Akiondoa Wazee Baraza la Mawaziri ametatua tatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akiondoa Wazee Baraza la Mawaziri ametatua tatizo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 17, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli Rais Kikwete anaamini tatizo la baraza lake la Mawaziri ni Umri? Kwamba akiweka vijana zaidi ndio ametatua tatizo la uongozi? Nchi gani duniani inaongozwa na viongozi vijana na imefanikiwa? Mheshimiwa Rais tatizo siyo umri; ni uwezo! Nipe wazee wenye uwezo wa uongozi siku yoyote kuliko kunipa vijana ili kufurahisha macho!

  Hivi viongozi vijana waliopo sasa kwenye baraza lake wana fair vipi kulinganisha na wazee?

  Ippmedia

  Rais Jakaya Kikwete ameahidi kuwa kama akijaliwa kupata kipindi cha pili cha kuiongoza Tanzania, atafanya jitihada kubwa kuubadilisha uongozi kuwa wa vijana.

  Akizungumza na vijana kutoka nchi kadhaa za Afrika juzi jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete pia alisema vijana ndiyo Tanzania ya kesho, na kama nchi haitawekeza vya kutosha kwa vijana na maendeleo yao, basi itakuwa haiwekezi katika hali yake ya baadaye.


  Katika mkutano huo wa Mpango wa Kulea Uongozi wa Afrika ambao unadhaminiwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Anglikana wa Afrika Kusini, Desmond Tutu, Rais Kikwete alisema anauthamini mpango huo na kusisitiza kwamba kadri miaka inavyokwenda ni lazima rika la wazee lipishe lile la vijana.

  “Kwenye uchaguzi mkuu ujao kama nitajaliwa na nikapata bahati ya kuchaguliwa tena, nitahakikisha kuwa naubadilisha uongozi wa Tanzania kwa kuufanya uongozi wa vijana zaidi," alisema.


  Aliongeza: “Wale viongozi wa rika langu, lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi, na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.”


  “Vijana ndiyo matumaini ya nchi hii katika miaka ijayo na kama hatukuwekeza kwa vijana wetu, basi ni dhahiri kuwa hatuwekezi ipasavyo katika miaka ijayo ya taifa letu,” alisisitiza.
  Baraza la Mawaziri la sasa la Rais Kikwete lina jumla ya mawaziri na manaibu mawaziri 51.

  Katika baraza hilo, mawaziri wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ni 14 wakati wenye umri kati ya miaka 50 hadi 59 ni 25. Mawaziri na manaibu mawaziri wenye umri chini ya miaka 50 ni 12.
  Waziri mwenye umri mkubwa kuliko wote ana miaka 67 akifutiwa na mwenye umri wa miaka 66.


  Akijibu maswali ya vijana hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Tanzania, Nigeria, Kenya, Afrika Kusini na Uganda, Rais Kikwete aliwaeleza vijana hao jinsi gani alivyojikuta anaingia katika siasa.
  Akijibu swali kuhusu maendeleo ya karibuni katika siasa za Zanzibar, Rais Kikwete alisema ni jambo la kufurahisha kwamba vyama vya siasa Zanzibar vimeamua kuachana na siasa na mazoea ya zamani na kuanza ukurasa mpya.


  “Nawatakia heri sana katika mwelekeo mpya na sahihi kabisa katika uendeshaji wa siasa. Ni mwelekeo ambao sote tumekuwa tunautafuta kwa muda mrefu,” alisema.


  Katika siku za karibuni, Chama cha Wananchi (CUF) kimeamua kumtabua Rais Amani Abeid Karume kama Rais halali wa Zanzibar, hatua ambayo imefungua kila aina ya uwezekano wa kupatikana maelewano na mwafaka Tanzania Visiwani.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mmkj hivi kweli na wewe unaamini hili? Mbona mimi nina wasiwasi sana na hili?
  Basi Bwana ninachoomba sio Seif kurudi tena kulia lia mwakani mwishoni, akishapigwa chini kwa namna yoyote ile. Sawa? Maana naona wazanzibari wanafanyiwa usanii kila siku na wanakubali tu kirahisi mkuu.
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
  MF
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hao anaowaita mawaziri wake vijana ndio hao wengine wanavuta bangi na kushinda kulewa Rose garden!! Uwezo wa mtu ndio kigezo sahihi na sio umri wake!! Muelewesheni Jakaya kama amewahi kumsikia THE ORACLE OF OMAHA na success zake na ana umri gani?
   
