Akojoa kwenye bwawa la maji ya kunywa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akojoa kwenye bwawa la maji ya kunywa...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 24, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Maji yote katika bwawa la maji kwaajili ya wakazi wa mji wa Portland, Oregon nchini Marekani yalimwagwa baada ya mlevi mmoja mjini humo kuamua kukojoa kwenlikuwa majira ya saa saba na nusu usiku wakati Joshua Seater, 21 aliposimama mbele ya bwawa la maji na kukojoa huku akiuelekeza mkojo wake kwenye maji ya bwawa hilo.

  Pamoja na kwamba kulikuwa na giza, kitendo chake hicho kilinaswa live na kamera za ulinzi CCTV.

  Kitendo hicho cha Joshua kilipelekea bodi ya mji wa Portland kuamua maji yote kwenye bwawa hilo yamwagwe na kisha bwawa hilo lijazwe maji mapya.

  Galoni milioni nane za maji ambayo yalikuwa yameishaandaliwa tayari kwa matumizi ya majumbani yalimwaga na hivyo kuutia hasara ya dola 36,000 mji huo.

  Wajumbe wa bodi ya Oregon walipingana kuhusiana na kumwagwa kwa maji hayo ambapo ilidaiwa kuwa kwakuwa maji ya bwawa hilo yalikuwa ni mengi sana, kiasi cha mkojo kilichoingia kwenye maji hayo kisingeweza kusababisha maambukizi yoyote kwa mnywaji.

  Hata hivyo, Bodi ya maji ilisema kuwa watu wangekuwa na mawazo mawili mawili kabla ya kunywa maji hayo iwapo wangejua kuna mtu aliyakojolea, hivyo uamuzi wa kuyamwaga maji yote ulikuwa sahihi.

  Joshua hajafunguliwa mashtaka yoyote ingawa amekuwa akiomba msamaha akisema kuwa amefanya kitendo cha kipuuzi na kama angekuwa ana pesa angelipa gharama zilizotokea lakini kwakuwa hana pesa wala kazi, yuko tayari kufanya kazi za kuitumikia jamii ili kufidia hasara iliyotokea.ye bwawa la maji ya kunywa kwaajili ya wakazi wa mji huo.
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kweli pombe ni mbaya sana!!
   
Loading...