereva wanaokiuka speed limit au kuchukua ya "ku brash viatu"
Swali langu ni kwamba kwenye highway kama ile ni sahihi kuwa na vibao kama vile kila baada ya kilometer moja au pengine chini ya hapo?
Dereva anapoona kibao ya 50kph atajuaje kwamba ameshafika mwisho wa katazo? Tena unaeza kuta unamaliza kibao kimoja cha 50 unakutana kingine cha 50kph!!!
Inawezekana barabara haijakabidhiwa kwa serikali kwa maana bado ipo kwenye matengenezo, sasa ni sawa kwa askari kukusanya "tozo"?
Kama ni sawa kwanini kwenye zile rush hours huwa wanahimiza madereva wakimbize magari bila kujali alama hizo ili kuepeusha foleni?
Mambo haya ndio yanafanya wananchi waamini maneno ya uvumi wa SIRI ILIYO WAZI kwamba askari wa usalama barabarani wanageuza madereva kua mtaji wao