 4. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kikubwa ni vijana wenye hulka na maadili mazuri, wenye uchungu na wananchi wa Tanzania; sio vijana aina ya akina Masha, Nchimbi n.k. kwani aina hiyo haitufai....!
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hana jipya ... ameanza kampeni kwa ajili ya kuwachota akili vijana hapo mwakani. Anajua vijana wana uelewa na hivyo ni rahisi sana kugawa kura kwa mgombea mwingine iwapo watasomeshwa na kuelewa.

  Hivi kwanini watanzania huwa tunatumika kirahisi sana? Mwaka 2005 JK alianza kubembelezwa na wasomi wa Mlimani wakiwa na matumaini kwamba akiingia Ikulu angeleta mabadiliko, lakini hakuna kitu.

  Mkapa wakati akimnadi JK kwenye Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 2005 alisema kwamba asilimia kubwa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ni Vijana na hivyo wawe makini wanapopiga kura zao, wampe kijana mwenzao kwa kuwa anaweza kuwa anaelewa matatizo ya vijana. Mpaka leo hii sijaona alichofanya JK katika kuwasaidia hao vijana.

  Mwaka 2005 siku JK ametua Dar akitokea Dodoma akiwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, alilakiwa na akina mama na vijana kibao, nikiangalia zile picha huwa ninatoa machozi maana watu walikuwa na matumaini makubwa sana kwamba sasa Mussa amekuja kutuondoa jangwani na kutupeleka nchi ya ahadi, Kanani, nchi ya asali na maziwa.

  Leo ni mwaka wa nne sijaona hayo maziwa wala asali. Bado tunaendelea kusota Jangwani, na hatujui tutatoka lini hapa Jangwani then jamaa anaanza tena ngojera kwamba yeye ni Mussa wa kweli, tukiendelea kumvumilia atatuvusha! BS!

  Vijana siyo suluhisho la matatizo ya uongozi Tanzania. Ngeleja na Malima ni vijana, wamefanya nini pale Nishati na Madini? Hawa wametaka kutuingiza kwenye mkenge wa kununua Dowans, umeme hakuna, madini yanaishia na hakuna tunachonufaina nacho.

  Masha kaleta nini kipya pale Mambo ya Ndani zaidi ya skendo ya mradi wa vitambulisho? Dr. Mwinyi na Nchimbi wako kule Ulinzi na Kujenga Taifa, naona ni mwendelezo wa ufisadi tu, hakuna kipya.

  Hata ukileta vijana kwenye Baraza lote la Mawaziri, kama wana mawazo ya kifisadi, hawako creative, hawajui priorities na hawajui wanatakiwa kufanya nini, ni sawa na kutwanga maji kwenye kitu. Miaka 5 ikiisha utajikuta umerudi nyuma hata 2 badala ya kusonga mbele japo hatua moja.
   
 6. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Issue hapa ni
  1-Lazima atagombea tena 2010,
  2-Kesha anza kampeni kwa ahadi mpya kwa vijana,
  3-Anajaribu kuonyesha kuwa wazee ndio wanamuangusha kwa ufisadi,

  Haya basi hebu tujaribu kufikiria hao vijana ambao si wa aina yao hao wazee alionao sasa ni kina nani ndani ya CCM? au atawatoa mbinguni?
   
 7. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu mheshimiwa inabidi aambiwe wazi kuwa tatizo la serikali yake ni yeye mwenyewe. Kama anafikiri tatizo la serikali yake ni wazee wenzake, basi na yeye aachie ngazi kwa sababu hizo hizo za uzee.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Hawa mawaziri vijana anawataka anawatafutia wapi? Maana waliopo wameonyesha wazi kuwa wengi hawana uwezo wa kuwa mawaziri. Bado utoto utoto unawasumbua. Lakini hata hivyo, wapo vijana wenye uwezo ingawa hawana kabisa nafasi ya kuwa viongozi maana hakuna anayewajua. Rais kweli ana kazi nzito!!Urais ni zaidi ya kuandika historia
   
 9. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kauli sahihi tatizo ni mazingira ya utekelezaji wake.

  Nchi hii inahistoria ya kuongozwa na VIJANA tena mwanzoni kabisa mwa UHURU wake.
  Mwalimu alikuwa na miaka 39 wakati anakuwa RAISI wa kwanza wa Taifa hili..Ni umri wa Kijana anayezungukwa na busara zaidi...
  Alizungwa na baraza la mawaziri vijana wengiiii..Mchango wao kiuongozi unaonekana..

