El Maestro
Senior Member
- Apr 12, 2020
- 178
- 126
Vp upinzani wakiwa kwenye jukwa la siasa wakiombea kura wagombea wao wa Upinzani, wanaweza shauri wapiga kura wachague CCM kama wanafaa zaidi ya Upinzani?Hii kauli kama kichwa cha habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.
Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.
Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.
Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.