Al Ahly wanastahili kucheza hata UEFA Champions League

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,877
3,617
Yes, no doubts

Nipo sebuleni kwangu naangalia mpira wa Al ahly vs Bayern Munich aiseee siamini kama kuna timu kutoka Africa inaweza cheza kwa kujituma katika level hiii. Timu za Tanzania zina safari kubwa ambayo itawachukua miongo kadhaaa kuwafikia hawa jamaaa.

Congratulations kwa league ya Misri, mpira ni pesa, mpira ni uwekezaji. Mpira sio press conference kila siku. Kufika level kunahitaji vision na sio ubabaishaji wa mitandaoni eti mnalinda brand. Huu ndio mpira sasa, hawa jamaa wanaweza cheza hata UEFA na kuna timu za kijinga jinga zinachezea goals za kutosha.

Ni hayo tu.
 
Hawa jamaa wakija kwa mkapa huwa hawakazi ila wakikaza kama hivi tutachezea mkono hapa hapa kwa mkapa.
 
Aisee Simba ni timu hasa,tena yenye mafanikio mpaka ndani ya mioyo ya Vidimbwi f.c.

Unaangalia mechi ya Al Ahly na Bayern ghafla ukapata hisia za Simba na kuanzisha uzi maalum kwa ajili ya kuijadili Simba kutokana na mechi ya Al Ahly na Bayern!?
 
Mpira ni pesa wewe wala siyo hiyo miongo unayosema. Unafikiri Psg imewachukua miongo au zimewekwa pesa ndio wakawafikia Marseille? Au Man city imewachukua miongo hapo walipo au ni pesa? Bila pesa hata ingekuwa karne hautafika pale walipo kwa maana ya kusakata kabumbu.

Halafu unapoikejeli timu moja tena inayojitahidi unaonekana shabiki maandazi. Hivi kati ya mambo ya brand , press conference na timu nyingine kutokuwa na uwanja hata wa mazoezi ipi inakwamisha kupiga hatua?

Au timu zingine zimekatazwa kufika mbali? Utopolo bhana!
 
timu hasa mbele ya nani? ruvu,yanga,azam ama maana hao tu wanaitoa jasho
Aisee Simba ni timu hasa,tena yenye mafanikio mpaka ndani ya mioyo ya Vidimbwi f.c.
Unaangalia mechi ya Al Ahly na Bayern ghafla ukapata hisia za Simba na kuanzisha uzi maalum kwa ajili ya kuijadili Simba kutokana na mechi ya Al Ahly na Bayern!
 
Uto kwa kujitafutia faraja hamjambo! Juzi mkatafuta timu ndogo mpate faraja ila mkakalia.

NB: Al Ahly ni timu bora zaidi Africa na hakuna timu yoyote ya kuishinda Ahly kwa hapa Africa ni hivyo tu mpira una maajabu wanaweza poteza ila wao ni bora zaidi Africa, tatizo uzi wako umejaa unazi wa Uto.
 
Back
Top Bottom