Akina Kingunge waenguliwa rasmi Ubungo. Ni baada ya kuiibia Serikali mapato

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,050
Jiji laanza kufaidi Mapato Kituo cha Mabasi Ubungo

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imeanza kazi ya kukusanya mapato katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo (UBT), Dar es Salaam, kutokana na kumalizika kwa mkataba wa Kampuni ya Smart Holdings inayomilikwa na familia ya mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi wa Jiji, Bakari Kingobi alisema mkataba huo na Smart Holdings uliokuwa umeanza Novemba 31, 2004, umemalizika juzi na kitakachofuata ni kutangazwa kwa upya kwa zabuni kwa ajili ya shughuli hiyo.

"Tayari tumeshakabidhiwa rasmi hapo juzi baada ya mkataba huo kuisha kwa kuwa ndio utaratibu uliokuwepo na kwa sasa Jiji ndiyo linaendesha shughuli ya ukusanyaji mapato katika eneo lile mpaka hapo baadaye tutakapoamua kutangaza zabuni nyingine," alisema Kingobi alipozungumza kwa njia ya simu na gazeti hili.

Jana, gazeti hili lilishuhudia wafanyakazi wa Jiji wakiwa na mavazi rasmi yenye vibandiko vya ofisi hiyo wakifanya kazi ya kuchukua mapato milangoni kwa magari yanayoingia na kutoka katika kituo hicho kikuu cha mabasi.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Smart Holdings, Hassan Khan alisema wapo tayari kuomba tena zabuni ya kukusanya mapato kituoni hapo mara itakapotangazwa na Jiji, kwa kuwa imejiridhisha na namna walivyofanikisha kufikisha malengo ya ukusanyaji wa mapato na kuyakabidhi serikalini bila upungufu wowote.

Khan alisema katika kipindi chote cha mkataba huo, kampuni hiyo imezingatia kanuni na kutimiza masharti yote ya mkataba; na katika ukusanyaji wake, imekabidhi zaidi ya Sh bilioni 3.8 kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji kulingana na makubaliano ya mkataba huo.

Alisema kampuni hiyo na Jiji zilitia saini makubaliano ya kazi ya ukusanyaji wa ushuru wa magari, wasindikizaji na wapokeaji wa abiria na kuhakikisha makusanyo yanafikia lengo la Sh milioni mbili kwa siku.

Khan alisema katika fedha hizo, Halmashauri ya Jiji ilikuwa ikichukua Sh milioni 1.5 sawa na asilimia 75 kwa siku huku Smart ikibakiwa na Sh 500,000 ya lengo kwa siku.

Alisema kwa upande wa kukusanya kodi za pango la mwezi kwa wafanyabiashara wadogo ndani ya kituo hicho, Halmasahauri ya Jiji ilitoa orodha ya wafanyabiashara na Sh 26,888,880 za lengo lililotakiwa kukusanywa kwa mwezi, Jiji lilikuwa likipata asilimia 80 bila kukosa huku kampuni hiyo ikibakiwa na asilimia 20 ya makusanyo hayo.

Kuhusu umiliki wa kampuni hiyo na hasa kuihusisha na familia ya Kingunge, alisema kampuni hiyo imesajiliwa na wamiliki watatu tofauti na siyo familia hiyo pekee.

"Kampuni ya Smart Holdings Ltd haimilikiwi kwa asilimia mia na familia hiyo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu…hii ni kampuni ambayo ina wamiliki watatu tofauti ambao ndio hao walioisajili pale Brela," alisema Khan.

Aliwataja wamiliki wengine kuwa ni Victor Mwiru ambaye pia ni Mkurugenzi mwenza wa Khan katika kampuni hiyo na Peres Mwiru ambaye ndiye Mwenyekiti.

Mwaka jana katika ziara yake mkoani Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilalamikiwa na wananchi kuhusu ubadhirifu wa fedha katika kituo hicho cha mabasi, huku mameneja wake wakijikanganya kuhusu mapato halisi serikali inayopata hapo.

Kutokana na hali hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alifanya ukaguzi maalumu kwenye kituo hicho pamoja na Soko Kuu la Kariakoo, na tayari amekabidhi ripoti zake kwa Waziri Mkuu ambaye wiki iliyopita alisema bungeni kuwa zinafanyiwa kazi na watendaji wake na zitawekwa hadharani hivi karibuni.

