Akina nani wakumbukwe?

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,586
1,678
Naleta uzi huu baada ya kuona mwelekeo wa kuvipa majina kiholela vitu muhimu, mali ya Watanzania wote. Aghalabu majina ya wanasiasa ndiyo tu yanayotumika. Tena wanasiasa wawili au watatu tu. Aidha, mtoaji wa jina huwa hakushauriana na yeyote, licha ya kuwa hana utaalamu mkubwa katika historia ya Tanzania.

Katika nchi nyingi duniani zinazojitambua, utoaji wa jina huwa ni heshima kubwa kwa huyo aliyeteuliwa na hili huandamana na mchango mkubwa, wa kipekee na nadra, alioutoa mhusika katika jamii, ima wa uongozi, fani, fikra na hata uhai wake. Mchango huu aghalabu manufaa yake hudumu vizazi na vizazi.

Na ili kujiridhisha kuwa mtu huyo anayetunukiwa amelifanya hilo si kwa kupita tu bali kwa imani ya daima, aghalabu jina hutolewa baada ya mtu huyo kuondoka duniani.

Nchi nyingi huweka sheria za namna heshima hiyo itavyotunukiwa mwananchi. Baadhi ya nchi huweka jopo maalum linalopendekeza, na nyingine ni bunge ndilo hupitisha heshima hiyo.

Alas! Siyo hapa kwetu hapa Tanzania! Heshima hiyo hugawiwa kiholela kama njugu kwa muktadha wa mapenzi na utashi wa kiongozi mwanasiasa! Wengine hujibandika wenyewe heshima hiyo, na wengine hubandikwa na sycophants (wachumia tumbo) wao!

Hii ni hatari sana. Kwamba wale watoao mchango nadra husahauliwa na badala yake waliofika madarakani kwa mbinu zozote ndiyo huwa 'mashujaa' wa kukumbukwa! Hata kama walichokifanya hakikumbukwi tena baada ya miaka yao ya uongozi, maana si kitu nadra wala cha kipekee!

Kuna Watanzania hadi leo mchango wao unakumbukwa na kusomwa na watu wa mataifa ya nje, lakini hapa kwetu hakuna hata kibanda kilichopewa jina lao!

Wapi utaona kumbukumbu ya kama JOHN STEPHEN AKHWARI, EDWARD SAID, SITI BINTI SAAD, FREDDIE MERCURY, MATHIAS MNYAMPALA? La hasha! Bali nusu ya wasomaji wa uzi huu naapa hawawajui wote hao na mchango wao mkubwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom