Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Kuna tajiri aliamua kupima akili za binadamu, aliamua kutafuta vijana watatu aliwapa milioni 50 kila mmoja, akiwataka wajikwamue kutoka kwenye umasikini.
1. Alitafuta shule aliongeza kiwango cha elimu yake, aliamua kupambana na shule, na kila course aliyosoma alihakikisha amefaulu vizuri.
2. Aliamua kuanzisha biashara, alifanya mabadiliko katika mfumo watu waliouzoea na kufanya biashara kutumia utandawazi. Alitangaza biashara zake kwa kutumia simu yake, redio, magazeti na luninga.
3. Aliamuma kujibadilisha yeye mwenyewe, milioni 50 ile, aliamua kutafuta sehemu yenye hadhi yake kwenda kuishi, alinunua TV mpya, mziki wa nguvu, furniture yote ya ndani pamoja na pamba yake yeye mwenyewe.
Baada ya miaka mitatu yule tajiri alitaka kujua maendeleo ya pesa zake.
1. Alisema nimeamua kuwekeza kwenye elimu kwakua ninafahamu ujuzi nitakoupata hakuna mtu anaweza kuniibia, utanisaidia mimi kwa njia mbali mbali, nikiamua kufanya bishara, kilimo au kupata ajira.
2. Alisema niko tayari kukurudishia pesa yako, katika hii miaka mitatu milioni yako 50 imeezaa maratatu. Yule tajiri alifurahi na alimwambia ile ilikuwa ni zawadi tu.
3. Alimkutua jamaa ana hali mbaya sana, kule alikohamia alishidwa kumudu kodi. Hali yake ni mbaya kuliko alivyokuwa kabla ya kupewa milioni 50. Ana madeni mengi sana, ana maadui wengi kwani alipata marafiki wa ajabu wakati wa kutumia pesa. Hana hata pa kukaa.