Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
Kutana na jamaa aliyekimbiwa na mkewe kwa sababu ya umaskini lakini hivi maajuzi alishinda shilingi milioni 20 pesa za Kenya! Jina lake ni Joseph Onywera, ana miaka 62 kutoka kijiji cha Kapiyo eneo la Kano huko Kisumu nchini Kenya.
Joseph anasema kwamba kabla ya kushinda milioni hizi, alikuwa fukara kupindukia, jambo ambalo halikumfurahisha mkewe, ambaye alichoka na baadaye kumkimbia. Alitumia shilingi 100 pekee alizokuwa nazi kwa kubashiri mchuano wa soka na kushinda jackpot. Kweli mungu halali.