Akutwa na ngozi ya mtu huko Mbozi - Je tutafika na hali hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akutwa na ngozi ya mtu huko Mbozi - Je tutafika na hali hii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'azagala, Nov 16, 2008.

 1. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2008
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Akutwa na ngozi ya mtu
  na Kenneth Mwazembe, Mbozi

  MKAZI wa Kijiji cha Halungu, wilayani Mbozi, Yalesi Mganji, anashikiliwa na polisi mjini Vwawa kwa tuhuma za kuuza ngozi ya binadamu.

  Mganji, alikamatwa jana na kupelekwa kituo cha polisi alipokuwa akitafuta mnunuzi wa ngozi za binadamu.

  Mfanyabiashara Ringson Chaula ambaye aliwahi kufanikisha ukamataji wa wachuna ngozi 1998, alisema jana kuwa Mganji alikwenda ofisini jana alfajiri na kumtaka anunue ngozi ya binadamu.

  Chaula ambaye aliandaliwa kununua ngozi mwaka 1998 ikiwa ni mtego wa polisi, anahisiwa kufanya biashara hiyo, ndiyo maana alifuatwa na wauzaji wa ngozi hizo wakiamini atanunua.

  Baada ya kijana huyo kumweleza nia yake hiyo, alimchukua mtuhumiwa huyo akisaidiana na walinzi wake kumpeleka kituo cha polisi.

  “Watu hawa wanazidi kunichafua, juzi wanawake wawili walikuja kuniuzia mimba ili wakijifungua wanipe watoto, niliwakatalia, sasa leo wanataka kuniuzia ngozi ya binadamu,” alilalama Chaula.

  Hata hivyo, Mganji alipohojiwa alisema hayupo peke yake, kwani alitumwa na Damson Nkota, ili apatane bei na Chaula kisha waende wakamchune mtu waliyemuandaa.

  Mlinzi wa Chaula, aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Mwakitwange, alisema kijana huyo alifika ofisini hapo akidai anamtafuta Chaula, ili amuuzie mali.

  Polisi wamethibitisha kuwpao kwa tukio hilo na kusema kwamba taarifa zitatolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa ambaye alikuwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa.

  Vitendo vya uchunaji ngozi viliibuka wilayani hapa mwaka 1998 na kushika kasi, hali iliyowatisha watu wengi.

  hivi tunatarajia neema kwa kila mtanzania ikiwa kuna matendo ya kishirikina kama haya? mara mauaji ya Albino, mara vichanga nk. kwa watu waishio vijijini,(Africa) haya mambo ya kishirikina/giza ni kizingiti kikubwa sana cha maendeleo, watu bado wanafikiri kuna option kama hii ya kuleta maendeleo (bado tupo enzi gani sijui!) lazima kwakweli watu tushirikiane na serikali kupambana na ujinga huu kwa dhati
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Du hiyo kali, kuna nini huko Mbeya? Ajabu ni kuwa nasikia Mbeya ni mkoa wenye makanisa mengi kabisa Tanzania, na ni mkoa wenye matukio makubwa kabisa ya kutisha, wanaJF wa Mbeya mtueleze kidogo kulikoni huko.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bongolander,

  Unaulaumu mkoa wote kwa makosa ya wapumbavu wachache? Inatakiwa watu kama hao mkong'oto wa nguvu utembee. Hayo yote ni matokeo ya ujinga na siasa mbovu za kushindwa kuwaendeleza watu wetu.

  Miaka karibu 50 ya uhuru wetu, bado kuna watu wanafikiri watapata utajiri kwa kununua au kuuza ngozi za binadamu wenzao?

  Sikuwahi kutegemea miaka ya 2000+ kuwe na watu wanachunwa ngozi au Albino wanauawa. Hii ni matokeo ya ujinga kuongezeka badala ya kupungua.

  Badala ya maendeleo ya nchi nzima, sasa maendeleo yanazidi kubaki Dar tu huku wilayani watu wanazidi kuwa wajinga.

  Vijana nendeni kaelemisheni hizo wilaya zenu, watu waachane na ushirikina na ujinga kupita kiasi.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa CCM itatawala vipi kama italeta elimu za kufuta ujinga na kuwaelimisha watu kwamba kuna magari siku hizi yanaendea maji ?
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Jk na washikaji zake wanatania mpaka sasa hatusikii wale watuhumiwa wa mauaji uya albino ndio maana watu wanazidi unyama huu.BBC wameweza kuwafikia waganga na iam sure majina ya waganga wauaji wanayo iweje serikali ya msanii jk ishindwe? mpaka liwaguse.
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Allah awasaidie wamjue yeye tu ndiyo haya yote yataisha. Mali ya nini ikiwa tunaishi ili tufe? They want to evade the blood truth. The only thing in life we are all sure of is DEATH. Why sasa kill for money that you can not take it anywhere along the life cycle. Its a shame and curse upon those mentally handcapped to the extent that they kill others. Anyway those killed have been forced to the next level of the life cycle. No problem. BUT the curse is upon them. They will search for money to find it is no help at the very time. They do not know this!!!?
   
