CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Mara baada tu ya matokeo ya uchaguzi viongozi wakuu wa CHADEMA walidai hawawezi kubariki uchafuzi na kwamba hakuna mbunge wao atakubali kuapishwa. Sasa wameapishwa!
Nimesikia Lissu akihojiwa leo na TV kuhusu kuapishwa wabunge wa CHADEMA naye akadai kwamba anajisikia kama Yesu aliyesalitiwa. Hapo hapo akaongeza kwamba mapambano lazima yafanyike nje na ndani! Hakutaka kujibu swali lililomtaka aeleze kama chama chake sasa kinayatambua matokeo au la!
Maswali yangu kwa Mbowe
1. Je, sasa CHADEMA kinatambua matokeo ya uchaguzi? Haoni kuwa dunia inaona hawana msimamo na ni kweli walishindwa kwenye sanduku la kura?
2. Je, yule wa Mpanda aliyekaidi agizo lake ataadhibiwa ikiwa hawa wamefanya alichofanya?
3. Ule mpango wa wabunge wa jimbo kuchangia 500000 na wa viti maalum 1M utaendelea ukitilia maanani sasa wachangiaji watakuwa wachache mno? Wa Mpanda akigoma mtamfanya nini?
4. Je, kitendo cha kukubali kushiriki bunge sio sawa na kuwasaliti wenzao wanaodai wanakimbia kwa kuhofia maisha yao? Iweje wanaodaiwa kuhatarisha maisha ya wenzenu ndio wanawaapisha? Hivi Halima na Bulaya wanatofauti gani na Lema hadi Lema akimbie hadi kupeleka mke na watoto jela Kenya?
5. Je, Mbowe mmepima faida na hasara ya kushiriki? Au wamama wametoa shinikizo ili waendelee kufaidi posho? Au ni ili walau ruzuku japo kiduchu ipatikane? Hivi ACT mtawaeleza nini ikiwa wao wamealikwa na wameshikilia msimamo ninyi mmeachia? Au na ACT ni suala la njaa na muda tu wataachia?
Kweli adui mwombee njaa. Wengine wakimbia nchi wengine wakimbilia Dodoma!