Akufaaye kwa dhiki ndio rafiki. Marekani Imewekeza Trilioni 11, Urusi Imewekeza nini Tanzania?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,992
49,655
Kuna baadhi ya Nchi tunaweka nazo urafiki ila hazina maana Wala Msaada Kwa Tanzania.

Nchi kama Russia/Urusi kuwa nayo urafiki ni hasara kuliko faida..

Marekani Imewekeza Takribani Tilioni 11 ndani ya Tanzania na Mingi ya hiyo miradi ni yenye faida Kwa Tanzania..

Sasa wale pro Russia waje watuambie Kuna faida ipi ya Tanzania kuwa rafiki na Nchi kama Russia ambayo Haina Msaada wowote Kwa Tanzania? Russia kawekeza nini hapa Tanzania? Bora hata Iran Huwa wanatukopesha pesa na pia wanatoa scholarship Kwa watu Wetu na mafunzo ya kijeshi..

Nikiwa Kiongozi lazima nichukue mkondo wa kuwa bega Kwa bega na Marekani na sio hoa wengine.
===
Uwekezaji wa TZS trilioni 10.97 wa Marekani nchini Tanzania umesaidia zaidi ya Watanzania 50,000 kupata ajira za moja kwa moja. Habari hii njema imekuja siku chache kabla ya ziara ya Kamala Harris nchini Tanzania.

Uwekezaji huu umelenga katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati, madini, miundombinu, utalii na kilimo. Kupitia uwekezaji huu, Tanzania imepata fursa ya kuimarisha uchumi wake na kujenga uhusiano mzuri na Marekani.

Kwa upande wake, ziara ya Kamala Harris inatarajiwa kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Marekani na Tanzania na kufungua zaidi fursa za biashara na uwekezaji. Kupitia ziara yake, Kamala Harris atakutana na viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wadau wengine ili kujadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.

Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji na biashara, na ziara ya Kamala Harris inaonesha nia njema ya Marekani katika kuimarisha ushirikiano huu. Ni matumaini yetu kuwa ziara hii italeta mafanikio makubwa kwa pande zote mbili na kuchochea zaidi ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Tanzania..

Kuna baadhi ya Nchi tunaweka nazo urafiki ila hazina maana Wala Msaada Kwa Tanzania.

Nchi kama Russia/Urusi kuwa nayo urafiki ni hasara kuliko faida..

Marekani Imewekeza Takribani Tilioni 11 ndani ya Tanzania na Mingi ya hiyo miradi ni yenye faida Kwa Tanzania..

Sasa wale pro Russia waje watuambie Kuna faida ipi ya Tanzania kuwa rafiki na Nchi kama Russia ambayo Haina Msaada wowote Kwa Tanzania? Russia kawekeza nini hapa Tanzania? Bora hata Iran Huwa wanatukopesha pesa na pia wanatoa scholarship Kwa watu Wetu na mafunzo ya kijeshi..

Nikiwa Kiongozi lazima nichukue mkondo wa kuwa bega Kwa bega na Marekani na sio hoa wengine..

Kwanza lazima uone hao wamarekani wamewekeza wapi na hao warusi wameweza wapi, unaweza kuta unaowaona wa maana wamewekeza kwenye mambo yale ya bendera ya rangi nyingi, wakati usiowakubali wamewekeza kwenye ulinzi wa taifa lako na hata ulinzi wa raia wewe unayetegemea sirikali kuhakikishiwa ulinzi wako na mali zako🤔
 
Kwanza lazima uone hao wamarekani wamewekeza wapi na hao warusi wameweza wapi,una weza kuta unaowaona wa maana wamewekeza kwenye mambo yale ya bendera ya rangi nyingi,wakati usiowakubali wamewekeza kwenye ulinzi wa taifa lako na hata ulinzi wa rais wewe unategemea sirikali kuhakikishiwa ulinzi wako na malizako🤔
Nina uwezo wa kukutajia wamarekani walichowekeza na pia walichotoa kama Msaada.

Vya Urusi sijawahi ona hata kimoja zaidi ya kuwachukua watu Wetu na kuwatumikisha kwenye vita huko Ukraine
 
Nina uwezo wa kukutajia wamarekan walichowekeza na pia walichotoa kama Msaada.

Vya Urusi sijawahi ona hata kimoja zaidi ya kuwachukua watu Wetu na kuwatumikisha kwenye vita huko Ukraine
Nikuambie tu,katika taifa ovu zaidi duniani,hilo linaongoza,unaa mwingi,wivu kwa washindani,na hata kwa wale tunaopambana kujikwamua😂
 
Nina uwezo wa kukutajia wamarekan walichowekeza na pia walichotoa kama Msaada.

Vya Urusi sijawahi ona hata kimoja zaidi ya kuwachukua watu Wetu na kuwatumikisha kwenye vita huko Ukraine
Vingine ni siri kali,huwezi ambiwa na yeyote,kama vile hujui tuna madege mangapi ya ulinzi wa taifa letu kutoka kwa Mrusi,hata zilizomfurusha Nduli🤸
 
Russia haina msaada wowote ule Tanzania.
Marekani ana msaada sehemu kubwa sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ukiwa na akili huwezi kuwa upande wa Urusi na watetezi wa Urusi Huwa wamejaa propaganda zisizo na msingi miaka ya Leo.

Hata China inatoa pesa Afrika ndio maana anapendwa sasa Russia wanatoa kipi? Bure kabisa
 
Back
Top Bottom