 7. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0


  Mkulu,
  Nashukuru kwa hii thread nilikua nataka kuanzia hapa pia,nitakuwekea picha sasa hivi ili uone kwamba hata hapa Dar es Salaam mambo kama hayo kama kazi.
  Nilikua nimetoka mahara fulani kupunga upepe ndio nikakutana na mauza uza hayo.

  Ngoja niweke alafu tujadiri,je tutafika?
   
 8. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wakulu ,this will take some time
   
 9. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  How long is some time Sanda Matuta. This is a forum of high precision and highest specificity. So do you?
   
 10. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  i am having difficulties uploading pics to this site.from my desktop,any help Mukulu!?
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  May be they must have been of high resolution and therefore what you can do is: either or in combination:
  1. Upload one by one or
  2. Download piccture resizer at http://bluefive.pair.com/PIXresizer.zip install on your computer and launch it to resize them to required jamiiforums.com server requirement
  3. Upload them somewhere else and put a link within your post relevant to the post and wording. e.g. servers that can store images and video of which offers great space. They are many; just GooGle them immediately

  If not of any help contact the moderator/admins right away for a serious help online.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unaona sasa haya mambo? Wametajwa Watu wa Mbeya. Hilo kweli tusi kwa mkoa mzima. Kuna watu wengine na dini zao au sehemu watokapo zingelikuwa zimetajwa basi ungelisikia "uombe msamaha..." Ataacha yote yaliyoandikwa na kushupalia kipointi kidogo tu au kitu ambacho hata si muhimu katika huo ujumbe. Nashukuru Mtanzania, pamoja na kuseme "usilaumu mkoa mzima", bado kaendelea na yeye kulaani kitendo hicho na hivyo kutoibadili hii habari. Hapa wangelikuwa wenyewe basi saa hizi ungelisikia "sisi Wamoravian wa Mbeya inabidi utuombe msamaha....."
  Naungana na mie kulaani huu ushamba. Inabidi kweli hawa watu waende jela na kupigwa viboko 30 kila mwezi kwa miaka sawa na umri wa mtu waliyemchuna ngozi ukitoa kwa 100. Akiwa mtoto ndivyo miaka inavyozidi kuwa 100.
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Wakulu vipi mbona mnajaribu kukwepa ukweli, kwamba hata viongozi wetu ni wachawi, hivi maamuzi mengi ya viongozi wetu kweli mnayaona kuwa yako sawa?

  Hivi hamuwezi kuona kua mengi yana dalili za kichawi chawi? Hili la uchawi sio la wananchi peke yao, hili ni la viongozi pia tena wa pande zote mbili, hivi mpaka tuseme ukweli wote tunaoujua hapa?

  Msionee wananchi wanaojaribu tu kuwaiga viongozi wao!
   
 14. M

  Mama JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  je unakubaliana na wanaosema Tanzania hakuna press.
   
 15. M

  Mama JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Pole, kwani wewe ni katika hao kina fulani? unawajua? tutajie basi tuwajue, usiogope. In JF you talk openly!

  Tanzania imeoza kwenye nini? press au kila kitu. Imeoza tu au imeoza na kunuka.
   
 16. M

  Mama JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Nimerudia kusoma lakini sijajua hasa nani wanazungumziwa zaidi ya wachuna ngozi. Na Mbeya huko kuna dini na makabila mengi.Ni kina nani hao ambao na wewe ni mmoja wao?

  Anyway, labda hutaji kwa sababu za kiusalama.
   
 17. M

  Mama JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Haya nyamaza, Mama amesikia, we mwache tu huyo. Okay?
   
 18. M

  Mama JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  na wewe naye, nilidhani umenyamaza kulia. Siko mashindanoni FYI. Kwa raha zangu acha niandike nitakacho! Sikuja kukualika siku niliporegister so ukome na wewe kuangalia nina posts ngapi. Mie mwenyewe sijui, we umejuaje kama si umbea?!
   
 19. M

  Mama JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Aww, kumbe wanihesabia matonge sio, sikuwa najua kuna watu wa aina yako hapa. Sikonge hakukosea,take five Sikonge ulimkuna kumoyo mwafulani. Anzisha thread kunijadili naona unanijua kuliko ninavyojijua.
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Vitu kadhaa vinanitatiza:
  1. Kuna Mkuu amesema tusiwaonee hawa wanafanya biashara ya ngozi kwa sababu wanaiga viongozi wao!
  2. Kwa vile watuhumiwa walikuwa wanatafuta dili kwanza kabla ya kwenda kumchuna mtu basi si waovu!

  Kweli tutafika hivi?
   
Loading...