Uchaguzi 2020 Akiwa Shinyanga Mjini Rais Magufuli anawataka Wananchi wasichague Mbunge wa Upinzani hata kama anafaa, kweli?

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
6,101
2,000
Kuna moja ya uzi ulishawahi kuletwa hapa jukwaani wa "One term president" nafikiri sasa ni wakati wake wakufikia utimilifu wake wote. Zile sauti za kolidoni na wale wahusika sasa ni wakati wao wakutimiza unabii huu.
mbenge, unabii umetimia kama ulivyoagiza
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
14,014
2,000
Kuna moja ya uzi ulishawahi kuletwa hapa jukwaani wa "One term president" nafikiri sasa ni wakati wake wakufikia utimilifu wake wote. Zile sauti za kolidoni na wale wahusika sasa ni wakati wao wakutimiza unabii huu.
Duh
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,868
2,000
Maneno ya Kampeni tu na wanaoambiwa Wana utashi na akili zao, wakiruhusu hilo, Sawa!

Mimi ni mshabiki wa Magufuli Ila Mbunge ni lazima nipembue anayenifaa, awe ni wa CCM au Chama chochote kile
Maneno mabaya ya huyu mtu wenu yatamwandama hadi siku ya kiama
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
13,160
2,000
Kuna moja ya uzi ulishawahi kuletwa hapa jukwaani wa "One term president" nafikiri sasa ni wakati wake wakufikia utimilifu wake wote. Zile sauti za kolidoni na wale wahusika sasa ni wakati wao wakutimiza unabii huu.
Yametimia mkuu
 
LGF

JF-Expert Member
Dec 6, 2020
517
500
Hii kauli kama Kichwa cha Habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Hawezi kuwa anafaa, kwa sababu chungu lazima kiwe na mafia matatu DIWANI MBUNGE NA RAIS. Magufuli alijieleza vi urine Tabata siku ile akimnadi Gwajima. Alisema kuwa Mbunge Halima alikuwa anapinga bajeti za kusaidia ujenzi Kawe kwa vile tu ni mpinzani. Utasema "anafaa"?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom