"Akumulikaye Mchana Usiku atakuchoma Moto" Kwa hawa Mawaziri na Wakuu wetu wa Mikoa,Wilaya?

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
kwanza ni wazi kwa mwenye akili yeyote atakubali kuwa hawa wakuu wa mikoa na wilaya ni muendelezo wa vyeo vya kupeana kwa hisani na shukrani. na wakati mwingine zawadi kwa watu wetu mbalimbali. kama mimi ningekuwa rais hivi vyeo najijua udhaifu wangu .. ningewapa sana masulia wangu. wasinisumbue. so hapo sitamsikia akinambia hana pesa ya matumizi au nini.kwangu inakuwa kazi tu. maana "NIMEMPA ACHUME"

nachelea kusema kuwa tukija kupata "Rais Kichaa" atachagua viongozi ambao nao ni vichaa. nikakumbuka mamlaka waliyopewa hawa wakuu wa mikoa na wilaya . je si wakati wa wao kuonesha ukichaa wao? kisaikolojia kila mtu ni kichaa sema tu kichaa kinakuwa kimelala. kikisubiria kuamshwa.

nawaza kuwa ikitokea mkuu wa mkoa kichaa, mkuu wa wilaya kichaa...kichaa chake kikimpanda... ikawa anahutubia halafu mwananchi mmoja hajapiga makofi kumshangilia si inaweza kuwa "inshu" akaagiza awekwe ndani? au ikatokea mkuu wa wilaya mzuka ,munkari ukampanda ikawa katika kuhutubia mwananchi mmoja akauliza swali la kuudhi... akaamsha kichaa cha ndugu mkuu wa mkoa/wilaya si atawekwa ndani au kudhuriwa vibaya sana?kuna wakuu wa mkoa itafikia mahali ukimtizama tu kwa jicho kali ataamuru "muwekeni ndani huyu maana amenitizama kwa jicho la kudhuru" unasukumwa ndani.na watoto wakija wanasukumwa ndani,na ndugu zako wanasukumwa ndani...mnasukumwa ndani tu...

nimewaza tu kutokana na kauli za mihemko na vitisho wanazoweza kuwa wanatoa wakuu wa mikoa na wilaya flani flani wakijinasibu wao ni watu hatari, wakuogopwa.. wengine wakijimilikisha na kusema 'watu wangu" n.k hizi ni sawa na kauli za mtu anayekumulika mchana. mtu anayekumulika kwa kijinga cha moto mchana unadhani usiku atakufanyaje? atakuchoma moto bila woga wowote.maana kipindi hicho hakuna wa kumwona akitenda ukatili huo.

kama atatokea Rais Kichaa (Mungu apishilie mbali jambo hili) Rais ambaye atakosa busara, atachukia kukosolewa. atataka awe zaidi ya Mungu ( maana Mungu pamoja na nguvu zake zoote na uwezo wake anaruhusu hata watu wamkashifu... imagine ingekuwa ukimkashifu anakubana mbavu, anakunyima pumzi kwa muda...ingekuwa "inshu" " ) tukipata Rais "kichaa" atachagua viongozi vichaa, hawa watatenda kwa ukichaa zaidi ya Rais aliyewachagua waswahili husema "wapambe nuksi" lakini haya yanatokana na muongzo toka kwa baba yao maana "ukiona zinduna, na ambali ipo nyuma"

haya yanaweza nenwa hadharani.. inapokuwa kifichoni ndipo miaka hiyo kwa kutumia viongozi hawa vichaa utasikia mtu kapotea, kashambuliwa n.k. waswahili hawakukosea waliposema "akumulikaye mchana, usiku atakuchoma moto" nawaza tu ikiwa wanaitendea hivi miti mibichi.itakuaje kwa miti mikavu?

wabillah tawfiq.
 
huu si muda sahihi wa kudill na siasa za bongo

usishangae siku moja kumkuta Mbowe yuko na kijana mzee POLEPOLE akitangaza kuunga juhudi

wanasiasa ndo walokokewa moto wa jahanamu
 
nimejaribu kusoma thread hii sijaona kabisa nlipotaja chadema. sijajua wewe hili wazo umetoka nalo wapi. mbona nimeandika kwa kiswahili chepesi kabisa?

Gudume kwani humjui huyo dada, akiwa kwenye 'joto' anawaza hata vitu visivyopo duniani anahama sayari nyingine mpaka apate wa kutuliza mzuka wake, hapo kakuotea sasa kazi kwako.
 
Kweli tuombe sana asije akatokea Rahis kichaa halafu awe jiwe itatugharimu, Mungu epushia mbali
 
maendeleo gani wewe kiwavi jeshi unaongelea??

Tangu kichaa awe rais kuna maendeleo gani wananch wanayo kuna unafuu gani wewe wakala wa ibilisi??
Tatizo lako umegubikwa na unyumbu huwezi kuona chochote.
Ukiachana na kuzungusha mikono na kudeki barabara utaona mengi
 
Chadema kimegeuka kuwa chama cha kupinga maendeleo ya wananchi
Certified Idiot
Jadili big Ideas kutoka kwenye thread Usilete mihemko na mipasho

Jifunze kutafakari kabla ya kureply

Endelea kutumia Title ya Certified Idiot kwani umeisotea miaka mingi tangu sekondari
 
GuDume nimekuelewa...upo smart sana aisee....sijui chuki niliyonayo juu ya hawa mapunga wa ccm itatokaje...qumamaye zao...hv wahehe mbn tunaangushana jaman?huyo mwenye jina la kike si mmpe ht kichomi kikali cha mwezi tu!walah atakuwa mweusi..inauma sanasana jaman..cha kuumiza watu tupo kimyaaaa
 
Certified Idiot
Jadili big Ideas kutoka kwenye thread Usilete mihemko na mipasho

Jifunze kutafakari kabla ya kureply

Endelea kutumia Title ya Certified Idiot kwani umeisotea miaka mingi tangu sekondari

Anapata wapi muda wa kufakari wakati muda wake wote anatafuta watu wa kushusha kigololi chake?
 
Back
Top Bottom