Akili yangu Imeshachoka sasa Narudi (Tunarudi nyumbani) Nipokeeni ndugu yenu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,353
11,491
Katika maisha Binadamu Hupitia hatua 3 muhimu sana. Huanza na 1. utoto. 2. ujana/utu uzima 3. uzee. VIVYO HIVYO KWENYE SIASA.

1. kipindi hiki ubongo wa mtoto huwa unakuwa haujakomaa na ndo maana mtoto anaweza kujisaidia kwenye nguo,kuongea maneno yasiyoeleweka, kutoweza kuchambua mema na mabaya,kuropoka au kunena lolote limjialo mdomoni na ndo maana mtu mzima akiwa na mambo kama haya wanasema "anafanya mambo ya kitoto" kwa mtoto huwa ni ruhusa kabisa haishangazi sana.

2. hapa tunategemea ubongo wa binadamu huyu uwe umekomaa unafaham mema na mabaya. una uwezo wa kuchambua na ku pangisha mambo mbalimbali kwnye vyumba vya ubongo huko kichwani. hatua hii binadamu huyu anajitambua na anaendesha mambo yake kwa ustadi.

3. uzee, hapa ubongo hurudi tena hatua ya kwanza ya utoto. hivyo si ajabu tena mtu huyu akaanza kufanya mambo ya kitoto. kwa asilimia 70- 100 akarudia yale mambo ya hatua ya kwanza. huyu sasa hana nguvu ,hana uwezo wa kufikiri na wakati mwingine huropoka, hutembea kwa kuchechemea au kuyumba kama MLEVI, MTOTO NA MGONJWA. huyu binadamu katika hatua hii hushinda nyumban au hurudi kukaa nyumbani asubiri kulelewa.


wanasiasa wetu kwa wakati tofauti tofaut hupitia Hatua hizo. Kuna ambao walikuwa chama A wakawa na akili za kitoto,kilevi na kigonjwa. wakahamia chama B wakapata changamoto akili zao zikafanya kazi wakajielewa. baadaye wakaanza tena kudumaa kiakili hivyo wakarudia hatua ya kwanza yaani chama A kwa kuwa akili zao zimeshachoka hawana uwezo tena. wakarudi nyumbani kwao. WASWAHILI Wanasema "MWENDA TEZI NA OMO MAREJEO NGAMANI"

Mwenye kuelewa na aelewe.
 
Nenda tu baba,Ila jina la MKIA linakuhusu,binafsi nimeogopa kunywa supu ya mkia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom