Uchaguzi 2020 Akiwa Shinyanga Mjini Rais Magufuli anawataka Wananchi wasichague Mbunge wa Upinzani hata kama anafaa, kweli?

El Maestro

Senior Member
Apr 12, 2020
178
250
Hii kauli kama kichwa cha habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Vp upinzani wakiwa kwenye jukwa la siasa wakiombea kura wagombea wao wa Upinzani, wanaweza shauri wapiga kura wachague CCM kama wanafaa zaidi ya Upinzani?
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
46,503
2,000
Maneno ya Kampeni tu na wanaoambiwa Wana utashi na akili zao, wakiruhusu hilo, Sawa!

Mimi ni mshabiki wa Magufuli Ila Mbunge ni lazima nipembue anayenifaa, awe ni wa CCM au Chama chochote kile

Ingekuwa tume ya uchaguzi ni huru hapo sawa, lakini kwa tume hii inayodhani jukumu lao ni kuhakikisha matakwa ya rais yanatimizwa unategemea nini? Narudia tena, iwapo wapinzani watasimama kidete kuhakikisha mgombea halali anatangazwa, basi machafuko ni lazima. Unapoona wanajeshi wameongezewa mishahara kimya kimya, hapo tegemea machafuko na mauaji juu.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
20,757
2,000
Hizo ni kampeni, hata Lisu anataka wabunge wote wachaguliwe wa chadema!

Magufuli kama mgombea hawezi kusema chagueni chadema!

Chadema acheni kulalamika kila kitu pigeni kampeni
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
20,757
2,000
Tunaweza kuwa na mgonjwa critical sana wa akili pale Chamwino ikulu.

Kwa kweli tulikosea sana 2015. Hadi aibu naona mimi kama hii ndo akili ya raisi wa nchi!
Naona umeshakata tamaa!

Hizi ni kampeni! Ni maneno ya kampeni haya! Ni kama Lisu anaposema kamwe tusithubutu kuichgmagua ccm,

Kwanini wapinzani mnalalamika sana?

Je ulitaka Magufuli aseme muichgue chadema wakati pale ana kinadi chama chake cha ccm?

Pigeni kampeni acheni kulalamika ni muda wa kampeni huu kila mtu anavutia kwake.
 
niachiemimi

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
3,109
2,000
Lissu akiwa ana mtukana rais Magufuli unafurahia sana. Mimi na muunga mkono Magufuli. Kama kata au jimbo wakachagua mpinzani na Magufuli akafanikiwa kua rais hao watu wasije waka mlaumu.
 
Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,748
2,000
Hii kauli kama kichwa cha habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Kwani jamaa yenu wa kiki na ushuhuda na kutoza sadaka za kikumi anapokuwa anazunguka yeye huwa anawanadi wagombea ubunge wa ccm?
Yaaani akilizenu sijui zikojeeee
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
17,944
2,000
Ndiyo muda wa kusikia maneno yasiyo na kichwa wala miguu,chamsingi ni kuvumiliana tu na kila mtu acheze mechi zake
 
Ngwanashigi Gagaga

JF-Expert Member
Mar 10, 2017
430
500
Hii kauli kama kichwa cha habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Mgombea wa chama chako anasema wachague kiongozi bora kutoka CCM?! Mbona sioni hoja hapo, CCM inaamini viongozi bora wanatoka CCM na nyie mnaamini ni wale wanaopinga kila kitu! Kila mtu anadi anachoamini ,huu ni uchaguzi!
 
wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,985
2,000
Kuna moja ya uzi ulishawahi kuletwa hapa jukwaani wa "One term president" nafikiri sasa ni wakati wake wakufikia utimilifu wake wote. Zile sauti za kolidoni na wale wahusika sasa ni wakati wao wakutimiza unabii huu.
Na kundi lote lile la waganga wanaomuunga mkono?
 
Luthertz

JF-Expert Member
Mar 7, 2018
206
1,000
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa,.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
23,557
2,000
Lissu akiwa ana mtukana rais Magufuli unafurahia sana. Mimi na muunga mkono Magufuli. Kama kata au jimbo wakachagua mpinzani na Magufuli akafanikiwa kua rais hao watu wasije waka mlaumu.
Unaona ujinga wenu sasa.wasimlaumu kwa sababu atawanyima fedha za Maendeleo je hizo fedha ni kodi za wana ccm peke yao au ni zetu watanzania wote? Ndio maana Hamfai kuwa madarakani.
 
BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,294
2,000
Hii kauli kama kichwa cha habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
Ulitaka awaambie kuwa, "chagueni wabunge wa upinzani?" Acheni kulia lia.
 
BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,294
2,000
Unaona ujinga wenu sasa.wasimlaumu kwa sababu atawanyima fedha za Maendeleo je hizo fedha ni kodi za wana ccm peke yao au ni zetu watanzania wote? Ndio maana Hamfai kuwa madarakani.
Kila mmoja atakula alipo peleka mboga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom