Akili inayotumika kumponda Hayati Dkt. Magufuli ndio ile ile iliyowagharimu wana Libya

Tanzania haijawahi kupata Rais muharibifu kama Hayati Magufuli.
Hakika aliharibu mpaka tukakosa huduma za jamii Kama maji na umeme wa uhakika na alijaa porojo na kutaka masifa Ila Sasa alieko ndio ameikomboa sana nchi yetu kwa Sasa huduma zote muhimu zimetamalaki na wananchi tunayo maendeleo ya watu yamajaa tele.
Ameharibu sana mpaka ukame ukamuogopa, njaa ikamuogopa, ujinga ukamuogopa, Sasa Giza, ukame, njaa vimerejea mahali pake panapotustahili sisi wananchi wajinga.
 
Ndio kusema kipindi cha jiwe watu walikuwa wanakula mazima na asali?

Embu toa uharo wako hapa
Vipi we unainjoy hali ya sasa ukitaka kwenda saluni hamna huduma inakupasa uvae kofia tu!

Ukitaka kupasi shati inabidi ukoleze mkaa!

Ukitaka kusaga mahindi inakupasa utwange kwenye kinu!

Ukitaka kuoga utoe 200 uuziwe ndoo ya maji chumvi wakati mabomba yapo!

Huku ndio kufungua nchi? Au kwako hii ndio asali na maziwa?
 
Alikuta sukari 1800 je Wakati anaondoka kaacha sh ngap kwa kilo?

Vipi kuhusu Cement kaikuta sh ngap na kaiachaje?

Mafuta ya kula je?

Kiufupi ndani ya utawala wa CCM wote ni walewale wanatofautiana muda tu
Kuna sababu ambazo zilipelekea hayo! Huwezi kuendesha kiwanda bila kufuata utaratibu kodi lazima ilipwe
 
Akili hiyohiyo ndiyo iliyotumika kumsifu na kutesa waliomkosoa.

Gang mwacheni Mama arekebishe nchi,Kimsingi kwa yeyote mwenye akili anachokifanya Mama sasa hivi ndiyo kinachotakiwa kufanyika kasoro kwa Mbowe,ila wenye upeo mpana na wanaoona mbali kisiasa wanajua kwanini anafanya hivyo kwa Mbowe wewe kwa upeo wako huwezi kuelewa.
 
Hawa vilaza na matangopori yao ya vijiweni wanakera sana.
libya imeshakuwa reference ya kila upuuzi unaotaka kuharalishwa.


mtu aliyeko namtumbo ndiye alinaejua asali ya libya ila mkaazi wa benghazi hajui chochote kuhusu hiyo asali.

utasikia:, walibya walikuwa wanapea dola milion 100 wakitaka kuoa
 
Salama humu,

Wale chawa wa awamu ya 6 wanajitahidi sana kufifisha yote mazuri yaliofanyika na kiongozi wa awamu ya 5!

Alikuwa na madhaifu yake kama binadamu ila swala la kukomalia social services ziwe available and accessible kwa umma ndio kitu ambacho wengi wenye akili tutamkumbuka nacho.

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kabisa kuna walakini katika mfumo wa kiuongozi kutokana na yale ambayo tunayashuhudia. Pesa hamna, vitu vinapanda bei juu, huduma za kijamii zinasua sua.

Haya yalitokea Libya pia miaka kadhaa nyuma ambako walikuwa wanakula asali na maziwa hadi kuvimbiwa na kuona kuwa sasa wanahitaji mtu tofauti wasijue kuwa walikuwa na lulu.

Jamaa alikuwa na madhaifu yake ila alikuwa na concern sana na jamii. Huyu ndio aina ya kiongozi anaeweza kutupeleka katika nchi ya asali na maziwa ila tumeamua kudharau na kukejeli sana yote ambayo mazuri yamefanyika kwa ajili ya umma. Wacha tuinjoy malimao sasa baada ya kutukana maepo.

Baba anayejali familia ndio baba bora, awe jambazi, mlevi, malaya hayo sio tija muhimu asimame na majukumu yake na kuhakikisha familia haikosi huduma zote stahiki. Baba mbabaishaji hata akiwa Paroko wa kanisa ni bure tu!
KAMA WENYE AKILI NI AINA YAKO BASI HAKUNA WENYE AKILI! WENGINE TUNAWAONA NI VICHAA TU KAMA YEYE MWENYEWE ALIVYOKUWA ANAJIITA.
 
95 Reactions
Reply
Back
Top Bottom