Alaa….. Kumbe ccm haipo kwa ajili ya zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alaa….. Kumbe ccm haipo kwa ajili ya zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Oct 15, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  [h=1]ALAA….. KUMBE CCM HAIPO KWA AJILI YA ZANZIBAR?[/h][​IMG]
  Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nikithubutu kujinasibu na kujivunia sana mulhaka nilionao na chama changu mama ‘Efuru’ (Afro Shirazi).Kwamba kilikuwa chama ambacho kilitulea na kilimlea kula Mzanzibari na bila shaka kilikuwa chama cha kizanzibari kwa ajili ya wazaznibari na Zanzibar yake. Kwa hayo machache yatosha kwangu kukikubali chama hicho na kukipa voti yangu.
  Mwaka 1977, vilipounganishwa vyama, niliona makengeza kidogo. Nikaona baba (ASP) anapunganishwa na baba mwenziwe wa upande wa pili (TANU), na huku nikitambuwa kuwa mafahali wawili hawakai zizi moja, nilipata bishara kwa mbali ya kupotea kwa muelekreo wa Zanzibar.
  Tukaletewa CCM, tukawamo, makobe na kasa. Kilichotokea kwa Zanzibar baada ya kuunganisha vyama hakna haja ya kuandikwa tena hapa hata kwa sentensi moja. Mambo yote hadharani. Ila kwa ufupi tu nitie kaditama ya mukaddimati wangu wa tahariri hii kwa kusema kuwa Efuru iliondoka na mashina yake na kuiacha Zanzibar pakavu.
  Porojo yotte hii unafikiri imekuja kwa kitu gani? Hewalaaaaa! Nikiwa kwa sasa si muumini wa CCM wala CUF kwa sababu zangu za kwamba naamini kwamba vyama vyote hivyo aidha havina uwezo au hata nia ya kuisaidia Zanzibar na watu wake. Si CUF wala si CCM kwa sasa labda halafu.
  Lengo langu si kuijadili CUF kwani kwa ukweli ni chama ambacho hakina hatamu ya uongozi na maamuzi makubwa ya nchi hii kwa sasa japo kuwa kwa upande mmoja ni sehemu ya Serikali kwa huku Zanzibar. Lengo langu hasa ni kuupambanua wahaka na mshangao ulionipata kuoona kuwa chama ambacho nimekitegemea sana, CCM, kuwa hakina nia wala malengo ya kuikwamua na kuitetea Zanzibar katika Muungano.
  Nafahamu kuwa lengo la CUF si kuvunja Muungano. Pia mimi si muumini wa kuuvunja muungano bali ni muumini mkubwa wa kupambana na uonevu na unyonyaji unaofanya na muungano dhidi ya Zanzibar kama vile walivyo uamsho kwa sasa. Mimi na wenzangu hautuhitaji kuvunja muungano lakini kwa nguvu moja tunataka chama cha CCM Zanzibar kishikamane na CUF na UAMSHO kwa kuitetea Zanzibar tu. Kwani vyombo vyote hivyo vitatu ni watoto wa mama mmoja, Zanzibar.
  Kinachonishangaza leo hii na kuona na kuamini kuwa CCM haina lengo kuitetea Zanzibar badala yake ni kuinakamaisha zaidi na kusaidia kuifuta katika ramani ya dunia, ni pale tunaposikia kuwa wana CCM wote wanapinga muungano ‘wakatwe vichwa’ sio angalau kuvuliwa magamba tu.
  Taarifa kutoka makao makuu ya CCM Zanzibar yathibitisha wazi kuwa viongozi kadhaa wa juu wa CCM watavuliwa vyeo na dhamana walizonazo hata wakiachwa na kadi watabaki kama mafuvu au mabupuru yasiyo kitu wala heshima katika chama ili kuwakomoa. Hali kama hii ilimfika mzee wetu Aboud Jumbe, ambae haonekani wala hasikiki katika CCM pamoja na kuwa alifanya mengi ya kuunufaisha huo Muungano na kuikandamiza Zanzibar. Mchawi hana huruma, imani wala ihsani.
  Kuna taarifa za kuaminika hapo jumba letu kubwa Kiswanduni kuwa Mh. Amani Karume atadamirishwa kwa kila hali muda si mrefu. Wengine ni Mansour Yussuf Himid, Mzee Moyo, na kambi yote ya Amani Karume iliyoshadidia mardhiano na inayounga mkono ukombozi na utetezi wa haki za Zanzibar ndani ya Muungano. Kama hayo hayajafanyika basi bado masaa na dakika tu.
  Lakini iwapo haya yatatekelezwa na kuwaondoa viongozi hao na mtandao wao katika chama kwa sababu tu wamedai haki za Zanzibar katika Muungano ambao kwa sasa kila mwananchi wa hapa Zanzibar , awe anautaka au hautaki, anauona kuwa hauna manufaa ya kweli kwa Zanzibar, hasa ukichukulia kuwa Muungano wenyewe umebadili sura ya umoja na kuwa ukoloni wa ndani.
  Iwapo viongozi wetu hao wa CCM watakatwa vichwa, taswira inayojengwa na CCM kwa wananchi ni ipi? Na kasha ifikapo wakati wa kampeni CCM itawaambia vipi wananchi ambao kwa sasa wanaamini umasikini walionao ni matokeo ya unyonyaji inaofanyiwa Zanzibar na Muungano? Hivi CCM haijui kuwa kufanya hivyo itakuwa inajikashifu?
  Naamini yawezekana haya yasiwakere ya wapi watpata kura za kuitawala tena Zanzibar kwani njia ya kupitia kwenda ikulu ina tundu nyingi kwao wao na ina njia moja tu kwa wapinzani wao CUF.CCM na ikulu damu damu, ikichaguliwa isichaguliwe itaingia lakini pia itazame na kusoma alama za nyakati. Kuna siku wananchi wakibaini kuwa CCM inatumika kama kibaraka wa MUUNGANO wa kuinyonya na kuikandamiza Zanzibar basi patakuwa hapatoshi. CCM hala hala ujiti na macho, na ncha ina hoho!

  From ALAA
   
Loading...