Ukiwa Mzanzibari moja kwa moja wewe ni Mtanzania. Lakini unaweza kuwa Mtanzania pasipo kuwa wewe ni Mzanzibari. Uraia una ncha nyingi , na ya muhimu ni nile ya kuwa raia wa kuzaliwa, na kutoukana uraiawako wa kuzaliwa.
duh haya yote tumeshayasema mkuu.. anaitwa Brig. Gen. Suleiman Yahya Mohammed Al-Adawi.. alizaliwa miaka ya hamsini na kuondoka Zanzibar miaka michache kabla ya mapinduzi ya Zanzibar.. familia yake ina nyumba Dar na Zanzibar (ana ndugu zake wengi tu na wana biashara kadhaa). Ana ukaribu wa mahusiano na Rostam na watawala wa Zanzibar.. pia vyanzo vya intelligencia vinadokeza kuwa ana mahusiano ya karibu na watu wa CUF hususan mmoja wa viongozi wakuu wa CUF..
Ni kweli alikuwapo Zanzibar kiasi cha wiki tatu zilizopita kwa hakika. Rostam alikwenda huko kuonana naye kama kawaida yao. Al Adawi ambaye alikuwa ADC wa Mfalme wa Oman, ni mtu muhimu sana kwa siasa za TAnzania. Ana majumba mawili ya kifahari katika beach za East eneo la Bwejuu na West Coast eneo la MAzizini. Mazizini aliuziwa kwa bei ya bure na Dk; Salmin Amour nyumba ya serikali na aliibomoa na kujenga kasri. Ahsante Gembe kutuzindua, tunamrafuta.