mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Ndugu wanaJF,
Juzi katika kipindi cha mada moto cha chanel ten kulikuwa na mjadala mkali sana kati ya Sabri, mwenyekiti wa DARCOBOA ambao sasa wameingia ubia kuiendesha UDART, na wawakilishi wa wengine wa wamiliki wa daladala Dar.
Licha ya wamiliki wa daladala kulalamika kwamba hawajalipwa fidia km walivyokubaliana ili waweze kuondoa daladala zao ktk route yanakopita mabasi ya DART, walilalamika pia kuwa suala la waalimu kusafiri bure hawakushirikishwa wala hawakukubaliana hivyo km ilivyodaiwa na Mkuu wa Mkoa, ndugu Makonda.
Walisema kwamba ni watu wachache walikaa akiwemo Sabri, ambaye wanamlaumu kwa kuwa na kimbelembele cha kuwasemea wengine, ghafla wakasikia mkuu wa mkoa by then wa wilaya akitangaza eti wamiliki wote wa daladala wamekubali kuwasafirisha waalimu bure!
Waliendelea kusema kwamba ilibidi wanysmaze tu kimya ili kumfichia mkuu Makonda aibu. Lakini kamwe hawakukubaliana.
Wamemshambuli vikali Sabri kwa kusimama upande wa serikali huku akishindwa kusimamia interests za wamiliki wa daladala Dar.
Chanzo: Chanel 10, kipindi cha Mada Moto cha Jumatano, tarehe 18.05.2016.
My take: Hili la viongozi kutafuta sifa za kisiasa kwa kufanya maamuzi bila kuwashirikisha kikamilifu wahusika haiwezi kuwa na matokeo chanya na endelevu! Ndugu Makonda una la kujifunza hapa!