Al-Shaabab yatishia kuishambulia Kenya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Al-Shabaab imetishia katika video mpya kwa kusema "wataianza safari" na kuongeza mashambulizi yake nchini Kenya ili kulipiza kisasi uwepo wa jeshi la nchi hiyo nchini Somalia, ambako kundi hilo lina makao yake.

Dürre Hungersnot Afrika Flash-Galerie

Kitengo cha habari cha al-Shabaab kimesema kwenye video hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya Rocket Chat na Telegram,

"Tunatuma salamu kwa Kenya, nchi ya makafiri. Tumefunga safari ambayo haina kurudi nyuma. Kwa makafiri, hizi ni nyakati za mwisho."

Chombo cha habari kinachohusishwa na kundi hilo kimedai hivi majuzi kwamba wanamgambo hao walizidisha mashambulizi yao nchini Kenya katika wiki za hivi karibuni kuelekea mwaka mpya.

Tangu Januari 3 mwaka huu, takriban watu 13 wameuawa katika mashambulizi yanayoshukiwa kutendwa na al-Shabab katika mikoa ya pwani ya Kenya iliyo jirani na Somalia. Al-Shabaab imekuwa ikifanya mashambulizi nchini Kenya tangu mwaka 2011, wakati wanajeshi wa nchi hiyo walipovuka mpaka na kuingia Somalia kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Al-Shabaab wanadaiwa kuhusika na mauaji ya raia kaunti ya Lamu

Ijumaa iliyopita, maafisa wanne wa polisi walishambuliwa na kuuawa katika eneo la pwani ya Kenya linalopakana na Somalia ambalo huwa rahisi kuvamiwa na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Shambulizi hilo lilitokea katika Kaunti ya Lamu, ambapo serikali ilituma vikosi vya usalama na kutangaza amri ya kutotoka nje kuanzia jioni hadi alfajiri baada ya mauaji ya raia saba katika msururu wa uvamizi.

Mapema wiki iliyopita polisi nchini Kenya walishuku kuwa wapiganaji wa Al-Shabaab walihusika na mauaji ya raia saba huko Lamu.

Mtu mmoja alikatwa kichwa na wengine kupigwa risasi au kuchomwa moto hadi kufa katika mashambulio mawili ya Jumapili na Jumatatu. Lakini polisi baadaye walisema ghasia hizo zilihusishwa na mzozo wa ardhi katika eneo hilo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya ilitangaza Jumatano iliyopita kuwa baadhi ya sehemu za kaunti ya Lamu ni "maeneo yenye misukosuko" na kusema timuya usalama itakayowajumuisha mawakala mbalimbali itafanya msako wa kutafuta silaha katika eneo hilo.

Chanzo: DW Swahili
 
Kenya waondoe jeshi huko Somalia. Wawaache hawa wajinga waendelee kuumizana.

Maana uwepo wa jeshi lao huko inasababisha wananchi wasio na hatia waendelee kufa.
They are just mouthing😬hao alshabaab mafala wa somalia,ata Kenya ikiondoa jeshi yao huko Somalia bado hao macoward watavamia Kenya tuu!

If they are real men let them dare confront us face to face!

Iko siku hio ufala itafanya KDF ikasirike iteke Somalia!

Ama hao somalia wanathani we too dont know to fight,there is a time we kenya people will take arms wajilinde tuone alshaabab atatokea wapi, mbona hawavamiagi maasai land,coward sana hao,they fear armed people thats why wanavamia raia watulivu! Just total cowardice!
 
They are just mouthinghao alshabaab mafala wa somalia,ata Kenya ikiondoa jeshi yao huko Somalia bado hao macoward watavamia Kenya tuu!
If they are real men let them dare confront us face to face!
Iko siku hio ufala itafanya KDF ikasirike iteke Somalia!
Ama hao somalia wanathani we too dont know to fight,there is a time we kenya people will take arms wajilinde tuone alshaabab atatokea wapi,mbona hawavamiagi maasai land,coward sana hao,they fear armed people thats why wanavamia raia watulivu!just total cowardice!
Ndani ya miaka 11 tangu Kenya kuivamia Somalia, wakenya wengi wasio na hatia wameuliwa, kumbuka hata USA wametoka Afghanistan, sio lazima kushupaza shingo wakati mnaumia.
 
They are just mouthing😬hao alshabaab mafala wa somalia,ata Kenya ikiondoa jeshi yao huko Somalia bado hao macoward watavamia Kenya tuu!

If they are real men let them dare confront us face to face!

Iko siku hio ufala itafanya KDF ikasirike iteke Somalia!

Ama hao somalia wanathani we too dont know to fight,there is a time we kenya people will take arms wajilinde tuone alshaabab atatokea wapi,mbona hawavamiagi maasai land,coward sana hao,they fear armed people thats why wanavamia raia watulivu!just total cowardice!
To please the full, just say yes. Kenyans are still suffering from these stupid cowards. Let them kill each other wabaki na ujinga wao
 
Ndani ya miaka 11 tangu Kenya kuivamia Somalia, wakenya wengi wasio na hatia wameuliwa, kumbuka hata USA wametoka Afghanistan, sio lazima kushupaza shingo wakati mnaumia.
Actually its true KDF inafaa iondoke tu, no matter how they try hard, they dont want peace, how I wish kutokee maji itayogawanisha Border ya Kenya na Somalia, ni jirani bure kabisa!
 
actually its true KDF inafaa iondoke tuu,no matter how they try hard,they dont want peace,how i wish kutokee maji itayogawanisha Border ya Kenya na Somalia,ni jirani bure kabisa!
Sio sawa kulaumu Somalia kwa kuwa jirani wa hovyo, Kenya inastahili kulaumuwa kwa kuchukua maamuzi ya kipuuzi kuivamia Somalia bila kufanya utafiti wa kutosha, kwa ujumla hapakua na sababu zozote za msingi kwa KDF kuingia Somalia, Kenya mlipaswa kuweka KDF katika mpaka wa Kenya na Somalia kuhakikisha Alshabab wanadhibitiwa wasiingie Kenya.
 
They are just mouthing😬hao alshabaab mafala wa somalia,ata Kenya ikiondoa jeshi yao huko Somalia bado hao macoward watavamia Kenya tuu!

If they are real men let them dare confront us face to face!

Iko siku hio ufala itafanya KDF ikasirike iteke Somalia!

Ama hao somalia wanathani we too dont know to fight,there is a time we kenya people will take arms wajilinde tuone alshaabab atatokea wapi,mbona hawavamiagi maasai land,coward sana hao,they fear armed people thats why wanavamia raia watulivu!just total cowardice!
Naona unajitekenya na kingereza uchwara mzee,hao alshabaab hamtawaweza maana hata mataifa makubwa tena yenye nguvu na technolojia waliwashindwa sembuse hao KDF wenu wezi wa supermarket.
 
kama hawababaishwi na hawaezekani🙈basi mbona wanalia waondolewe KDF huko Somalia,terrorist are cowards!
 
Naona unajitekenya na kingereza uchwara mzee,hao alshabaab hamtawaweza maana hata mataifa makubwa tena yenye nguvu na technolojia waliwashindwa sembuse hao KDF wenu wezi wa supermarket.
alafu hii ufala yao ya kujificha na kulipua"cat and mouse game"ndio unaona ni brave kwako?pia sisi huku Kenya tunao magaidi na hawaulizagi majirani!Ama unathani wangegeuka terrorists kama kuna mtu angewezana nao?
Kutatiza raia wakawaida ni tendo bure kabisa!!!
 
Wakenya mnachekesha sana, yaani mnategemea alshabab watoke mpambane face to face mtasubiri hadi yesu arudi.