  Wengi waliendeleaa na awamu zilizofuata hata wakawa wazee na bado wapo na wanaishi kama watawala kwa kila jambo wafanyalo na kushauri mpaka sasa..

  Tatizo sio vijana. Tatizo ni mazingira ya aina gani yaliyopo kiuongoziiiii yanayomzunguka kijana au mzee aliyepewa madaraka ya kuongozaa..Kikwete naye alianza uongozi kama kijana mpaka anaukwaa URAISI alikuwa na bashasha za Ujana. Ni moja ya kigezo muhimu cha ule ushindi wake wa Tsunami!!!!

  Ndio anatambua umuhimu na utamu wa vijana katika uongoziii..
  Mwanakjjj Usiogope kauli ya Raisi kwani hisia zako ndizo kikwazo kwamba vijana atakaowachagua ni wale wale..Ndio lazima wawe wale wale kwani ndo walioko pamoja katika MIKAKATI ya kuwepo madarakani DAIMA..

  Tubadili mazingira yetu ya kiuongozi ili kuwa na viongozi watenda kazi, waadilifu na wenye upeoo wa kupimika kijamiiii bila kuangalia umri wao.
  Marekani wao wana mazingira hayoo tayariiii..
   
 10. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bravo Rais JK kwa hili tuansubiri kwa hamu kubwa mabadiliko hayo,ikiwezekana yafanyika hata ndani ya chama cha ccm
   
 11. GY

  GY JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Labda anataka kutumia Maximo style!
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Nov 17, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Goodness gracious!! Hata hajui alisemalo.
   
 13. P

  PWIDA Member

  #13
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 20, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 25
  Hivi nahodha kama hajui anakokwenda si atafika bandari yeyote tu au ataishia kugonga mwamba, kusema atabadili mabaharia na kuweka vijana si bado kama hana anakokwenda si ataishia popote labda watamsaidia kufika huko popote haraka. Tatizo letu sio uzee tatizo letu unataka kutupeleka wapi mpaka sasa hujui tunakotaka tuende na hivi juzi juzi ulikiri ilani za ccm ukushirikishwa kuziandaa kwa hiyo hazitekeleziki (haya yalisemwa na mwenyekiti wa chama). Na kama ilani ya ccm sio yako na wewe ya kwako ujaweka wazi basi hapa tulipo hatukufika kwa bahati mbaya maana kuaamua au kutokuamua yote ni maamuzi hata kama hukuwa timamu katika hayo yote mawili ya kuamua au kutokuamua.

  Hatuwezi kuendelea kwa kubahatisha tu. Maendeleo ya kweli upangwa na kazi kufanyika kuyafuata maendeleo hayo uliyo yapanga, unapoyalenga unaendelea kuyafuatilia mpaka uyapate.

  Mpaka sasa hatujui msimamo wako zaidi ya kukaaa kimya kila wakati watu wanapoitaji muongozo wako.

  Walau tungejua kuwa baba analia njaa na uwezo wa kutafuta chakula hana, ndio by natural law mtu mwingine angechukua madaraka yako kufanya hilo usiloliweza. Ukikaa kimya tunafikiri unatunga sheria kumbe ???????

  Tumekuwa watu wa kulalamika tu siku zote hizi ulizoingia madarakani, wananchi wanalalamika, rais analalamika, ccm wanalamika, wapinzani wanalalamika.

  Viongozi wako wapi? Kama wote tumebaki kwenye cycle ya malalamiko. Tatizo letu kubwa hapa tanzania ni viongozi wafuasi wapo kibao wanasubiri viongozi ambao hawapo.

  Mbaya zaidi watu wote wenye mapenzi mema mmepotea hampo mmetuachia hawa watuongoze makaburini.

