Akitoa hotuba wakati wa kuapishwa Dkt Magufuli. Je, mtazamo wa Museveni unahakisi ule wa wengi wa Marais wa Afrika juu ya demokrasia ya vyama vingi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Nimejaribu kumsikiliza Rais Museveni wa Uganda wakati wa kuapishwa kwa Rais Dr Magufuli ili kuelewa anasema nini hasa. Nakubaliana nae juu ya mambo manne aliyoyasema- liberation, prosperity, strategic security na brotherhood. Ingawaje hiyo strategic security sikuielewa vizuri.

Pia alisema kuwa vyama vya upinzani havina uelekeo, yaani itikadi na kufikia kusema suala juu ya vibaraka. Kwa kifupi, ushindi wa CCM anauona kama ni ushindi wa wazalendo dhidi ya 'vibaraka', na kujihakikishia kuwa bado kuna wananchi wanavihitaji vyama aina ya CCM kikiwemo chake kwani alisema kura nyingi za 2015 kule Ilemela zilionesha kuwa bado kuna watu wao, na hivi juzi kule Hai, imeonesha kuna watu wa aina anayoipenda.

Cha kushangaza hakuona dosari za uchaguzi, pili anaangalia TV moja tu TBC1, na anasema ni uchaguzi wa amani.

Ila hawa ni 'ndege wanaofanana huruka pamoja.'

 
Kwani kuna asiyejua kulikuwa na vibaraka uchaguzi huu?
Jamaa ameshangazwa na jinsi Nyerere alivyopandikiza uzalendo na umoja kwenye taifa hili.
 
Back
Top Bottom