Romana Mallya | Nipashe

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza rasmi kukusanya mapato katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) baada ya mkataba wa kampuni binafsi inayomilikiwa na familia ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyokuwa ikifanya kazi hiyo kukatishwa.

Kampuni ya Smart Holdings, inayomilikiwa na familia ya Mbunge huyo wa kuteuliwa ilipewa zabuni ya kukusanya mapato kituoni hapo na imekuwa akifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kutolewa malalamiko kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikikusanya mapato makubwa, lakini ikiishia kuilipa serikali fedha kidogo Sh. 1,500,000 tu kwa siku hata kama imekusanya mapato makubwa zaidi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotembelea kituo hicho Machi mwaka huu, alimuagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kufanya uchunguzi na kuwasilisha taarifa ofisini kwake.

Aidha, Pinda alimwagiza CAG kukagua ukusanyaji wa mapato katika Soko Kuu la Kariakoo.

Utouh alikabidhi ripoti ya Ubungo kwa Pinda mjini Dodoma Julai mwaka huu wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge.

Hata hivyo, Pinda wiki iliyopita wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni alisema kuwa ripoti hiyo inapitiwa na Katibu Mkuu wa Tamisemi na yule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na kuahidi kuwa itatolewa hadharani baada ya maofisa hao wa serikali kumaliza kazi ya kuipitia.

Hata hivyo, kabla Pinda hajatoa kauli hiyo, wiki kadhaa zilizopita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alidokeza kuwa Serikali ingekichukua kituo cha Ubungo kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwisho wa mwezi uliopita.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilianza kukusanya mapato Ubungo kuanzia mapema jana asubuhi.

Nipashe iliziona risiti zilizokuwa zikitumika kukusanyia mapato zikiwa zimeandikwa jina la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ikidhihirisha kuwa kampuni ya familia ya Kingunge imenyang'anywa rasmi zabuni hiyo.

Gazeti hili lilifika kituoni hapo, asubuhi na kushuhudia foleni kubwa ya mabasi ambayo yalikuwa yakitoka kituoni hapo kuelekea mikoani na nchi jirani.

Watozaji wa ushuru walikuwa wakifanya kazi hiyo huku wakiwa wamevaa vizibao vilivyokuwa vimeandikwa jina la Halmashauri hiyo.

Ingawa wakusanya mapato kuwa zaidi ya wawili kituoni hapo, lakini haikusaidia kupunguza foleni ya magari na kusababisha mabasi kuchelewa kuondoka kueleka mikoani.

Baadhi ya wasafiri waliozungumza na gazeti hili, ndani ya kituo hicho walisema pamoja na serikali kuchukua zabuni hiyo inapaswa kuongeza watendaji wake ili kuondokana na foleni zisizo za lazima.

Mmoja wa wasafiri waliokutwa kituoni hapo wakiwa kwenye moja ya mabasi yanayofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kuelekea Arusha, Michael Damian, alisema uchache wa wafanyakazi ndio unaosababisha foleni hiyo.

Amina Athuman, aliyekuwa akielekea Mbeya, alisema utaratibu mbovu wa uchukuaji wa fedha za ushuru unaofanywa na wafanyakazi hao ndio unaosababisha foleni hiyo.

"Sidhani kama uchache wao ni tatizo. Mpaka serikali imewaweka hivyo haina maana kuwa ni wachache, nafikiri wanatakiwa kujipanga hasa magari yanapofika eneo karibu na geti la kutokea wawe tayari wameshachukua fedha, wasisubiri mpaka gari lifike mlangoni kabisa," alisema.

Msimamizi wa Kituo cha Trafiki Polisi kilichopo ndani ya kituo cha Ubungo, Hassan Hamadi, alithibitisha kuwepo kwa kero ya foleni kituoni hapo jana.

Hata hivyo, alisema hali hiyo imesababishwa na ugeni wa watumishi hao na kueleza kuwa kadri wanavyoendelea nayo foleni itapungua.

The Dar es Salaam City Council has announced tenders for fee collection at the city's Ubungo bus terminal.The DCC Director said in a newspaper advertisement that the council was expecting to privatize fee collection at the terminal for the 2013/14 and were thus inviting application from interested bidders for the offer.

The tenders will be according to rules and regulations under the procurement laws of the country.

The Director of the Dar es Salaam City Council, Mr. Wilson Kabwe, said in an interview that the new move was aimed at increasing revenue collection and improving efficiency at the terminal.

"We thought it was pertinent to have a transparent process of privatizing fee collection. We are expecting increased revenue collection and improved efficiency at the terminal," he said.

Poor service seen in the form of stranded passengers, annoying touts, and series of demolitions, have often characterized the running of the terminal opened in 1999 for internal and external bus service.

Concerns about corruption and inefficiency have also clouded operations in the terminal which was once under the management of Smart Holding Company linked to the family of a veteran politician, Mr Kingunge Ngombale Mwiru.

An audit report carried out by the CAG showed that UBT was losing TZS 3,118,629m a day under Smart Holding Company.
 
Hongera sana Serikali kuona ufisadi hapo Ubungo na kuchukua hatua. sasa vp wale mafisadi papa? washughulikieni haraka kama mlivyo fanya Ubungo.
 
hongera sana serikali kuona ufisadi hapo ubungo na kuchukua hatua. Sasa vp wale mafisadi papa? Washughulikieni haraka kama mlivyo fanya ubungo.

ripoti inanasema nini??????????? Tunaomba tujuzwe juu ya hili. Je mkataba umevunjwa au vipi sababu za kuvunja ni zipi, mambo yawe wazi.
 
huu ni utapeli na kiini macho tu kama kawa..hapa ni kuwa itakuja kampuni nyingine ambayo ina 'koneksheni' na wakubwa na mchezo utakuwa ule ule ...
 
du kampuni haimilikiwi na familia hiyo pekee!!

MASIHARA HAYO kwani Victor MWIRU NA PERES MWIRU utawatengaje na familia ya kingunge ngombale MWIRU?
 
Jiji ndo wanakusanya mapato? Ngoja tuyaone ila nina shaka sana na efficiency yao.Kuna mtu alitania kuwa kuwa hela zitaishia mifukoni mwa watu watagawana kila mtu gari kadhaa maisha yanaendelea na huduma zinazidi kudhoofika
 
This will be more worse!!! Jiji likusanye mapato? yale yale ya RETCO na nyinginezo!!!
 
Jiji ndo wanakusanya mapato? Ngoja tuyaone ila nina shaka sana na efficiency yao.Kuna mtu alitania kuwa kuwa hela zitaishia mifukoni mwa watu watagawana kila mtu gari kadhaa maisha yanaendelea na huduma zinazidi kudhoofika
hata mimi mkubwa natilia shaka sana uwezo wao kwenye kuifanya kazi hii. Najua wataanza kwa moto kama kawaida yao lakini tatizo litakuja kwenye kumaintain the standards. Hapa ndio tunapochemkaga zaidi. Monitoring and time to time evaluation inahitajika kama kweli nchi inataka kufaidika na kituo hiki kikubwa.
 
mimi naona hawa jiji ndio waliochongea kampuni ya kingunge maana wanataka na wenyewe kula sasa mtaona kama hatujaambiwa kuwa hakuna kinachokusanywa kutoka kituoni, ufisadi tu kila sehemu
 
Wakuu kuna m2 mwenye ripoti ya CAG kuhusu mapato ya hiyo stendi aimwage hapa?
 
Wabunge na biashara. Kumbe kampuni ni ya Kingunge! Kudadeki Tanzania tunaliwa!
 
Masanilo,

Do you have an idea of the best way to run the Bus terminal?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu, kichwa cha habari kimekosewa. Kingesomeka hivi:
VIONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI WAANZA KUFAIDI MAPATO UBT
 
Jiji watakusanya kwa muda mfupi wakati wanasubiri mchakato wa kumpata mkusunyaji baada ya tenda. Hii siyo kazi yao ya kudumu.

Victor Mwiru na Peres Mwiru na Ngombale Mwiru....you dont need to have a master degree to connect 'em dots...

Only in Madafuland.

MJ
 
Kweli wajinga ndio waliwao. Hivi J'iji' linahitaji vitendea kazi gani mahsusi saaaana na ma-expert waliobobea gani mpaka hiyo kazi ya kukusanya kodi na makorokocho mengine kwenye hiyo gereji mpaka wahitaji mzabuni? Mwe! Nchi kweli imejaa watu vichwa boga.
 
Romana Mallya | Nipashe

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza rasmi kukusanya mapato katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) baada ya mkataba wa kampuni binafsi inayomilikiwa na familia ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyokuwa ikifanya kazi hiyo kukatishwa.

Kampuni ya Smart Holdings, inayomilikiwa na familia ya Mbunge huyo wa kuteuliwa ilipewa zabuni ya kukusanya mapato kituoni hapo na imekuwa akifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kutolewa malalamiko kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikikusanya mapato makubwa, lakini ikiishia kuilipa serikali fedha kidogo Sh. 1,500,000 tu kwa siku hata kama imekusanya mapato makubwa zaidi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotembelea kituo hicho Machi mwaka huu, alimuagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kufanya uchunguzi na kuwasilisha taarifa ofisini kwake.

Aidha, Pinda alimwagiza CAG kukagua ukusanyaji wa mapato katika Soko Kuu la Kariakoo.

Utouh alikabidhi ripoti ya Ubungo kwa Pinda mjini Dodoma Julai mwaka huu wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge.

Hata hivyo, Pinda wiki iliyopita wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni alisema kuwa ripoti hiyo inapitiwa na Katibu Mkuu wa Tamisemi na yule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na kuahidi kuwa itatolewa hadharani baada ya maofisa hao wa serikali kumaliza kazi ya kuipitia.

Hata hivyo, kabla Pinda hajatoa kauli hiyo, wiki kadhaa zilizopita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alidokeza kuwa Serikali ingekichukua kituo cha Ubungo kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwisho wa mwezi uliopita.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilianza kukusanya mapato Ubungo kuanzia mapema jana asubuhi.

Nipashe iliziona risiti zilizokuwa zikitumika kukusanyia mapato zikiwa zimeandikwa jina la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ikidhihirisha kuwa kampuni ya familia ya Kingunge imenyang'anywa rasmi zabuni hiyo.

Gazeti hili lilifika kituoni hapo, asubuhi na kushuhudia foleni kubwa ya mabasi ambayo yalikuwa yakitoka kituoni hapo kuelekea mikoani na nchi jirani.

Watozaji wa ushuru walikuwa wakifanya kazi hiyo huku wakiwa wamevaa vizibao vilivyokuwa vimeandikwa jina la Halmashauri hiyo.

Ingawa wakusanya mapato kuwa zaidi ya wawili kituoni hapo, lakini haikusaidia kupunguza foleni ya magari na kusababisha mabasi kuchelewa kuondoka kueleka mikoani.

Baadhi ya wasafiri waliozungumza na gazeti hili, ndani ya kituo hicho walisema pamoja na serikali kuchukua zabuni hiyo inapaswa kuongeza watendaji wake ili kuondokana na foleni zisizo za lazima.

Mmoja wa wasafiri waliokutwa kituoni hapo wakiwa kwenye moja ya mabasi yanayofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kuelekea Arusha, Michael Damian, alisema uchache wa wafanyakazi ndio unaosababisha foleni hiyo.

Amina Athuman, aliyekuwa akielekea Mbeya, alisema utaratibu mbovu wa uchukuaji wa fedha za ushuru unaofanywa na wafanyakazi hao ndio unaosababisha foleni hiyo.

"Sidhani kama uchache wao ni tatizo. Mpaka serikali imewaweka hivyo haina maana kuwa ni wachache, nafikiri wanatakiwa kujipanga hasa magari yanapofika eneo karibu na geti la kutokea wawe tayari wameshachukua fedha, wasisubiri mpaka gari lifike mlangoni kabisa," alisema.

Msimamizi wa Kituo cha Trafiki Polisi kilichopo ndani ya kituo cha Ubungo, Hassan Hamadi, alithibitisha kuwepo kwa kero ya foleni kituoni hapo jana.

Hata hivyo, alisema hali hiyo imesababishwa na ugeni wa watumishi hao na kueleza kuwa kadri wanavyoendelea nayo foleni itapungua.
 
Sirikali ilikuwa inatumia Kingunge kukusanya kodi. Kazi kweli kweli. Hivi hakuna City of Dar Es Salaam? Wao wanapata wapi fedha za kuendesha jiji?
 
Back
Top Bottom