Uchaguzi 2020 Akiwa Shinyanga Mjini Rais Magufuli anawataka Wananchi wasichague Mbunge wa Upinzani hata kama anafaa, kweli?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,214
2,000
Hii kauli kama Kichwa cha Habari kinavyosema eti hakuna kuchagua mbunge wa upinzani hata kama anafaa.

Maneno kama haya kuzungumzwa na kiongozi mwenye dola ambaye anawania muhula mwingine wa uongozi ni kuhujumu uchaguzi mkuu.

Maneno kama haya kuzungumziwa wananchi ni kama kuwatisha kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora. Kauli hii haikubaliki kamwe.

Mbaya zaidi kauli kama hizi ndizo zinaleta mzozo mkubwa siku za kutangaza matokeo. Kimsingi kauli hii ninaiona kama imetoka katika kinywa kilichokosa ustaarabu mkubwa wa kisiasa. Mbaya zaidi anayezungumza ni kiongozi wa nchi anayehubiri kuwa maendeleo hayana chama.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,604
2,000
Kuna moja ya uzi ulishawahi kuletwa hapa jukwaani wa "One term president" nafikiri sasa ni wakati wake wakufikia utimilifu wake wote. Zile sauti za kolidoni na wale wahusika sasa ni wakati wao wakutimiza unabii huu.
 

Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
692
1,000
Huwezi pangia wananchi wamchague nani katika jimbo husika, kwanza Rais na jimbo wapi wapi? maana hadi kufikia kumpigia fulani kura ili awawakilishe bungeni ni kwamba wana imani nae, Jiwe aache za kuleta kwanza ilitakiwa awe anapanda ndege kama JK bahati mbaya lugha ya malikia imempiga chenga.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,350
2,000
Tuwekee kipande video mkuu, mkoloni mweusi hatari, akumbuke alipo mzee Mkapa leo akanyage kwa adabu ardhi ya Muumba.
 

Gmox

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
303
500
huko ni kukosa uungwana... kwanini ahubiri chuki badala ya haki hakika anastahili kupingwa na kila mtu kwanini atugawe kiasi hiki...😏
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,251
2,000
Chuki huwa haimuishi, Rais anayekataa kutoa pesa kwenye majimbo ya upinzani halafu humu kuna vidudumtu vinasema Lissu anaonesha chuki kwa mgombea wa CCM!
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
10,715
2,000
Kwa hiyo CCM wameweka mtu wao hata kama hafai,tofauti na chaguo la wananchi. Hii ni dharau kwa wananchi...CCM wametuona mazezeta


Hii ni ishara kwamba hata yeye kishajiona hafai kwasababu ya upepo wa kisiasa anaouona leo, kwakuwa hafai basi watu wamchague tu !!!!.

Hili ni kosa kubwa alilolifanya kwa miaka 5 ya kuwafungia wapinzani wasifanye shughuli za kisiasa, katika kipindi hicho hakujua kina cha maji ya kisiasa yakoje kwasababu wapinzani walikuwa kifungoni katika kipindi hicho naye alijiamini na ushindi kupita kiasi, sasa anashangaa kuona kina cha maji kipo shingoni bado kidogo kifike mdomoni.

Haya ndiyo mambo yaliyomkuta K, Kaunda wa Zambia na chama chake cha UNIP.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,504
2,000
Kama wewe ni mshabiki wake basi inabidi ukapimwe akili, hauko sawa sawa wewe.
Kati ya wapiga Kura M29+ Kati ya hao ni 1.5M. Pekee ambao wapinzani watagawana hizo Kura,
Sasa jiulize, ni wepi ambao wanapaswa kupimwa akili na Afya ya Ubongo wao?

Je wale M37+ watakaompa Kura Magufuli ndio wakapimwe au wale 1.5M ndio wakapimwe akili, maana na wewe ni miongoni mwa hao 1.5M
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,815
2,000
Wananchi wanatakiwa kumuonesha kwa vitendo wana akili zao timamu, hawadanganyiki wala kupangiwa jambo la kufanya na mtu yeyote, na hilo sina shaka nalo, jibu atalipata oktoba.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
8,102
2,000
Tunaweza kuwa na mgonjwa critical sana wa akili pale Chamwino ikulu.

Kwa kweli tulikosea sana 2015. Hadi aibu naona mimi kama hii ndo akili ya raisi wa nchi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom