Akili na Bahati kipi cha kwanza?

Carbondioxide

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
733
195
Akili na Bahati kipi cha kwanza?
Mfano:Tumeenda machimbo tumechimba madini kwa mwaka mmoja hatujapata madini.

Afu gafla kuna vijana wengine watokea nao wanataka kuchimba madini baada ya wiki mbili tu wamepata madini.Je aliekaa mwaka mmoja mgidini bila kupata madini ana akili au ana bahati?

Na je wale vijana waliokaa wiki mbili wakapata madini wana akili au wanabahati?
 
Kuna tafiti huwa zinafanywa kitaalamu kwanza ili kujua chini ya Ardhi kuna dhahabu au hakuna? Kuna Oil au hakuna? Kuna Gesi au hakuna? Na mengineyo, huwezi kuchimba tu kama kipofu!

Binafsi siamini "Bahati" kama ipo kweli ni mambo ya kiimani tu bali hayana uhalisia wowote,

Mafanikiohuja kwa Juhudi,Maarifa na Mipango na sio bahati,

Kwa mfano unajiingiza kwenye biashara ya kuuza Magari bila kuifanyia research! Biashara ikibuma unasema huna bahati? Au umerogwa? Hakuna kitu Bahati kwa imani yangu binafsi,

Pengine hao waliokuja nyuma yenu na wakapata Dhahabu kabla yenu wao wana utaalamu zaidi yenu kwa kuungalia tu mwamba na kujua dalili za sehemu ambazo kuna dhahabu.
 
Back
Top Bottom