Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?

kuna link yeyote labda tusome au tuone clip Makonda akijifananisha na Mungu?
Kuna clip inatembea kwenyemitandao ya kijamii hasa whatsapp alipokua akiongea na bi Rehema ndipo hilo neon lilipo mtoka kinywani mwake. NI kweli alisema hivyo though kila mtu anaweza kua na tafsiri yake.
 
Mimi mpaka sasa nimekuwa nikiwashangaa watu kwa kujitolea kuwasaidia wagonjwa wengine wa akili lakini wanamtelekeza Makonda.
Najua Makonda uu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

mimi-mungu-jpg.441219

Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda.
 
Makonda ni demagogue kwa walisoma political science !! ameenda mbali, ulimi uliteleza, ila sasa uliteleza kweli? je kwa nafasi yake ulimi uteleze ? akatubu tu!! na tumuombee tu
 
Huyu atapinda huo mdomo kama Seif Khatib siku sio nyingi

Ila mbona kama nimemuelewa Makonda ,Alisema mimi nikisamama mahali Mungu amesimama ,yaani kwamba alipo yeye Mungu yupo naye au mimi ndio sielewi ?

Hakuna sekta ilikuwa imeoza kama ardhi ,alitakiwa awatie vibao kabisa hao washenzi
Acha kupotosha habari uzuri video bado ipo hewani, alisema akisimama yeye ni sawa kasimama Mungu.
 
Acha kupotosha habari uzuri bado video ipo hewani, alisema akisimama yeye ni sawa kasimama Mungu.
Mkuu Makonda sijawahi kushawishika naye tokea ameingia madarakani .ila pia usinilazimishe kwamba tafsiri uliyonayo wewe juu ya huo msemo ndio sahihi zaidi ya tafsiri yangu ..kila mtu kautafsiri kwa namna yake
 
Ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka. Jamaa imefika mahala anajiweka sawa na Mungu. Hii ni kufuru!! Jamaa anabahati sana hajakutana na watu waliopinda, angejuta kuzaliwa kwa kutoa kauli kama hizo.
 
Mkuu Makonda sijawahi kushawishika naye tokea ameingia madarakani .ila pia usinilazimishe kwamba tafsiri uliyonayo wewe juu ya huo msemo ndio sahihi zaidi ya tafsiri yangu ..kila mtu kautafsiri kwa namna yake
Haya kichaa mwingine huyu...yaani maneno kayatamka Makonda kwa mdomo wake, wewe unataka kuleta tafsiri zako za kijinga! Hebu msikilize tena kwa makini na kama bado utaamini kuna tafsiri zaidi ya tunayoisikia basi na wewe unayo matatizo ya akili kama huyo Makonda wako.
 
Kuna statement zingine ni obvious huwezi kupindisha hata robo.
 
Jamaa ana akili mbovu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
With due respect, weka m badala ya M
 
Wana JF and All GTs,

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Bwana Paulo Makonda ametoa matamshi mazito kwenye moja ya mikutano yak ya kutatua kero za Wananchi!
Kitendo cha kusema nanukuu

,"NIKISIMAMA MIMI NI MUNGU AMESIMAMA" ni kauli ambayo kwa Imani za Kikristo ni KUFURU kwa Mwenyezi Mungu! Kulingana na Biblia Takatifu mtu anayemkufuru Mungu hawezi kubaki salama.

Tanzania tuna Maaskofu, Masheikh na Wachungaji mimi naomba watoe tamko kulingana Imani zao kama alichosema Makonda ni sahihi au siyo sahihi! Maana kama mwanadamu mwenzetu anasimama mbele ya hadhara na kudai yeye ni Mungu basi anaweza kufanya lolote na asiguswe!

Karibuni kwenye mada.
 
Haya kichaa mwingine huyu...yaani maneno kayatamka Makonda kwa mdomo wake, wewe unataka kuleta tafsiri zako za kijinga! Hebu msikilize tena kwa makini na kama bado utaamini kuna tafsiri zaidi ya tunayoisikia basi na wewe unayo matatizo ya akili kama huyo Makonda wako.
Eti anataka tuamini alimaanisha alipo Makonda Mungu yupo, anataka kutufanya sisi ni watoto wa class 2.
 
Haya kichaa mwingine huyu...yaani maneno kayatamka Makonda kwa mdomo wake, wewe unataka kuleta tafsiri zako za kijinga! Hebu msikilize tena kwa makini na kama bado utaamini kuna tafsiri zaidi ya tunayoisikia basi na wewe unayo matatizo ya akili kama huyo Makonda wako.
Asante mkuu mimi ni kichaa kwa sababu tu sijakubaliana na unachotaka wewe ila pia wewe utakuwa kichaa zaidi kumuingiza Magufuli kwenye hili la Makonda sijui kuna uhusiano gani wa kauli aliyotoa Makonda na Mungu wa Magufuli

Halafu nyie ndio mnaojiita wakongwe wa Jf mnasikitisha
 
Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

mimi-mungu-jpg.441219

Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda. Hapa yabidi tujiulize kwa nini mpaka dakika hii mteuzi wake hajachukua hatua yoyote kutunusuru raia na kadhia hii?

Najua pia kumetokea si mara moja ama mbili tu Makonda, ameamrisha Jeshi letu la Polisi, kutii amri zake zisizo na uhalali wowote. Bila shaka haya yote yemewezekana kwa sababu Makonda akitamka, mungu katamka. Hii imewajengea wengi taswira kwamba kila anachofanya Makonda kina baraka za aliyemteua ambaye pia ndiye Jemadari Mkuu wa Taifa kikatiba. Sasa kama Makonda ni mungu, Rais Magufuli pia ni moja katika waumini wake?

Makonda Kiboko yenu
 
Back
Top Bottom