Akili ya binadamu

Nadhani naanza kupata clue.
Ngoja niende mdogo mdogo maana mpaka kesho nahangaisha mawazo yangu kuhusu uwezo wetu wa kumbukumbu hususani ukubwa wa akili zetu.. Na huu ujio wa AI ndiyo kabisaa naona kumbe bado hatujawahi kutumia akili zetu kwa uwezo unaotakiwa kukidhi viwango vya akili....

Ngoja nisome taratibu
fanya hivyo mkuu usiwe na haraka kabisa.
 
Mkuu OMOYOGWANE
Kuna mechanism gani ya mtu kujua kuwa hapa nilipo naota..
Yaani nipo ndotoni lakini najua kuwa hapa naota..
Hii inanitokea sana..?
 
hilo swali ulilo uliza ni swali la PSYCHIATRY/MENTAL HEALTH unaweza kuona umeuliza swali dogo ila ni kubwa sana na majibu yake ukiyajua utakuwa sawa na daktari yeyote namaanisha MD wa nchi hii kwenye eneo la afya ya akili wewe soma uzi wote uuelewe upate kitu mwezi wa sita au saba nkiwa na muda ntakuja kuendelea nilipoishia ntaufufua huu uzi tuombe uzima.
Pia kuna issue inayoambatana na tatizo la stroke yaani kupooza. nayo ni NEUROLOGY. Kwenye eneo la kufahamu uwezo wa AKILI, tunawezaje kumfanya mtu anayepoteza kumbukumbu kupitia tatizo la neurology kurejea kwenye hali ya kawaida.

Ukirejea, jibu swali hili pia la uwepo wa immaginary cloud kwenye kila akili ambapo kumbukumbu zinahifadhiwa. kKule kwenye pg ya kwanza ulisema kuwa memory zinaweza kufutwa... how?
 
Natumai mko poa pamoja na hizi tozo.

Mind-body dualism hii ni dhana kwamba akili(mind) na mwili(body) wa binadamu ni vitu viwili tofauti kila kimoja kinajitegemea kivyake.Dhana hii ilikua maarufu katika karne ya 17 kutokana na mwanamahesabu wa ufaransa aitwaye René Descartes,alikua na msemo wa kilatin “Cogito, ergo sum,” kwa kiingereza ni "I think, therefore I am” kwa lugha nyepesi ntasema "You are not your mind, you are the one listening to it" yanii wewe sio akili yako wewe ni yule unaesikiliza akili inakwambia nini.

Akili(mind) inahusisha ufahamu (consciousness) hii inafanya akili igawanyike kwenye makundi makuu matatu hii dhanaria ilikuwepo kitambo lakini ilielezewa vizuri na mwanasaikolojia kutoka Austria,bwana Sigmund Freud.

Makundi ya akili ya binadamu
1.unconscious mind
2.subconscious mind na
3.conscious mind

1.UNCONSCIOUS MIND.

Akili hii imeundwa na hisia,tabia,mawazo,mihemko kwa ujumla kumbukumbu za zamani au za sasa ambazo mara nyingi huwa ni za kuogofya au za kututia aibu,hivyo tunazipotezea na tunaziweka nje ya ufahamu wetu tusiweze kuzikumbuka.

Ingawa hatujui uwepo wa kumbukumbuku hizi ila zina ushawishi mkubwa juu ya tabia zetu za kila siku,zinaweza kusababisha shida kadhaa, pamoja na
hasira,woga,tabia ya kuchaguachagua vitu(mfano chakula),mwingiliano mgumu wa kijamii na shida kwenye mahusiano.Freud aliamini kuwa wakati mwingine kumbukumbu hizi zilizofichwa hujidhihirisha kupitia ndoto na kuteleza kwa ulimi(ulimi hauna mfupa).


