Akina baba kushiriki afya ya uzazi ni ndoto

m2me

Member
Jul 23, 2012
64
95
Ni muda mrefu jamii hasa akina baba wamekuwa wakiimizwa kushiriki Afya ya uzazi kwa maelezo kuwa akina baba wanaposhiriki kikamilifu husaidia kupunguza vifo vinavyotokana na matatizo ya uzazi.

Mimi ni mmojawapo wa watu waliokuwa wamehamasika nakuwa mstari wa mbele kutimiza kampeni hiyo ya kupunguza vifo, lakini sasa nimekata tamaa na hiyo itabaki kuwa kazi ya mke wangu.

Mara kadha nimepeleka watoto hospitali nikiwa na mke wangu lakini inapofika wakati wa majibu ya vipimo mimi hutolewa nje na hata pale mke anaposisitiza huwepo wangu daktari hugoma.

Leo nimempeleka mke wangu kwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake baada ya kulalamika tumbo lakini cha kushangaza Dr. amenitoa nje ili mke wangu apande kitandani kwa ajili ya uchunguzi. Mke wangu kamuuliza Dr. kwanini atolewe nje wakati ni mme wangu lakini Dr. kashikiria msimamo wake.

Sijui kitaaluma ikoje lakini nahisi madaktari wanaingilia Uhuru wa wanandoa walioamua kushirikiana kwa kila jambo kufuatia kuaminishwa na vitabu vitakatifu kuwa wao ni mwili mmoja.

Kulikuwepo na mjadala wa wanaume kushuhudia wake zao wakijifungua na majibu yalikuwa kuwa wanaruhusiwa tatizo ni kukosa faragha kwa wazazi wengine katika wodi zinazotumiwa na mtu zaidi ya mmoja.

Sasa najiuliza, kama kuangaliwa tumbo tu tena katika chumba cha peke yako ni shida namna hii je wakati wa kujifungua itawezekanaje?

Naimani hapa wapo wataalamu na wenye mamlaka, uenda mimi na wenzangu tukapata majibu ya kwanini akina baba tutengwe na kudhalilishwa kiasi hicho. Unabaki nje kama dereva aliyekodiwa wakati umeacha shughuli zako kushiriki afya ya familia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom