Akombwa Kila Kitu na buzi! Wadada Muwe Makini na Utapeli Mpya

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,131
Amani ya bwana iwe rohoni mwenu!

Shoga yangu mie, mtu wangu wa karibu, ningekuwa nimezaliwa 1990s ningemuita BAE sijui, mambo ya ride or die, sema nilizaliwa dark ages, ze mtandao was not available, KAKOMBWA KILA KITUUUUUU! Kasafishwa haswaaaaaaaa! Na kibuzi or BF in the making. Tobaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Usijute kwanza.

Huyu shoga angu mie katoka UK juzi juzi tu hapa, alienda chukua Masters in kitu gani sijui pale London school of tropical medicines, very expensive education, under very heavy scholarship of the Common Wealth. (Every damn year naomba hii kitu, ndo American dream yangu imelalia hapo, tatizo nyotaaa! Kila mwaka application not successful najuuuuuta kuwafahamu wakoloni hawa. One day Yes) Sasa huko alikaa almost 3 years, alikuwa anaepwa hela nzuri karudi kajipanga kapangika.

Common Wealth ukiwasikia sio watu wa njaa njaaa, wamjipanga, walikuwa wanammwagia sterling pounds za kutoshaaa, aishi comfortably, chezea ze future mind of Tanzania? Thubutuuuuuuu! Afu mtu mwenyewe sio kama Lara ujanja wote kuingia jf basi, Insta siielewi elewi vizuri. Yupo technological savvy. Anamind gadgets za ukwee. Ndo kadondoka nazo.

Navovijua mimi vilivonifanya nishoboke ni I pad Air 2 na I pad Min, Laptop ya Sonny Vaiao Prototype, Original Dr.Dre Beats, Saa ya De Grisogono Instrumento Uno, Iphone 5, Sonny Experia Z na Galaxy Note 3,So (Haya majina tuwiane radhi hivo hivo maana lugha ilikuja na jahazi hii), Camera ya maana, na mazagaa kibao latest versions. Navosema technological savvy sio masiharaaaaa.

Bibie alikuwa yuko vizuri. Anajua vitu vizuri na kuvimiliki. Alivomaliza kule walimua award scholarship ya PHD akachomoa anataka afanye kazi kidogo, azae ikibidi afu shule baadae. Karudi na pond za kutosha katafuta ghetto la maana, kapiga Kitu cha Flat screen, Ultra thin, Super HD, Curved sijui, whooping 51 inches, sofa la royal furnishers, na mizaga mingne ya sebuleni.

Yaani ukimbiwa huyu mtu yupo exposed unakubali. Sio masiharaaa! Mdada tu 25, maisha kayabahatisha. Chezea common wealth weyeee? Hapana chezea.

Akaja akapata mtonyo bank moja mjini, akawa yupo yupo bongo you know! Sasa alipopanga akakutana na mkaka. Waambiwa HB afu ana Harrier ya Silver. Ile kumzoea you know. Madai yake nae anaishi mitaa ile ile. Basi ndo kujifosi kujikaribisha nyumbani, kuona ule m TV naona ali blow mapigo! Msofa wa Royal Funishers ndo kabisaaa. Ikawa kaka gentle man. Uko wapi mda wa kazi , anapigwa lunch KFC.

Si unajua nshomire wakitoka nje basi hadi kuku wakila wanataka wawe wa brand. Najuuuuut. Kaka analipa. Jioni ile wakitoka tukutane sehemu flani, dada anakunywa magarita (Pale samaki samaki 1 glass 14k last time i checked) na shots za japanese liquor na midude kama hio heinken inaonekana ushuzi tu mtoto. Anakunywa hata 10 maana kazoea vodka, kaka wa watu analipa.

One time nili chill nao kisehemu, kaka alilipa damage almost 400k for 3 people pale capetown fish market. Gadem! Mchaga nilimsoma kimya kimya. Shoga angu huyu akinipigia simu najua show si ya kitoto, nmkubali kwanza, si mbabaishaji. Hivo hivo bata batani.

Wakazoeana mambo yakawiva shalo tinatina. Kaka ana hela dada ana hela, watoto wa maskini tukasema kweli ngombe wa maskini hazai, akizaa ujue dume ndo uzazi umeisha hapo na maji hayatoki bahari kwenda mtoni hata siku moja. Mwenye nacho anaongezewa.

(STORY ILIFUTIKA BAHATI MBAYA NAIMALIZIA IN SHORT TU, SWAGA ZILIKUWA ON ORIGINAL VERSION) I

Kaka siku ya mwisho akamuita dada mtoko wa jioni, dada akanywa Margarita kama kawaida akasikia kichwa kizito. Anachokumbuka yule kaka akimuingiza kwenye harrier ya huyu kaka sasa. Akaja kustuka kesho yake usiku maana alilala more than 24 hrs. Akakuta ameibiw kila kituuuuuuuuuu! Kasoro kabati na kitanda ambavyo havipiti mlangoni bila kudis assemble. Kadi za bank ameiba wamebeba mi dollar yote, maskini alikuwa anatafuta kiwanja. Mwenye nyumba akamwambia walimtumia sms kwenye simu ya bi dada awasaidie hao wezi kuhama yeye bi dada kahamishiwa Arusha kikazi na ashatangulia na ndege. Maskini.

Hapa tunavoongea kadata.Polisi wametahadharisha huo wizi upo sanaaaa. Waada muwe macho.
 
Back
Top Bottom