2. SUBCONSCIOUS MIND.

Akili hii imeundwa na kumbukumbu zote zinazohitajika kukumbukika kwa urahisi, kama tarehe ya siku yako ya kuzaliwa,inashikilia kumbukumbu tunazotumia kila siku, kama tabia na hisia.Pia hushughulika na kila kitu ambacho mwili wako unahitaji kufanya kazi vizuri, kutoka mfumo wa chakula hadi mfumo wa upumuaji hata unapokua umelala na pia ndio chanzo cha ndoto tunazoziota hata kama tukiwa tumelala na hatujitambui.

Subconscious mind mara nyingi huwa inahusishwa na imani kwani ina nguvu sana katika maisha ya binadamu, miujiza yote kama uponyaji huwa inatokea kwenye akili hii mtu anapoamini,kwasababu wazo lolote tunalopanda katika akili hii aidha baya au zuri kwa kurudiarudia siku moja litakuwa ukweli(maneno uumba) hivyo tunahitaji kuwa makini sana na mambo tunayofikiria na kuyaongea.Tukiwaza vitu hasi(negative) itatupelekea kutokuwa na furaha,afya bora na kutofaulu katika maisha yetu pia tukiwaza vitu chanya (positive) tutapata furaha,afya bora na utafanikiwa kwenye maisha yetu.

Kwa kuchukua udhibiti wa akili hii, tunaweza kuwa na uhakika wa kudhibiti tena maisha yetu na kufanikisha chochote tunachotaka. Hii ni kwa sababu wakati subconscious mind, conscious mind na mwili(body) zinapofanya kazi pamoja ili kufikia lengo moja, tunaweza kuamini kwamba lengo hilo litafanikiwa kivyovyote. Meditation ni njia rahisi zaidi inayoweza kutuunganisha na akili hii.


3. CONSCIOUS MIND.

Akili hii inahusisha vitu tunavyotambua na ambavyo tunavifikiria hivi sasa kwa mfano, unavyousoma huu uzi, sauti ya muziki unaosikiliza na kufanya mazungumzo.

Akiili hii ndio mlango wa taarifa kwa njia ya picha au sauti kutoka kwenye mazingira ya nje yanayomzunguka binadamu na kuzihifadhi kwenye akili nyingine za binadamu,pia ni kupitia akili hii ndio tunaweza kufikia subconscious mind na kuficha na kufukia kumbukumbu nyingine kwenye unconscious mind.




Fisherman.
Mbona point ya mwisho umepalasa?
 
Mkuu kila siku mutu anaota vitu mbali mbali mpaka kupiga miti mtu, tena basi unakojoa kabisaaa kojo mwaa, inatokeaga hasa ukiwa na ugwadu wa muda mrefu!! hapa umehusisha ubongo lazima!! na pia

ndoto nyingine kibao tu...... mtu mwenye afya ana wastani wa ndoto kumi kwa usiku mmoja, hapa ni akili inatumika mkuu! huwezi ota bila kuhusha akili never! tena nitendo la miaka kibao, hata Farao alikuwa muotaji, amabae sijawahi sikia aliota ni Yesu tu!

Mfano huwa ninawaza misamiati mingi sana, ya lugha ya kiingereza nikistuka tu naandika, asubuhi nikija kwa Dictionary yaani ni kweli kabisaa na nilicho kiota,

kwa mfano leo hii nimeota mneno mawili ya kiingereza mojawapo ni aprinox, nikaliandika, asubuhi kucheck hili neno lipo kweli! yaani huwa najishangaa kindoto! akili lazima ilihusika Medulla Oblongata! na maamuzi ya kuandika nisisahau ni ya ubongo pia! iko hivi

Ni either mtu asahau au akumbuke baadhi ya ndoto zake hizo!! je nakuuliza hapa kinacho fanya kazi ni nini km si ubongo? njia pekee ya Kupumzisha ubongo ni kuamua wewe mwenyewe wkt umekaa au umejilaza kitandani na kusema

''sitaki kuwaza chochote ; kitu unapiga hola na huwazi kabisaa hata masaa 3, lkn ukifanya uamuzi huu wkt umejilaza kwa kitanda lazima usingizi ukubebe na huko utaota lazima! elezea hii mkuu ikoje? kulingana na ufahamu wako!!
Mkuu hapa napingana na wewe kwenye hilo swala la kuamka na kuandika huo msamiati, kiukweli kabisa binadamu tuna sehemu mboli za memory storage ambazo ni temporary and permanent storage, hiyo temporary ni ile ambayo mtu unaihifadhi kwa muda mfupi tu baada ya kuona au kusikia kitu na hufutika haraka sasa ili kitu kiende kwenye permanent storage unahitaji kurudia rudia mara nyingi hilo jambo either jina la mtu,namba ya simu,sura,maneno,njia,nyimbo etc. Sasa wewe hilo neno la kiingereza sio kwamba lilikuja tu automatically bali kuna sehemu uliliona au kulisikia ila kwa kuwa hukulitilia maanani basi ubongo ukahifadhi kwenye temporary storage , hii pia hutokea sana kuna kipindi unakuta umeota ndoto na kwenye hiyo ndoto kuna sira ngeni tu ,hiyo pia sio bahati mbaya ni kwamba ubongo uli store picha za watu wakati unatembea so during bedtime hizo memories zinaanza kuji play
 
Pia kuna issue inayoambatana na tatizo la stroke yaani kupooza. nayo ni NEUROLOGY. Kwenye eneo la kufahamu uwezo wa AKILI, tunawezaje kumfanya mtu anayepoteza kumbukumbu kupitia tatizo la neurology kurejea kwenye hali ya kawaida.

Ukirejea, jibu swali hili pia la uwepo wa immaginary cloud kwenye kila akili ambapo kumbukumbu zinahifadhiwa. kKule kwenye pg ya kwanza ulisema kuwa memory zinaweza kufutwa... how?
Mh. Hakuna tatizo linaloitwa neurology...!!
Neurology ni muunganiko wa masomo/mafundisho yote yanayohusu neurones/mfumo wa fahamu wa binadamu/wanyama! Ni sawa na masomo yahusuyo urology, oncology, orthopaedics n.k,
Pia kupoteza kumbukumbu halijawahi kuwa tatizo, tatizo ni unapoteza kumbukumbu kwa kiwango gan...!!?
The creator/mother nature vyovyote unavyoita na kuamini! Aliweka memory loss purposely, laiti kama kila tunachopitia kuona, kuhisi, kusikia, kugusa na kunusa memory zake zingekuwa permanent hii dunia isingekalika!
Lakini mother nature through memory loss ameneutralize mambo!
Kila kitu kwenye mwili wa binadamu kina ideal condition yake kikipungua au kikizidi ndiyo tunaita tatizo sasa,
mfano blood pressure, ikiwa juu ya wastani ni tatizo na ikiwa chini ya wastani pia ni tatizo,
Sukari(sugar/glucose) ikiwa juu ya wastani ni tatizo na ikiwa chini ni tatizo pia...!
Umewahi kujiuliza kwanini na kwa namna gani magonjwa(diseases) au disorders zinatokea??!



Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Mwenzetu aliyetoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa fahamu na ubongo, amejitahidi sana kutokuwa biased hasa pale alipoliweka somo hili kwa mtindo wa maswali...!
Amefanya somo limekuwa rahisi kueleweka kwasababu, kuna mtu anauliza swali linalofanana na mfumo wa fahamu lakini specific limebase kwenye socialogy, au psychology, au psychiatric, au neurology, au imani za kidini kabisa...! Mtoa mada endapo kama angeanza kuleta desa moja kwa moja asingeweza kukata kiu za hawa wasomaji wote...!! The nerve system is a complex system amongst!
Mungu ameweka mifumo mbalimbali ili mwili wa binadamu ufanye kazi vizuri lakini mfumo wa fahamu ndiyo baba lao...!!

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom