Uchaguzi 2020 Akiwa Shinyanga Mjini Rais Magufuli anawataka Wananchi wasichague Mbunge wa Upinzani hata kama anafaa, kweli?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
50,832
2,000
Hii kauli kama kichwa cha habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Rais chagua Mkapa lakini mbunge ni chaguo lako by J K Nyerere 1995 Iringa mjini
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,770
2,000
Alete sera za maendeleo aache kutoa hotuba za chuki.
Hana cha kuongea wala kukumbusha. Nyimbo za uchumi wa kati, midege na madaraja ya Dar hazina mvuto huku vijijini. Wakulima kama si uwepo wa uchaguzi walikuwa wamekopwa for good. Hadithi za makinikia ni vichekesho vitupu vya akina Kabundi.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
15,251
2,000
Kati ya wapiga Kura M29+ Kati ya hao ni 1.5M. Pekee ambao wapinzani watagawana hizo Kura,
Sasa jiulize, ni wepi ambao wanapaswa kupimwa akili na Afya ya Ubongo wao?

Je wale M37+ watakaompa Kura Magufuli ndio wakapimwe au wale 1.5M ndio wakapimwe akili, maana na wewe ni miongoni mwa hao 1.5M
Hizi hesabu zako zinaitwaje, au ndo Magufuliglus?
 
Mnyaluhala.

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,385
2,000
We fala kweli unajaza seva za watu na maswali yako ya kijinga. We unaweza kufungua duka alafu wateja wakija unawaambia wakanunue duka la jirani kuna vitu vizuri kuliko dukani kwako?
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Hii kauli kama Kichwa cha Habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Huyu ni rais wa tumbo lake na familia yake,mtu yoyote makini hawezi kutamani kufanya kazi na watu wasio faa.Nashangaa ni mtanzania wa aina gani anayeweza kupoteza muda wake kwenda kumsikiliza huyu incompetent
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,432
2,000
Wakuu tuache ushabiki maandazi, hata kama hatumpendi jee nyinyi mlitegeaaseme tofauti ?, au mnategemea Mbowe aseme umchague mwana CCM kwa ubunge hata awe ndugu yake. Tujitahidi kufikiri kidogo sio kupiga mayowe kwa kila kitu.
 
kinsakina

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
932
1,000
bado tuna mioyo ya unyani,miili inaonekana ni binadamu lakini ndani ni masokwe,itafika kipindi tutaaza kulana nyama hadharani
 
kinsakina

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
932
1,000
Kati ya wapiga Kura M29+ Kati ya hao ni 1.5M. Pekee ambao wapinzani watagawana hizo Kura,
Sasa jiulize, ni wepi ambao wanapaswa kupimwa akili na Afya ya Ubongo wao?

Je wale M37+ watakaompa Kura Magufuli ndio wakapimwe au wale 1.5M ndio wakapimwe akili, maana na wewe ni miongoni mwa hao 1.5M
wezi wa kura nyinyi ,ccm toka lini mkashinda
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
4,875
2,000
Ulitegemea ampigie kampeni wa upinzani.
Hivi kweli we kichwani zimo.
Upinzani nani umesikia akimpiga kampeni mwenzake ashinde.

Kanuni ya " Mtangulize mwenzako"
Ni kwa watu wa dini tu

Na wanasiasa hawana dini wala kanuni za Mungu hazitumiwi
 
NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
11,950
2,000
Haaa,,,!!! Chadema kuna mambo mepesi yanawaumiza nafsi,,,!!!.
Aanze Lissu basi kuonyesha fair play aseme hivi"wanachadema kama kuna wagombea wa CCM wanaofaa muwape kura"
 
Benzodiazepine

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
644
1,000
Kama wewe ni mshabiki wake basi inabidi ukapimwe akili, hauko sawa sawa wewe.
CHIZI PIA HUONA WENZIE NDO MACHIZI. HIVYO KIPIMO CHA AKILI/UCHIZI NI KIGUMU SANA.
Kila mtu ana Uhuru wa kuamua anachotaka kuamini. ila usivunje sheria na kuingilia Uhuru wa wengine.
Cha muhimu ni Tuhamasishane Tukapige Kura Uchaguzi ukifika.
ili Tutumie vizuri haki yetu kikatiba.
 
Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
3,005
2,000
Hii kauli kama Kichwa cha Habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Kosa liko wapi? Huu ni ushindani, kila mmoja anasema ya kuvutia kwake. Mbona mnasema CCM majambazi lakini hawalalamiki? Matusi, kejeli na dharau dhidi ya CCM vimepita kiwango lakini wanavumilia. Vumilieni pia au mkiweza semeni na nyie pia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom