Al-qaeda waanza kulipiza kisasi waua watu 80 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Al-qaeda waanza kulipiza kisasi waua watu 80

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mjunguonline, May 15, 2011.

 1. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ISLAMABAD, Pakistani WATU 80 wakiwamo wanajeshi 65 , wameuawa na wengine 117 kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili ya mabomu iliyotekelezwa na washirika wa mitandao ya kigaidi wa Al-Qaeda, Taliban. *


  Habari zimeeleza kuwa milipuko hiyo ya kujitoa muhanga iliyotokea kwa nyakati tofauti, pia iliharibu magari, nyumba na maduka kadhaa Pakistani.


  Mara baada ya milipuko hiyo Msemaji wa Taliban, Ehsanullah Ehsan alitoa taarifa akisema: " Hiki kisasi cha kwanza. Ni kama rasharasha tu, baadaye itakuwa zaidi ya hapa* kwa sababu kiongozi wetu ameshauawa tutaendelea kulipiza kisasi."


  Jumatatu ya Mei 2 huu, makachero wa Marekani walivamia makazi ya aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al- Qaeda, Osama bin Laden yaliyoko mjini Abbobatab* na kumuua.


  Polisi wa
  Pakistani wamethibitisha tukio hilo la kwanza tangu kifo cha bin Laden na kueleza kuwa moja lilitokea kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Shabqadar, Wilaya ya Charsadda na kuua wanajeshi 65. Walisema walipuaji wawili wa mabomu hayo, nao walifariki dunia papo hapo.


  "Kulikuwa na 0milipuko miwili ya mabomu," Ofisa Mkuu wa Polisi Shabqadar, Jahanzeb Khan aliliambia Shirika la Habari la AFP. Taarifa zilisema kwamba shambulio hilo lilitokea wakati wanajeshi wapya walipokuwa wanaingia kwenyemabasi kwa ajili ya kwenda likizo fupi baada ya mafunzo.


  Msemaji wa Polisi* wa Pakistani, Nisar Khan Marwat alisema mauaji hayo yalifanyika katika eneo la jeshi huko Shabqadar, karibu maili 19 Kaskazini Magharibi mwa Mji wa Peshawar na kuthibitisha kuwa yalikuwa ya kulipiza kisasi cha mauaji ya bin Laden.

  Alisema jumla ya watu waliofariki ni 80 na miongoni mwao ni wanajeshi. Watu wengine 30 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu ingawa hali zao si nzuri.


  Alisema mabomu hayo yaliyotumika kulipua eneo hilo na kusababisha madhara kwa jeshi na wananchi wa Pakistani, yalikuwa na uzito wa kilo
  10.


  Alisema mbali ya kuuawa kwa wanajeshi hao, zaidi ya magari 12 na maduka 20 yalilipuliwa na kuharibiwa vibaya. Mmoja wa mawaziri waandamizi wa Pakistani, Bashir Bilor alithibitisha vifo hivyo na kusema watu 80 wameshathibitishwa kufariki dunia lakini idadi inaweza kuongezeka.


  Alisema wakati tukio hilo linatokea hakuna aliyekuwa amejiandaa kwa mapambano ndiyo maana idadi ya watu waliofariki ikawa kubwa ndani ya jeshi.


  Hili ni shambulio la pili kuua watu wengi baada ya watu 4 ,300 kufariki dunia katika tukio la mabomu ya kujitoa muhanga yaliyotokea nchini humo mwaka 2007 katika Msikiti wa Islamabad.
   
 2. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,405
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  hawa nao wapumbavu, OSAMA ameuliwa na WAMAREKANI vipi mnaua ndg zenu na kumuacha muuaji..?
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  duh,...lots to come with same like thz
   
 4. T

  Tabby JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,871
  Likes Received: 5,466
  Trophy Points: 280
  Kwa wanaodai tukio la Osama limeamsha hasira za waislam, hii ndiyo image ya uislam? Kuwauwa wa Pakistan wenzao tena wanajeshi waliokuwa wanaishi na osama bila kumbugudhi eti kwa kulipa kisasi kwa America, ndio uislam? Hawa waliouliwa siyo waislam? Wanahatia gani katika suala zima la mauaji ya osama? Naomba muislam anijibu tafadhali ili tuende pamoja
   
Loading...