Al Ahly yatwaa ubingwa wa CAF Champions league

DreezyD98

JF-Expert Member
Nov 6, 2020
1,503
2,662
Timu ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa taji la CAF Champions league baada ya kuifunga Zamalek magoli mawili kwa moja.

Ahly walipata magoli yao kupitia kwa Al sulaya 5" na Kafsha 86". Goli pekee la Zamalek liliwekwa wavuni na Shikabala 31".

Ahly wanachukua ubingwa wao wa 9.

Pitso anaweka historia ya kuchukua kombe akiwa na timu mbili tofauti.
 
Mpira magoli jamani kha maana zamaleki wameupapasa mpira hatari.

Alafu bongo kweli tunarukaruka yule ali maaloul alikuwa anapanda wee na kuoverlap dhidi ya tz atakavyo leo hii namtafuta simuoni kabisa
 
Jamaa pesa wanayo aisee. Acha watawale mpira wa Africa. Tuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwao; uwekezaji na namna ya kuongoza mifumo ya mpira.
 
Kujifunza tumejifunza kitambo tu...ila hatuna hela mkuu...makelele ndiyo halali yetu...wababe Africa watabaki walewale tu timu za uarabuni Tp Mazambe labda Mamelody kidogo...na hizo timu nyingine za south zikijielewa.
 
Naona Pitso anazidi kuwakamua tuu waaarabu pesa zao.

Kwanini "MO" asituletee hili jembe pale Msimbazi. 😀😀😀😀
 
Kujifunza tumejifunza kitambo tu...ila hatuna hela mkuu...makelele ndiyo halali yetu...wababe Africa watabaki walewale tu timu za uarabuni Tp Mazambe labda Mamelody kidogo...na hizo timu nyingine za south zikijielewa.
Sisi tuendelee kujiita pira ubwabwa na pira mihogo mpaka wakati tutakapoanza kuwa serious kwenye mpira.
 
Back
Top Bottom