  Wale waliokuwa wanachagua viongozi wenye busara zao wako wapi? Haingii akilini kuwa na mawaziri ambao unapaswa kumfundisha kwanza aishi vipi kama mke au mume, halafu ukamwambia aende vipi kama waziri? Jama huo muda wa mafunzo hayo yote tunao?
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,673
  Likes Received: 21,903
  Trophy Points: 280
  Wabunge wetu walituletea Taarabu na mipasho kule Dodoma, sasa na mkuu naye anatupatia ngonjera? Ah! mapambazuko hayawezi kuja yenyewe nchi hii, labda atokee jasiri na kumtekenya jogoo ili awike kuche.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Ni jambo zuri analilifikiria Rais.Najiuliza tu hao vijana ndio wale waliomo UVCCM au kuna strategy gani hasa ya kuwapa watu mahiri na sio opportunist ambao leo wanaonekana wazi kuwa mzigo mkubwa kwa nchi maskini kama yetu maana hakuna mchango wa maana wanaoweza kujivunia. Siamini kabisa kama kweli hakuna vijana wenye uwezo wa kufanya maajabu.Yes! Wapo. Ila wataonekanaje?????
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jamani amesema anawaanda vijana...kuandaa ni pamoja na kuanza kuweka vijana katika uongozi..sijui kitu gani hamuelewi nyinyi?? lol
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Hivi Boris Yetsin alimuonaje Putin kama ni kiongozi anayeweza kumrithi? Nahisi, hakuwa kwenye wale waliokuwa wanachuana kumrithi na kufanya kazi ya urais kama wasipoipata basi maisha nayo hayatakuwapo, maana hata Nyerere alituasa tuwaogope kama ukoma and yet he was tough!
  Na secret service je walimuonaje? Nahisi walimuona akiwa anacheza judo wakajenga interest, na baadae wakamuona anawafaa.
  Sisi tuko vipi katika kutambua vipaji vya watu watakaofaa kuwa viongozi wa baadae?Hili kwangu ni suala la muhimu sana maana kama tutapata viongozi wazuri, hata muelekeo wa mambo utabadilika sana
   
 18. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani Mkuu atakuwa amepotoka sana kama anadhani umri ndio utatuzi wa matatizo ya nchi hii.

  Uongozi, kama ilivyo kazi nyingine yoyote inahitaji uzoefu (Experience is the mother of all education). Lakini pia, kiongozi anaeteua viongozi wenzake inabidi atambue ufahamu, ujuzi na uzoefu wa wale anaotaka kuwateua. Ajue anataka kufikia mafanikio gani, kwa muda gani na ni sifa gani za uongozi zinazoweza/zinazotakiwa kukamilisha mategemeo yake. Kuteua vijana au wazee bila kuzingatia mahitaji halisi ni kupiga maji kwa fimbo, hayatakimbia.

  Ili kuwe na ufanisi, tunahitaji mikakati, ubunifu na utaalamu zaidi ya tunavyofanya sasa ili nchi iweze kuendelea au kupiga hatua zenye kuleta maana katika kila sekta.

  Taarifa hii inanikumbusha makosa ambayo viongozi hufanya katika kuteua watu kushika madaraka ya juu ya uongozi. Mtaalamu wa mifupa, sio lazima awe kiongozi mzuri wa hospitali. Anaweza kupewa nafasi ya kukua zaidi katika fani yake bila kuwa kiongozi wa watu kwenye taasisi yake. Vinginevyo, ni rahisi kujikuta unampoteza katika taaluma yake, na vile vile kukosa kiongozi bora (unakosa yote). Hii haina maana pia kuwa wataalamu wote hawana uwezo wa kuongoza. Uongozi ni sifa ambayo si kila mtu anayo. Ni vyema kujua mtu binafsi ana uwezo gani wa kuongoza kabla hajapewa madaraka.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inafaa akae chini tena atafute chanzo cha mtatizo yanaoikabili serikali yake na chama chake kwa sababu matatizo hayo hayapo katika umri wa mtu yeyote
   
 20. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Tatizo hapa sio Kikwete, bali ni sisi tunaopoteza muda wetu kufuatilia siasa za Tanzania. Kusema ukweli, mtu ukitaka kuwa kichaa basi fuatilia siasa za Tanzania ! Nchi imeoza kwenye kila sekta that one can imagine , matatizo ya Tanzania ni zaidi ya Kikwete au baraza la mawaziri. Tatizo kubwa ni culture of corruption ambayo imejenga mizizi kwa decades sasa.

  Watu wamekuwa super selfish and worst of all shallow minded. Inasikitisha kuona vijana wengi hata wale wenye exposure are flocking to CCM , this is really SAD! Nashindwa kuelewa hata hao mnaowaita wapiganaji ambao wako ndani ya CCM, the question that we ought to ask ourselves is how is someone going to bite the hand that feeds him/her ?
   
Loading...