Mfupa umemshinda mmarekani kdf mtaweza, kuliko kuendelea kuumia bure bora mrudi nyuma muokoe maisha ya wakenya wasiokuwa na hatia
 
Sio sawa kulaumu Somalia kwa kuwa jirani wa hovyo, Kenya inastahili kulaumuwa kwa kuchukua maamuzi ya kipuuzi kuivamia Somalia bila kufanya utafiti wa kutosha, kwa ujumla hapakua na sababu zozote za msingi kwa KDF kuingia Somalia, Kenya mlipaswa kuweka KDF katika mpaka wa Kenya na Somalia kuhakikisha Alshabab wanadhibitiwa wasiingie Kenya.
Hayakuwa matakwa yao bali walisukumwa na waamerica na magharib

Sent from my TECNO BC2c using JamiiForums mobile app
 
mashabibi wazee wa makobazz hawana jipyaa..kazi kujilipua lipua tu ovyo hovyoo...tunafagia tunaendelea na kazi mazeee!!. ..nipo tarakea waswahilii ss hivii naenjoy na totooz..tz hoyee
 
Al-Shabaab imetishia katika video mpya kwa kusema "wataianza safari" na kuongeza mashambulizi yake nchini Kenya ili kulipiza kisasi uwepo wa jeshi la nchi hiyo nchini Somalia, ambako kundi hilo lina makao yake.

Dürre Hungersnot Afrika Flash-Galerie

Kitengo cha habari cha al-Shabaab kimesema kwenye video hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya Rocket Chat na Telegram,

"Tunatuma salamu kwa Kenya, nchi ya makafiri. Tumefunga safari ambayo haina kurudi nyuma. Kwa makafiri, hizi ni nyakati za mwisho."

Chombo cha habari kinachohusishwa na kundi hilo kimedai hivi majuzi kwamba wanamgambo hao walizidisha mashambulizi yao nchini Kenya katika wiki za hivi karibuni kuelekea mwaka mpya.

Tangu Januari 3 mwaka huu, takriban watu 13 wameuawa katika mashambulizi yanayoshukiwa kutendwa na al-Shabab katika mikoa ya pwani ya Kenya iliyo jirani na Somalia. Al-Shabaab imekuwa ikifanya mashambulizi nchini Kenya tangu mwaka 2011, wakati wanajeshi wa nchi hiyo walipovuka mpaka na kuingia Somalia kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Al-Shabaab wanadaiwa kuhusika na mauaji ya raia kaunti ya Lamu

Ijumaa iliyopita, maafisa wanne wa polisi walishambuliwa na kuuawa katika eneo la pwani ya Kenya linalopakana na Somalia ambalo huwa rahisi kuvamiwa na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Shambulizi hilo lilitokea katika Kaunti ya Lamu, ambapo serikali ilituma vikosi vya usalama na kutangaza amri ya kutotoka nje kuanzia jioni hadi alfajiri baada ya mauaji ya raia saba katika msururu wa uvamizi.

Mapema wiki iliyopita polisi nchini Kenya walishuku kuwa wapiganaji wa Al-Shabaab walihusika na mauaji ya raia saba huko Lamu.

Mtu mmoja alikatwa kichwa na wengine kupigwa risasi au kuchomwa moto hadi kufa katika mashambulio mawili ya Jumapili na Jumatatu. Lakini polisi baadaye walisema ghasia hizo zilihusishwa na mzozo wa ardhi katika eneo hilo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya ilitangaza Jumatano iliyopita kuwa baadhi ya sehemu za kaunti ya Lamu ni "maeneo yenye misukosuko" na kusema timuya usalama itakayowajumuisha mawakala mbalimbali itafanya msako wa kutafuta silaha katika eneo hilo.

DW Swahili

Kwa hii kasi yenu ya kupigia alshabaab promo, muwe pia mnaleta habari kama hivi hapa ambapo Alshabaab wameuawa kumi na tano kwa mpigo Police Kill 15 Suspected Al Shabaab Terrorists
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom